Sugu ajitolea kuwa mbunge wa Kyela; Amzunguka Mwakyembe

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Katika mkutano CHADEMA wilayani humo. JOSEPH MBILINYI ambaye ni mbunge wa Mbeya mjini amejitolea kuwa mbunge wa jimbo la kyela hadi watakapolichukua rasmi 2015. Sugu alihoji kinachomchelewesha kujiuzulu ikiwa watu waliomchagua ndiyo wanaomkataa leo? Aliwapa pia namba ya simu na kudai wampe kero zao na atazifikisha bungeni. Pia ametoa siku 7 za kukarabati stand, vinginevyo ataongoza maandamano. Amedai pia alitegemea amkute Mwakyembe jimboni lakini amemkimbia... Hiyo ndiyo Kyela na mbunge mpya, SUGU
 
Dah Ugu kampiga mwenzake bao la tobo kwa style ya counter-attack...patamu hapa...ngoja nitarudi tena!!
 
imekaa utamu hebu tuone je shoka laweza angusha mbuyu?
gud start sugu mtaji huo mh.
 
Mwakyembe haeleweki kabisa siku hizi,hajatulia...Sijui wamemroga?Teh teh teh,bongo kuna mambo...Kama kweli kamkimbia sugu,basi kuna tatizo sugu hapo.
 
Spidi ile ile waliyoitumia kumkubali, ndiyo wanayoitumia kumkataa. Hakika hakuna marefu yasiyo na ncha, huwez ukawadanganya watu wote muda wote
 
Mwakyembe yupo safi kiutendaji mpaka maadili, tatizo ni watu waliomzunguka, wengi wakiwa makada wa chama chake! Bt yote tisa, SUGU chapa kazi!
 
juzi mbowe alisema wabunge wa chadema ni wa kitaifa si wa majimbo..naona sugu kasha anza kutekeleza..
 
Utendaji upi huo usioonekana kwa wapiga kura wake? Je yeye kachukua hatua gani? Mwanzo alimsingizia Mwakipesile kwamba ndiye kikwazo ambao ni uongo mkubwa, sasa kyela wameshashituka, labda akawadanganye wazungu.
Mwakyembe yupo safi kiutendaji mpaka maadili, tatizo ni watu waliomzunguka, wengi wakiwa makada wa chama chake! Bt yote tisa, SUGU chapa kazi!
 
Mwakyembe yupo safi kiutendaji mpaka maadili, tatizo ni watu waliomzunguka, wengi wakiwa makada wa chama chake! Bt yote tisa, SUGU chapa kazi!

Tatizo si usafi bali ni utendaji! Mwakyembe amekuwa mtu wa sound sana, anatumia muda mwingi kuzunguka na waandishi wa habari! 2005 - 2010 alidai kuwa Mwakipesile alikuwa anamkwamisha katika kuleta maendeleo Wilayani Kyela! Sasa hivi hana tena huo udhuru kwa kuwa yeye ni Naibu Waziri na yuko juu ya Mkuu wa Mkoa. Huko kudai kwamba tatizo ni wale wanaomzunguka ni ujinga usiokuwa na kifani!
 
Huwa nampenda Mwakyembe tatizo kundi lake ndo linalomwangusha!
keshaingia kundini sasa anazitafuna vilivyo... zile contracts na per diem!!!

Nani alisema ni lazima uwe mpiganaji for life?
 
Mheshimiwa katika bunge la Tanzania anajiita SUGU....hahahah.
yes, na nisugu kweli, kama vile tingatinga, mapacha watatu, vasco da gama, tyson, kicheche, vijisenti, nk

unachekesha sana... hahahaaaaaaaaaa
 
Mwakyembe haeleweki kabisa siku hizi,hajatulia...Sijui wamemroga?Teh teh teh,bongo kuna mambo...Kama kweli kamkimbia sugu,basi kuna tatizo sugu hapo.

Mwakyembe kile cheo kimemchanganya kabisa kiasi hata upiganaji wake kauweka kando! au wakati anapewa hicho cheo alipewa sharti la kukaa kimya
:A S-baby:
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom