Sugu ashauri watu waache pombe ili kuikomoa Serikali. Unakubaliana naye?

Sep 17, 2021
39
84
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Mbeya kupitia CHADEMA, Joseph Mbilinyi ameshauri watu kuacha kunywa pombe ili waikomoe Serikali ikubali kukaa mezani kujadili Katiba.

Sugu amesema kwa mawazo yao wao CHADEMA ni vyema Serikali ikakosa kipato (Ishindwe kuhudumia wananchi na watu wakose ajira), na hilo litawezekana watu wakiamua kuacha pombe kwa siku kadhaa kwani pombe inachangia kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa.

Wazo hilo limeungwa mkono na baadhi ya watu wa CHADEAM akiwemo mwanaharakati wao Maria Sarungi, ambaye ametaka watu kuchagua siku moja ya kuacha kunya pombe katika kipindiu hiki cha sikukuu.

Vipi wewe Mwana Jamvi, uko tayari kusikitisha pombe msimu huu wa sikukuu ili kuongeza moto wa Katiba?

IMG_0642.jpg
 
Walevi hawafungamani na upande wowote.

Ndio mbunge wetu huyo. Ametoa mawazo chanya kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Amesahau wakati wanagawa viroba kwenye kampeni zao?Au anafikiri hatuna kumbukumbu nzuri?Wajinga?Wapumbavu au AFKANI?
 
Back
Top Bottom