Sugu: Zile hostel za Magufuli tunadanganywa zimejengwa kwa bil 10 wakati ni zaidi ya bil 54, mimi niko kwenye kamati

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
IMG-20180605-WA0010.jpg
 
Nimemsikiliza bungeni, amesema kamati ya bunge iligundua yale majengo yalijengwa kwa zaidi ya bilioni 54 na point na sio bilioni kumi kama serikali inavyotangaza.

Amesema kama kweli yale majengo yangejengwa kwa kwa thamani inayotangazwa na serikali hata yeye angechangia majengo mawili.

Amehoji serikali inamdanganya nani kwa faida gani, wakati fedha ni zetu wote na maendeleo ni yetu sote na kwa nini CAG hakukagua gharama za ule ujenzi.
 
Hata hivyo hapo awali si ilikuwa iwe zaidi ya 90B na zijengwe kwa takribani miaka sita.

Kama haitoshi kawaokoa wanafunzi asilimia kadhaa kuishi maisha hatarishi huko mtaani. Wanywa gongo/mataputapu waliwadhalilisha vijana wetu Huyu Sugu anamtoto binti wa miaka mingapi labda? Ili tuone kama anajua hatari ya kusoma ukiwa umepanga nyumba moja na wala mihadarati na gongo.
 
Kwa hiyo zaidi ya Billion 90 zikitumika zikiwa na nyaraka na nyingine mkaalikana kwenye kuwacheza ngoma wale wali wenu ndio unaona akili.


Tunachohoji ni kudanganyana, wananchi tunajua serikali inabana matumizi kumbe ndio inatumia zaidi.

Haya hiyo bilioni 40 imetumika bila nyaraka zozote zile na watu mnashangilia..
 
Hata hivyo hapo awali si ilikuwa iwe zaidi ya 90B na zijengwe kwa takribani miaka sita.

Kama haitoshi kawaokoa wanafunzi asilimia kadhaa kuishi maisha hatarishi huko mtaani. Wanywa gongo/mataputapu waliwadhalilisha vijana wetu Huyu Sugu anamtoto binti wa miaka mingapi labda? Ili tuone kama anajua hatari ya kusoma ukiwa umepanga nyumba moja na wala mihadarati na gongo.
mkuu usiwe pimbi wa kiasi hicho, kwanza majibu yako hapa yanaonesha hujasoma chuo chochote wewe. aliyekwambia kuna mahusiano kati ya kunywa mataputapu na kusoma ni nani? hivi pale zile hostel zilipo hayo mataputapu hayapatikani? pale na ubungo msewe au ubungo kuna umbali gani?
KINACHONGELEWA HAPA NI GHARAMA, KWMBA GHARAMA TUNAZOTANGAZIWA NI NDOGO KULIKO UHALISIA, WANAOHOJI WANAHOJI NI KWAMBA ANAYEDANGANYA ANADANGANYA KWA FAIDA YA NANI WAKATI PESA NI ZA WALIPA KODI?
HATA UJENGE HOSTEL NZURI VIPIIIIII KAMA HAKUNA MIKOPO YA UHAKIKA KWA WANAFUNZI WA VYUO NI KUJIDANGANYA TUUU
 
54B????? kumbe sio 10B..daaah hawa watu wamezidi kupika hizi data ..wataendelea kuumbuka hv hv..nasikitika kuwa ndugu zangu walioko vijijini bado wana imani na mtu huyu kwakuwa hawana uwezo wa kupata hz taarifa...ila kwakuwa kijana wao nipo hapa nitawafikishia ujumbe maana wao walimshangilia kwa vigelegele wakati akifuta sherehe za uhuru kwa kubana bajeti na sasa bajeti iliyobanwa ndio yatumika vibaya hv

huwa nawashangaa sana hawa wanaojigamba mbele ya umati kuwa ufisadi umezuiwa kwa asilimia kubwa...lakini ukweli ni kuwa ufisadi upo tena ni mkubwa sana...kikubwa ufisadi wa sasa umeongezeka kiteknolojia..hivi sasa keki ya taifa wanoyo ifisadi ni kikundi kidogo ndani ya chama ambacho kimejipa mamlaka makubwa sana..
tutegemee mpasuko mkubwa ndani ya chama kwakuwa keki ni ya wachache msimu huu na hao wachache wanaila kweli kweli
 
Toka 1995 kuiba tuu hadi rambirambi. Hii tasnia ya wizi jamaa ni mweledi halafu anavyojiona mjanja anatubia na kututukana sijaleta tetemeko limeni sitawapa chakula poa aina kweree mr Trillionare
 
Back
Top Bottom