Sugu awatukana waandaaji wa fiesta kwenye facebook

Alichoandika mr 2 sugu kuhusu fiesta kwenye wall yake ya facebookkama hii ndio chadema school of thought, muda si mrefu nitarudisha kadi niungane na mtikila.Mods in jf tunasema "where we dare to talk openly"so please if that is true then msiondoe hii thread.
Rudisha hata leo,cdm will wax stronger when you go out.Usitishie nyau watu wazima,tembeaaa.
 
Hahahah..kama mambo yenyewe ndio haya mmmh! Halafu utakuta mtu anajiita Great Thinker halafu ana Kadi ya chama cha kihuni kama cha huyu mheshimiwa!!!

Usiwahukumu wenye kadi za CHADEMA...Sugu alifika pale kama mgombea tu, in short aliwekwa ili wachukue jimbo la Mbeya Mjini, si mtu aliyekua na mizizi wa msingi katika chama...so, walaumu kwa kuwapelekea upupu wananchi wa Mbeya, kadi usirudishe, mtafute Sugu umkanye!!!
 
Amesimama ktk imani halisi ya utetezi wa maslahi ya msanii!
Wale vichwa pasi wataona kakosea lakini wenye kuona mbali tumemkubali!!
 
Picha please kwa wale mliokuwepo ndani ya viwanja vya Dk slaa. pia kwa wale waliokuwepo kwenye kiwanja vya sokoine. Na ninavyojua watu wanavyopenda vitu vya bure lazima tamasha la Mr Two lilifurika watu wengi, vipi balozi nae alikuwepo?
 
Mimi kama mzaliwa wa Mbeya mjini sisemi kama kakosea au hajakosea lakini anatumia juhudi na muda mwingi katika mambo ambayo hayana manufaa kwa waliomchagua abadili vipaumbele.
 
Ninamfahamu sugu kidogo,kwenye kitu anachokiamini na kukitetea huwezi mbadilisha atakudundisha chini tu,kinachofanywa na hao claus na chama cha magamba kwa wa tz ni zaidi ya gilo neno alilolitumia mheshimiwa.
 
Mtu gani mwenye akili timamu anayeweza tena kumchagua mtu anayemwaga mitusi mizito hivyo? Alikosa kabisa njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake kistaarabu?

hivi kabla hajachaguliwa alikuwa hatoi hayo matusi au?
 
Mimi kama mzaliwa wa Mbeya mjini sisemi kama kakosea au hajakosea lakini anatumia juhudi na muda mwingi katika mambo ambayo hayana manufaa kwa waliomchagua abadili vipaumbele.
Hapo umenena. Anahitaji ushauri.
 
Mtu gani mwenye akili timamu anayeweza tena kumchagua mtu anayemwaga mitusi mizito hivyo? Alikosa kabisa njia nyingine ya kufikisha ujumbe wake kistaarabu?
sina nia ya kumtetea yeyote, lakini neno 'tusi' inategemea pia tunalitafsiri vipi, mbona kila siku tunatukwana na hao wanaotutukana ndio tunaowarudisha madarakani, haihitaji akili ya ziada kuona hii nchi imetawaliwa na kila aina ya uchafu na ufisadi, lakini tunapotoa sauti zetu kulalamikia tunajibiwa kwa kejeli na mizaha kuwa leteni ushahidi, je hili sio 'tusi' ?
 
hivi kabla hajachaguliwa alikuwa hatoi hayo matusi au?
Kwa wakati huo tulikuwa tunamtambua Sugu kama msanii, na siamini kama alishawahi kutoa matusi mazito hivyo! Tulimzoea tu kwa malalamiko yake dhidi ya unyonywaji wa wasanii na kazi zao.Tumeshampa Kofia nyingine! Sasa hivi inabidi abehave kutokana na Maadili ya Mhimili wa serikali-Bunge!Hebu jiulize, anatujengea picha gani wananchi dhidi ya Bunge?
 
kuna lugha za kisiasa.

Kuna lugha za kitabibu

Kuna lugha zakitaani

Kwa kiswahil fasaha hapo kwenye lugha unaweza weka REJESTA. Sugu Ame express hisia zake,

Clauds kwanini wamefake sauti yake?

Kama katukana najua fika ametukana ku onesha jinsi alivyochukizwa na unyonyaji wa hao "Radio mawingu"

Ameongelea mambo ya usanii na si chama,ni haki yake kuwatukana. Mbona hamjahoji uhalali wa clauds kufoji sauti yake(sugu)?

Mi nadhani na naona mr2 yupo katika mstari,na amefanya hivyo ili kuonyesha uchungu alionao bila kuficha.
 
Awali nilishasema kuwa chadema ni chama cha wahuni, na mods wakafuta bandiko langu... Sasa angalieni mhuni mbunge huyo!
 
Ushabiki wa kisiasa ukifika kiwango hiki tumekwisha, CDM wanapaswa kujitofautisha na CCM ktk kila eneo. Matusi imekuwa lugha ya kawaida kwa Sugu hata kwnye mikutano ya hadhara, alifanya hivyo Kyela wakati akielezea CDM walivyomsusia JK bungeni. Anawaletea wana Mbeya ugomvi wake na Ruga badala ya maendeleo, hapana hatukumchagua kwa hilo, na hili litawa cost CDM, subirini muone.
 
Sugu amenifurahisha sana, sugu ni tofauti na PIMBI wote kwenye Bongo flava industry, anajiamini na anajua anachofanya. Kuna waosha vinywa humu huwa wanamponda Sugu kwa kujiona wamesoma na wanajua sana lakini let me tel u guys Sugu anajua afanyacho na he goes places for that. Sielewi tafsiri ya ubunge hapa Jf ni nini, mnamfahamu mbunge wa Makadara, Nai? Angalieni mabunge mengine mjifunze. Ubunge ni zaidi ya kuvaa masuti, kutembelea shangingi, kukalili kamusi ya kiswahili fasaha ama kuwa mnafiki hata pale unapokuwa na dukuduku, ni zaidi ya kuiga wale ma ndito, vijana simameni ktk kile mnachoamini. Sugu ni mfano kati ya wengi hasa mh. Mbowe alinifurahisha alipomchapa kibao msimamizi wa uchaguzi kule Hai. Jana nilisliza clouds toka tano asbh ckusikia mbwembwe za Mbeya nadhani walibanwa kiana. Wasanii stukeni mtakwisha. Cowards die many times before their deaths, the valiant never taste of death but once. - Shakespeare.
Kweli mkuu clouds hadi sasa wamekuwa wapole toka jana sijasikia tangazo hata moja la fiesta,
fiesta inakwenda Arusha lakini kimya waige sauti ya kamanda Lema waone moto ni zaidi ya Sugu.
Unajua watu wa type ya ki CCM kama clouds si watu wakuchekea wanafaa watu kama Sugu na Lema na Mbowe
ukileta za kuleta unakula kibao.
 
Hapa "Sugu" kakosea hata atetewe vipi. Hiyo lugha si tu ni mbaya kutamkwa na mbunge bali mtu yoyote yule hata kama ni msanii. Kama hizi ndiyo lugha za kisanii na bado ana taka kuzitumia arudi kwenye mzika. Kashaanza kuchemsha mapema ndiyo maana badala ya kupigia kelele vitu vya maana ana lalamikia Fiesta na ukichunguza ugomvi wake na Fiesta unatokana na bifu personal alilo nalo na watu wa clouds wala asijidai ni kujali wasanii. 2015 toeni huyu mtu.
 
Alichoandika mr 2 sugu kuhusu fiesta kwenye wall yake ya facebookkama hii ndio chadema school of thought, muda si mrefu nitarudisha kadi niungane na mtikila.Mods in jf tunasema "where we dare to talk openly"so please if that is true then msiondoe hii thread.
Mkuu hayo ni maneno ya kimjinimjini tu....ni sawa na kuambiwa huna akili, huna uelekeo, huna maana nk., hakuna tusi hapo.......ukitaka kuyatafsiri upendavyo wewe utatukana. Maneno hayo hayana uhusiano na kuwepo kwako Chamani, we kama unatoka usitafute visingizio.
 
Back
Top Bottom