kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,734
Wana JF wenzangu tangu Rais Magufuli apige marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi kuanzia jana Tarehe 21.02.2016 Sukari imepanda bei kwani maeneo nilipo mimi mfuko wa sukari Kg.25 ambao ulikuwa unauzwa 44,000/= sasa hivi ni Tshs. 47,000/= hadi 48,000/=.
Hii imenipa shida sana kujua kama tamko lile lilikuwa na lengo la kutusaidia sisi wananchi wa kawaida au lilikuwa ni kuwasaidia wafanya biashara hususani wenye viwanda ili wauze hiyo sukari yao kwa bei wanayopanga wao kwani tulisikia kuwa magodown yao yamejaa sukari na wameshindwa kuuza kwa kuwa tu kuna sukari inaingizwa kutoka nje ya nchi.
Ni vema Serikali ikaliangalia hili kwa upeo mkubwa bila kukurupuka kwani kama ina nia ya dhati kusaidia wananchi na hususani wenye hali ya chini itoe bei ilekezi ambayo itakuwa chini ya ile ya sukari kutoka nje ya nchi tofauti na hivyo tutaelewa wazi kuwa mpango unaofanyika ni kuwanufaisha wafanya biashara wakubwa na wenye viwanda vya sukari.