SuitsTailoring Service-DAR ES SALAAM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SuitsTailoring Service-DAR ES SALAAM

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Samwel John, Aug 5, 2009.

 1. S

  Samwel John New Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima zenu wakuu,

  Naomba kuuliza kama kuna member yeyote anayejua tailor mzuri wa suit hapa Dar es salaam, Nina Suit zangu nimetumiwa na jamaa wangu lakini zina kasoro kidogo ya vipimo, ni kubwa kiasi natafuta fundi mzuri anirekebishie.

  Asanteni

  Samwel John
   
 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kabla ya kutumiwa hizo yaani ulikuwa hujawahi kushona suti? Si bora ungemwambia mchizi akutumie jeans........! Sorry am joking.......! Kuna jamaa mitaa ya Ilala bungoni pia wana ofisi kariakoo, wana mafundi almost 20 wanapiga kazi usiku na mchana. Suti kibao unazoziona mitaa ya Posta jamaa ndio wanatengeneza, then wanawabambika wakuja kuwa zimetoka Italy, Hong Kong etc.

  Nimejaribu kucheki namba ya simu ya jamaa lakini bahati mbaya sina. Lakini ukiwa mjanja nyatia duka lolote zuri la nguo Posta waulize kwa kidizaini wahudumu mafundi wao wanapatikana wapi........basi watakutonya.

  I hope this helps
   
 3. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Muone Jeetu, ni fundi mzuri sana. Anapatikana kwa namba 0784-483242.
  Yuko karibu na kitumbini. Itapendeza kama utashona kittu kipya kabisa kuliko kumpa dili la kurekebisha....

  Nimefurahi pia kujifunza kwa kwetunikwetu kuwa kuna mafundi wanawachomekea "wa kuja" wakiwauzia suti za ilala na kudai ni za italy. Hii inaonesha kuwa watanzania tuna uwezo wa kutengeneza vitu vizuri vikauzika lakini mpaka mtu kuamini kuwa product yako ni nzuri, inabidi umdanganye kuwa ni ya nje ya nchi ....
  Jameni, tutafika????
   
  Last edited: Aug 6, 2009
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hiyo biashara iko sana Bankok, Thailand. Unashonewa suti na kuulizwa lebo unayotaka ili wakuwekee. Kama si mataalamu, huwezi kuona tofauti na zile za kwenye maduka makubwa ya ulaya. Ila mbaya ni pale ukiikuta tayari imeshonwa na kuingizwa dukani. Unaweza kununua suti ya dola 50 kwa dola 300.
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Bongo noma, usipime mkuu
   
 6. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani, nani anaweza kutusaidia vigezo vya kuhakikisha suti ni suti ya kiukweli-ukweli :confused:
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni ngumu sana mkuu...kwa vile quality iko juu...! Manake vifaa wanavyotumia ni vya kisasa kama kawa, pili material ya vitambaa wanavyotumia ni classic, labels ndio usipime manake jamaa wanaagiza huko huko zitokako. Kingine ni kuwa wale wenye maduka ndio wanaagiza vitambaa pamoja na labels na kila kitu. Mafundi wanapewa contract za kushona tu kwa kuzingatia style walizopewa.......!

  Kuna Uncle wangu alijitapa sana alipouziwa suti laki tatu pale posta. Nilipokuja kumthibitishia kuwa huo mzigo ni wa Bungoni alichoka.......hata hiyo suti kaisusa...roho inamuuma kila akiiona!
   
 8. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  there is no way you can know,just imagine mpaka gari ya FERRARI,zimekutwa zinatengenezwa fake na you just cant see the difference
   
 9. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni ngumu sana kwa kweli, mimi nilinunua sutu Kariakoo kwa Tsh 70,000 na brand hiyo hiyo ilikuwa inauzwa posta 250,000! Wajanja siju hizi wanakuonesha sutu za 300,000 posta halafu wanakuambia wape 150,000 wakakutolee kumbe wanaenda chukua Kariakoo kwa 70,000 na kuipeleka pressing dry cleaner na kukuuzia 150,000!
   
 10. D

  Dr Berno New Member

  #10
  Aug 6, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nenda R.D Tilors kitumbini (0784483242), they are the best n country, nlishona pia za kwangu hapo
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Nenda KHARID maeneo ya Mnazi mmoja karibu na bank ya NBC mtaa wa Agrey/Jamhuri kwenye kona pale huyu jamaa namwaminia hata Magufuli iwa anashona pale.
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu Fidel,

  Hebu nisaidie kidogo. Magufuli ameingiaje hapa? Una maana ndiye SI unit ya wavaa suti hapa bongo i.e ndiye mwenye suti bomba kuliko wote?
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha mkuu nasisitiza tu jamaa mtaalamu wa kushona mkuu hata Tiba nae iwa anaenda pale kushonesha au ni vibaya Magufuli kushonesha suti maeneo ya mnazi mkuu?
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu. Tuko pamoja. Nilitaka kujua kama Magufuli ndiye kinara wa suti kwa Bongo. Si unajua tena mambo ya role model! Otherwise, ni poa tu kushona suti popote labda kama tunaongelea aina nyingine ya suti. Bongo lugha inakua kila siku!!:rolleyes:
   
 15. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Mkuu Fidel,

  Tiba mbona huwa zinamvaa au unamuongelea Tiba mwingine?.

  MJ
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehe mkuu ndo style yake bana.
   
 17. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hahaha...

  Sasa ni style ya Tiba au ya fundi...lol..sasa fundi mbona hampi ushauri mzee Tiba...Suit zake mabega yako kwenye Bisept na mikono ya suit inaishia kwenye kucha.
   
 18. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nani anashona za Mo Dewji kwa kuwa zake kali kwelikweli..
   
 19. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante Dr. Berno,
  huyo R&D Tailors ndio huyo huyo Jeetu niliyemtaja asubuhi. Suti zake utazipenda nakwambia. Mimi nimeshona pale si chini ya mara tatu, suti koti jamani asikudanganye mtu ....
  Viatu vizuri vya kuvalia suti vinapatikana wapi jamani kwa bei nzuri lakini quality nzuri pia??
   
Loading...