Sugu ashikiliwa na Polisi Mbeya

sekulu

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
988
157
Leo Usiku niliamka kama Saa 8 usiki nikawa nasikiliza Radio,

Nikasikia Sugu akamatwa na polisi Huko eneo la Nzovwe Mbeya Kwa kufanya mkutano kinyume cha sheria, Lakini wakaendelea kusema kwamba eti kamatwa yake inatokana na Kitendo chake cha kufanya Onyesho la bure eneo la Luanda Mbeya, huku pembeni yake uwanja wa Sokoine kukifanyika Tamasha La Fiesta linaloendeshwa na Clouds Fm.

Kuna mtu mwenye Data Zaidi?

SOurce: Radio 5
 
Tena TBC wanasema Sababu za kukamatwa kwake Hakujawekwa wazi na Jeshi la Polisi!, anyway huenda ikawa ni kwa sababu ya Kutaka kufanya onyesho la Bure
 
Mbona Luanda na Uwanja wa Sokoine ni sehemu mbili tofauti?
Sugu tumekuwa tukimsikia akiipromoti fiesta.
Lakini ngoja tukae kimya, habari kamili zitatufikia tu.

Swali la kizushu:-
hivi bunge limeisha? Inakuwaje Sugu awepo jimboni kwake badala ya kuhudhuria vikao vya bunge?
 
sio sauti ya sugu ile kwenye tangazo la fiesta wamechakachua kama kawaida yao
 
Mbona Luanda na Uwanja wa Sokoine ni sehemu mbili tofauti?
Sugu tumekuwa tukimsikia akiipromoti fiesta.
Lakini ngoja tukae kimya, habari kamili zitatufikia tu.

Swali la kizushu:-
hivi bunge limeisha? Inakuwaje Sugu awepo jimboni kwake badala ya kuhudhuria vikao vya bunge?

Hapo kwenye Red, Wapi umemsikia akipromoti??
 
Ishu ni kwamba nasikia na yeye alipanga kufanya Tamasha la Bure kwa wananchi wake,
 
Mbona Luanda na Uwanja wa Sokoine ni sehemu mbili tofauti?
Sugu tumekuwa tukimsikia akiipromoti fiesta.
Lakini ngoja tukae kimya, habari kamili zitatufikia tu.

Swali la kizushu:-
hivi bunge limeisha? Inakuwaje Sugu awepo jimboni kwake badala ya kuhudhuria vikao vya bunge?

Sugu bado anatabia za kihuni, ndio maana utakuta anafanya maajabu tu. ivi nani anaweza kuniambia toka awe mbunge hata kwa kuongea tu ni mchango gani kisha toa? Hili bunge linaloendelea sijasikia alichangia nini. Sugu alijifanya kukataa hao jamaa wa fiesta kuwa wasikanyage jimboni kwake bila kujua kuwa yeye siyo last say, waomba kibari wala huwa hawamuombi mbunge wanaomba serikali, na ninahisi alikuwa anaumia sana alipokuwa akisikia sauti ya Jembe Zitto na yule Diwani wa mbeya wakihamasisha watu waende kwenye huo ufiesta.
 
Hapo kwenye red ndio wabunge wa chama chetu wapo kimajungu zaidi au wewe huyu sugu na kusaga wana bifu la zaidi ya muongo mmoja? alienda kufanya tamasha lake baada ya juhudi za kuzuia fiesta isifanyike kugonga mwamba angefanikiwa angebaki mjengoni.
 
Sugu bado anatabia za kihuni, ndio maana utakuta anafanya maajabu tu. ivi nani anaweza kuniambia toka awe mbunge hata kwa kuongea tu ni mchango gani kisha toa? Hili bunge linaloendelea sijasikia alichangia nini. Sugu alijifanya kukataa hao jamaa wa fiesta kuwa wasikanyage jimboni kwake bila kujua kuwa yeye siyo last say, waomba kibari wala huwa hawamuombi mbunge wanaomba serikali, na ninahisi alikuwa anaumia sana alipokuwa akisikia sauti ya Jembe Zitto na yule Diwani wa mbeya wakihamasisha watu waende kwenye huo ufiesta.

Hapo kwenye Red Ngoja Nicheki kwenye Hansard!, Nakumbuka kuna siku Joseph Mbilinyi Aliongea Bungeni!

Kukamatwa kwake ni wakati anafanya Mkutano wa Hadhara!, Pia aliandaa show Siku ya leo Jumapili Show hiyo itafanyika Buuuure!, na huku upande wa pili hapo hapo Mbeya Mjini Kutakuwa na Onyesho la Fiesta la Clouds Fm!, Alafu kwanini Polisi Hawajaeleza wazi kwanini Kakamatwa??, au walipata Taarifa Za kiintellijentia?
 
Sugu naye aache mabishano yasiyokuwa na tija. Yeye ni Mbunge na sio Mmiliki wa Mbeya. He should be above huu ugomvi wa kitoto kati yake na Clouds FM. Sasa hivi ni mbunge afikirie ni namna gani atainua maisha ya wana-jimbo wake.
 
Hapa maswali ni mengi kuliko majibu. Sababu zinazoelezwa hapa zinaonekana ni hisia zaidi kuliko uhalisia! Kama ameandaa tamasha sambamba na fiesta, mbona j2 haijafika? Na kama "ameandaa" tamasha la bure, hajafuata taratibu? Na mbona wamemkamata kabla ya kutenda kosa lenyewe? Maana leo ni jmosi. Kutakuwa na jambo ambalo bado hatujalijua. Wana jf mby tunategemea mtuletee habari kamili. Kuhusu bungeni, naamini mbunge anajua anachokifanya na kuchangia sio lazima kuongea. Kuna kuchangia kwa maandishi.
 
Sugu naye aache mabishano yasiyokuwa na tija. Yeye ni Mbunge na sio Mmiliki wa Mbeya. He should be above huu ugomvi wa kitoto kati yake na Clouds FM. Sasa hivi ni mbunge afikirie ni namna gani atainua maisha ya wana-jimbo wake.
Naanza kuwa na mashaka na hawa makamanda. Mbunge unafanya mambo ya kihuni tena wa kitoto kiasi hicho, no!
 
Sugu hajaandaa tamasha lolote ila habari kutoka Mby ni kwamba kuna kampuni imeandaa tamasha mby na Sugu ni mgeni rasmi. Wasanii mbalimbali watatumbuiza bure Afande sele, mchizi mox , mkoloni, gsolo na wengine maarufu. Clouds wanahofia fiesta kudoda na hili suala la kumshikilia sugu ni kosa la kiufundi
 
..Waliokuwa maarufu enzi hizoo...
 
Clouds ni matapeli, huwa wanadanganya wanamuziki na kuwarubuni kwa kuwapa fake contract ambazo
haziwanufaishi kabisa, Ukistuka na kutaka kuwakacha mziki wako hautapigwa kamwe hata kama unafunza jamii
pia ni CCM hawa hata matangazo yao utawasikia wanavyoponda upinzani, hawana jipya zaidi ya kunyonya

Sugu toa hisia zako fanya tamasha lako la bure wananchi waburudike baada ya kazi ngumu,
Tena ukaongee na TBL wakupe vinywaji watu wakatike vizuri.
 
Leo Usiku niliamka kama Saa 8 usiki nikawa nasikiliza Radio,

Nikasikia Sugu akamatwa na polisi Huko eneo la Nzovwe Mbeya Kwa kufanya mkutano kinyume cha sheria, Lakini wakaendelea kusema kwamba eti kamatwa yake inatokana na Kitendo chake cha kufanya Onyesho la bure eneo la Luanda Mbeya, huku pembeni yake uwanja wa Sokoine kukifanyika Tamasha La Fiesta linaloendeshwa na Clouds Fm.

Kuna mtu mwenye Data Zaidi?

SOurce: Radio 5

Huu ndo ujinga wa Polisi wa CCM wanao ufanya kila siku alafu baadae wanakuja na kusema anatafuta umaarufu wkt umaarufu huo ni wao wenyewe wanampa
 
Back
Top Bottom