Sugu amlipua january makamba juu ya dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu amlipua january makamba juu ya dowans

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mujumba, Mar 15, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi Mr.Sugu akiwahutubia jana mamia ya wananchi wa Uyole kata ya Insalaga katika mkutano wa hadhala uliofanyika viwanja vya kibonde

  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu (Chadema), amemjia juu Mbunge wa jimbo la Bumbuli, January Makamba (CCM), kwamba anaichezea serikali kutokana na msimamo wake wa kutaka mitambo ya kampuni ya kufua umeme ya Dowans Tanzania Limited ikodishwe kwa ajili ya kuzalisha umeme.
  Akizungumza na wananchi wa Uyole jana jijini hapa, katika mfululizo wa ziara yake ya kuwashukuru kwa kumchagua, Sugu alisema Makamba ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, anaichezea serikali kwa kushinikiza mitambo ya Dowans iwashwe wakati yeye jukumu lake ni kuisimamia serikali.
  Alisema inasikitisha kuona mbunge huyo ambaye ni mwakilishi wa wananchi anakuwa na msimamo kama huo wa kutaka mitambo ya Dowans ikodishwe wakati anafahamu kuwa kuna utata katika mitambo hiyo.
  “Mimi nina historia nimesukuma mkokoteni nikauza mitumba Mwanjelwa na ndiyo maana nina uchungu mpaka ndani maana nayajua maisha. Mimi siyo kama wabunge kama hao ambao wanakwenda bungeni wanasema mitambo ya Dowans ikodishwe, hivi kuna nini kimejificha katika Dowans hadi watu waipigie chapuo kiasi hiki?” alihoji.
  Alisema inashangaza kuona Dowans ikipigiwa debe na baadhi ya wabunge kama akina Makamba.
  Alisema Watanzania lazima watambue kuwa kuna jambo limejificha nyuma ya pazia kuhusu sakata la Dowans na ndiyo maana kuna danadana zinapita kila mara na kwamba hata hivyo, Watanzania wa sasa ni waelewa sana hivyo hawatakubali kuendelea kudanganywa.
  Akielezea maandamano yanayofanywa na Chadema mikoani, alisema chama hicho hakitumii mikutano na maandamano hayo kuwakashifu wala kuwatukana viongozi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu wasiokitakia mema.
  Alisema Watanzania lazima watambue kuwa maandamano na mikutano inayofanywa na Chadema mikoani inatumika kuwaeleza wananchi masuala ya maendeleo sambamba na kuwafahamisha hali ya maisha ilivyokuwa ngumu sasa na hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na serikali ya CCM.
  “Hakuna Mtanzania asiyefahamu sasa kwamba hali ya maisha imekuwa ngumu sana, mafuta na sukari vinauzwa bei juu, lakini baya zaidi ni kwamba umeme nao bei imepandishwa japokuwa umeme wenyewe ni wa mgawo.” alisema Mbilinyi.
  Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo vyombo vya ulinzi na usalama visikubali kusikia upotoshwaji unaofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu wasioitakia mema Chadema kwa kueleza kuwa kinafanya matusi na kukashifu viongozi kwani wanaosema hayo wanaogopa pengine kwa sababu wamepata uongozi kwa njia haramu.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sawaaaa
   
Loading...