Sugu atofautiana na Mwenyekiti Mbowe kuhusu uchaguzi 2025

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,159
2,000
Katika pitapita zangu mitandaoni nikoana post ya aliyekuwa mbunge wa mbeya mjini "SUGU" akisema ni lazima awe mbunge 2025.
Hii imenishangaza kwa kuwa hadi sasa msimamo wa mwenyekiti pamoja na chama ni kuwa 2025 hawatashiriki uchaguzi bila tume huru wala katiba mpya.

Sasa nashindwa kuelewa maamuzi haya ya sugu anamaanisha tayari tuna katiba mpya na tume huru?

Kwa nini asingeanza kudai hiyo katiba mpya ndio aje na ndoto za ubunge 2025? Au anataka kuhama chama?

Ila pia ni kwa nini anahisi ana haki sana ya kuwa mbunge? Asipokuwa mbunge kwani shida ni nini?

Nilitegemea wananchi wa Mbeya ndio waseme na sio yeye kusema eti nilazima nitakuwa mbunge.

Ni kweli nyie mlioonja utamu wa ubunge hamuwezi kufanya jambo lingine lolote zaidi ya kuwa wabunge? Hii tabia ipo hadi CCM , Kuna watu wanaamini wao wamezaliwa kuwa wabunge, hawawezi kufanya jambo lingine lolote zaidi ya kuwa wabunge.

Sugu mbona ulituonyesha kuna biashara zako unafanya na ukasema zinaenda vizuri tu? Sasa tena hii hamu ya kusema lazima uwe mbunge 2025 inatoka wapi tena? Pia umeagana na Mungu kuwa utafika hiyo 2025?

Pesa za ubunge ni tamu sana eeh? Si ajabu uliwasaliti wenzio kwenye movement ya ant-virus, ukavuta mpunga ukawaacha hawana njia.

Kwa kauli yako ya leo nitakupinga hapa na hata hiyo 2025.Screenshot_20210618-183354_1.jpg
 
Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
55,207
2,000
Ndio tuna cha kujifunza kutoka kwa wanasiasa....

Wakati wao wako busy na matumbo yao sisi tupo busy kuwapigia makofi, kushangilia U-CCM na U-Chadema na sio U-Taifa kwanza
Miaka yote bungeni, mpunga alovuta, bila shaka ana vyanzo vingine vya kipato (hotel D) ila bado ana ndoto za kuajiriwa.

Huku huko bungeni tunaambiwa vijana wajiajiri..ila wao hawajiajiri na mitaji wanayo tayari.

#Hii nchi imechezewa sana.
 
kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
4,635
2,000
Kachukue chako kwa Tulia Ackson... Jingine lazima usikalili matamko, hapa lazima tumehuru na katiba vitekelezwe ndipo agombee
 
Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,813
2,000
Ndio tuna cha kujifunza kutoka kwa wanasiasa....

Wakati wao wako busy na matumbo yao sisi tupo busy kuwapigia makofi, kushangilia U-CCM na U-Chadema na sio U-Taifa kwanza
Miaka yote bungeni, mpunga alovuta, bila shaka ana vyanzo vingine vya kipato (hotel D) ila bado ana ndoto za kuajiriwa.

Huku huko bungeni tunaambiwa vijana wajiajiri..ila wao hawajiajiri na mitaji wanayo tayari.

#Hii nchi imechezewa sana.
I love Evelyn salt
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,612
2,000
Kutofautiana ni haki yao na hii inajionyesha jinsi demokrasi ilivyokomaa ndani ya CDM
 
chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
771
1,000
Kutofautiana ni haki yao na hii inajionyesha jinsi demokrasi ilivyokomaa ndani ya CDM
Hiyo Democracy inakomaa leo ndani ya CCM? mbona Musiba wa hayati Disamburo hawakuhuduria na wakakataa KABISA kuagwa kwake, sasa hapa pengine wa kumsifia kidogo ni mwenyekiti wao wa CCM, sio kuisifia CCM.
 
Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
3,906
2,000
Tuna ujinga mwingi sana, na ni ngumu kupiga hatua kwa akili hizi....

Kuna mambo yanayohitaji siasa/kichama/ uccm na uchadema na kuna mambo ya msingi yanahitaji sapoti ya wananchi siasa zikae kando. Ila haya hatuelewi.

Ilimradi tunapua inatosha.
Maendeleo hayana chamaa!🤓
 
Agogwe

JF-Expert Member
Feb 20, 2013
2,310
2,000
si huyu mwenyekiti kashasema anastaafu 2023, halafu anawashauri wasishiriki uchaguzi 2025...
 
chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
771
1,000
Eti..??
Vipi kama wanachadema wa Mbeya Mjini watapendekeza mtu mwingine kuwa mgombea? Anajuaje kuwa atapendekezwa yeye?
SUGU anauhakika wa mapenzi ya wana MBEYA kwake ndio maana ana imani ya uhakika kuwa ikiwepo tume huru ya uchaguzi' 2025 atashinda ubunge.
 
Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
8,159
2,000
Ndio tuna cha kujifunza kutoka kwa wanasiasa....

Wakati wao wako busy na matumbo yao sisi tupo busy kuwapigia makofi, kushangilia U-CCM na U-Chadema na sio U-Taifa kwanza
Miaka yote bungeni, mpunga alovuta, bila shaka ana vyanzo vingine vya kipato (hotel D) ila bado ana ndoto za kuajiriwa.

Huku huko bungeni tunaambiwa vijana wajiajiri..ila wao hawajiajiri na mitaji wanayo tayari.

#Hii nchi imechezewa sana.
Wajinga ni washabiki wao, Mimi simo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom