The Humble Dreamer
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 7,440
- 10,232
Wakuu Salaam;
Nimezunguka madukani kutafuta sukari ili nipate chai angalau nichangamke kipindi hiki cha mvua maana baridi ipo kweli huku duniani niliko, sasa kila duka naloingia naambiwa sukari hamna!
Nimejaribu kwenda hadi maeneo ya stendi lakini bado sukari najibiwa hamna.
Nimeamua ninywe chai na malimao tu maana yenyewe yataifanya hiyo chai hata iwe na ladha. Malimao yenyewe saivi kuyapata ni shughuli haswa mana watu wananunua wakachanganye kwenye mvukizo ili wajifukize.
Nimejaribu kuwauliza watu baadhi wanadai sukari hakuna kila sehemu na watu wameficha stock ila hawana uhakika kama kweli wameficha. Sasa tatizo ni nini wakati juzi limetoka tamko lenye bei elekezi ya sukari?
Kuna mmoja kanidokeza kua, wale waliokua na sukari kabla tamko la bei elekezi halijatoka, waliendelea kuuza kwa bei ile ile ya juu yani 3500. Sasa wakikutwa wanauza bei hiyo au mteja akisema kauziwa kwa bei hiyo, muuzaji anakamatwa.
Kwanini ifikie hali hii sukari iadimike ghafla? Au kweli sukari hamna?
Au wafanya biashara wanaficha sukari?
Kama vipi serikali ije na tathmini mpya juu ya hili swala.
Huko ulipo vipi sukari inapatikana kama kawaida au nako hamna kama maeneo ya huku?
Na vipi kuhusu bei ya sukari huko ulipo? Au unatumia malimao kama mimi?