Sugu naye chupuchupu, gari lake lilitaka kuwaka moto. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu naye chupuchupu, gari lake lilitaka kuwaka moto.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Losambo, Jan 17, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wakati bado watu wakiwa katika majonzi mazito ya msiba wa Mh. Regia Mtema gari la Mh. Joseph Mbilinyi aka Sugu nusura iwake moto na kuwateketeza!!!!! Ajali hiyo ya moto ilitokea mkoani Pwani.

  "Kuhusu ajali yake, Sugu alisema kuwa alishangaa gari lake kuwaka moto kwa sababu halikuwa na hitilafu yoyote.
  "Kabla ya kuanza safari ya kutokea Mbeya lilifanyiwa ‘service', tukiwa tumeianza Pwani, tukaanza kusikia harufu ya kitu kinaungua, tukajua ni gari lingine.
  "Tulipofika Kwamatiasi, kuna hiace ilitupita wakatuambia gari linawaka moto. Bahati nzuri tulikuwa na fire extinguisher, tukazima kwa sababu vyuma vya chini vilikuwa vinateketea.
  "Tulikaa pale Kwamatiasi mpaka tukapewa msaada kutoka Makao Makuu ya Chadema ndiyo wakaja mafundi, wakalitengeneza na kulifikisha Dar," alisema Sugu." Mwisho wa nukuu.

  Wabunge wote wa CDM ni kipindi cha kuwa makini sana maana kuna dalili la balaa kuwaandama.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hii imo hapa majukwaani!
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sijaiona hiyo thread, nashukuru kwa taarifa nadhani MoDs watafanya kazi yao.
   
Loading...