Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani

MKURABITA

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
317
126
MBUNGE wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi, ameanza kukumbana na machungu ya uongozi baada ya kukabidhiwa ofisi ambayo haina samani ndani yake.
Ofisi hiyo imebainika kukosa samani zinazotakiwa baada ya mbunge huyo kwenda kwa Mkurugenzi wa Jiji, Juma Rashid Idd, kwa lengo la kukabidhiwa rasmi ili aanze kazi za kuwatumikia wananchi wa Jiji la Mbeya.

Makabidhiano hayo yalifanyika juzi, majira ya saa 3.30 kati ya Mkurugenzi wa Jiji Idd na mbunge huyo, lakini lilikwama kutokana na mazingira ya uchafu yaliyo mithili ya ofisi iliyotelekezwa na haikuwa na samani ndani yake.

Baadhi ya maofisa wa jiji la Mbeya ambao walishuhudia tukio la kukabidhiana ofisi, waliiambia Tanzania Daima Jumatano kuwa kutokana na kukosekana kwa samani katika ofisi hiyo, Mbunge huyo hakuweza kukabidhiwa hadi hapo zitakaponunuliwa nyingine.

“Ni kweli Mbunge kashindwa kukabidhiwa ofisi hiyo maana hali ya ofisi ni mbaya, ukiangalia kwa haraka utagundua kabisa kuwa jamaa…(akimaanisha mbunge aliyepita Benson Mpesya CCM) hakuwa akiitumia kwa muda mrefu,” alisema mmoja wa maafisa jiji ambaye aliomba jina lake lisitajwe.

Mbali ya kutokuwa na samani, ofisi hiyo pia haikuwa na mafaili yoyote yanayotumika kuhifadhia nyaraka mbalimbali za kiofisi ikiwemo mipango iliyotekelezwa na inayotarajia kutekelezwa na mbunge.

Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, kila mwezi mbunge hupokea sh 500,000 kwa ajili ya shughuli za jimbo, ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ofisi.

Source: Tanzania Daima 01/12/2010

Hivi huu ndo mpango wa CCM au ni utashi mdogo wa viongozi wa siasa?
 
Ni vizuri akaanza kazi bila ya hizo samani. Kumbuka, you start from the bottom to the top.
 
Mlio karibu na MH Sugu mwambie atuletee kizibiti cha picha hapa Jamvini. Fanyeni hivyo pia kwa Wabunge wote watako patwa na Masahibu hayo.
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
 
Samani ni furniture. Kwa hiyo kiswahili kiko sawa. .
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Wewe ndiye uliyechemsha. Maneno SAMANI na THAMANI yote ni ya kiswahili na yana maana tofauti. La kwanza maana yake ni FURNITURE na la pili ni VALUE. Kwa kutojua neno samani naweza nikakadiria elimu yako na kazi unayofanya. Inawezekana elimu yako ni darasa la saba na kazi yako ni mkulima au mfanyabiashara wa maparachichi au maembe. Naomba kuwasilisha kwa heshima na taadhima.
 
duh! kaka ka nakuona vile! una uhakika mpaka umeandika huku umeisimamia keyboard.....karudie tena fail
 
...Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, kila mwezi mbunge hupokea sh 500,000 kwa ajili ya shughuli za jimbo, ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ofisi.

....

...blah blah nyiiiingi hazitusaidii, tungekuwa tunaanzia hapa kwenye 'accountability' kuwapeleka hao wabunge waliomaliza muda wao polisi kisha mahakamani. Kila senti 'inayofujwa' inatokana na kodi yangu mimi na wewe mwananchi. Tuna kila sababu ya kuhoji matumizi yake. Laki tano kwa mwezi nyingi, ni sawa na 6,000,000/= kwa mwaka, au...30m/= kwa miaka mitano!
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

We wajifanya wajua kumbe waungua na jua!

Samani ni Furniture kwa Lugha ya Elizabeth

Thamani ni Value kwa lugha ya Elizabeth.

Usikimbilie kufindisha kabla hujahitim.
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
Kama wewe siyo mhindi utakuwa Mpare.
 
Wewe ndiye uliyechemsha. Maneno SAMANI na THAMANI yote ni ya kiswahili na yana maana tofauti. La kwanza maana yake ni FURNITURE na la pili ni VALUE. Kwa kutojua neno samani naweza nikakadiria elimu yako na kazi unayofanya. Inawezekana elimu yako ni darasa la saba na kazi yako ni mkulima au mfanyabiashara wa maparachichi au maembe. Naomba kuwasilisha kwa heshima na taadhima.
Kama si muuza miwa labda anauza madafu.
 
...blah blah nyiiiingi hazitusaidii, tungekuwa tunaanzia hapa kwenye 'accountability' kuwapeleka hao wabunge waliomaliza muda wao polisi kisha mahakamani. Kila senti 'inayofujwa' inatokana na kodi yangu mimi na wewe mwananchi. Tuna kila sababu ya kuhoji matumizi yake. Laki tano kwa mwezi nyingi, ni sawa na 6,000,000/= kwa mwaka, au...30m/= kwa miaka mitano!
accountability kwa wanasiasa ni alien...

BTW, nani alikwambia wabunge wa ccm wanajua hata maana ya ofisi ya bunge?? kwao ofisi yao ni pale bungeni dodoma kwisha vikao vikiisha wanarudi kuendelea na hamsini zao
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha
Mkuu, unatumia kamusi gani isiyo na neno samani? Naanza kuamini kwamba wewe kiswahili kinakupiga chenga, sasa sijui utamfundisha nani kiswahili usichookijua. Samani ni furnichers kwa kimombo, au vyombo vya kufanyia kazi nyumbani au chumbani. Kumbe nyani kweli haoni nanihii lake. Yaonekana wewe una Diploma wakati mwenzio anayo Degree, kwa hiyo kwa mtizamo wako wewe unamzidi kujua mambo mwenye degree. Tusiwe na haraka kuzuzua watu kabla hatujajiangalia wenyewe kwenye kioo.
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Samani ni furniture kama alivyosema Maamuma - jamani tusome kwanza kabla ya kutoa comment hasa kama hauna uhakika na kitu mfano neno au ndio unalisikia kwa mara ya kwanza.

Chadema MPs show former CCM MPs and CCM that you are serious with your work. Please start using those offices even if they do not have pieces of furniture - just two chairs and one table then listen to your people ready for next Bunge session. When you quit the office after 5 years, leave every thing in that office for the next MP regardless of their political party.

In the Bunge standing orders I think the aspect of office and furniture should be featured and must read that whatever is provided by Bunge say furniture is Bunge property and not MPs'. Is this connected to JK's speech when inaugurating 10th Bunge?
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

umechemsha ndugu yangu, na usipende kukosoa kitu usicho kijua. usije ukaumbuka mbele ya kadamnasi
 
Naanza kufundisha watu kiswahili sasa katika wana JF mada "Sugu akabidhiwa ofisi isiyo na samani" katika kiswahili hakuna neno samani kuna neno linaitwa Thamani weka kiswahili sawa.
Nawakilisha

Nenda shule kwanza ufundishwe ukielewa uje ufundishe
 
...blah blah nyiiiingi hazitusaidii, tungekuwa tunaanzia hapa kwenye 'accountability' kuwapeleka hao wabunge waliomaliza muda wao polisi kisha mahakamani. Kila senti 'inayofujwa' inatokana na kodi yangu mimi na wewe mwananchi. Tuna kila sababu ya kuhoji matumizi yake. Laki tano kwa mwezi nyingi, ni sawa na 6,000,000/= kwa mwaka, au...30m/= kwa miaka mitano!
Hapa kweli wanastahili kushtakiwa. Kinachonichanganya pia ni kuwa kwa hawa wapya wasiokuwa na fenicha, wanasubiri wakurugenzi waweke fenicha ndo wakabidhiwe ofisi, issue hapa ni kuwa, kama wanapokea hela kwa kazi hiyo Je? Watazirudisha kwa Halmashauri husika pesa zilizotumika kununua hizo fenicha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom