Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 226
Kinachoendelea Sudani wengi wanaweza wakafikiria kwamba Jeshi linastahili lawama, ni kweli yaliyotokea yanahuzunisha, hayawezi kufumbiwa macho wala kutetewa lakini swali ni je, nani wa kulaumiwa kati ya Jeshi na Waandamanaji wanaotaka kupewa madaraka ya kusimamia nchi?
Itakumbukwa hata Libya ilikuwa ni hivyohivyo, waandamanaji walidai kutaka kuuondoa utawala wa kidikteta wa Muammar Gaddafi lakini nyuma ya pazia kumbe wananchi hao waandamanaji hawakuwa wamejiandaa wala kujipanga kuitawala nchi na isitoshe kumbe, katika msafara wa mamba kenge nao walikuwemo. Kulikuwa na watu wasioitakia mema kabisa Libya, watu wenye misimamo mikali wanaoendelea kuihangaisha Libya mpaka kesho.
Ikiwa Wanajeshi wa Sudani Walikubali kumuondoa bosi wao, Ommar Al Bashir, waandamanaji walitakiwa kuwa wavumilivu na kukubali kufanya kazi na jeshi mpaka pale hali itakapokuwa shwari na raia kukabidhiwa madaraka kwa amani. Ikiwa Jeshi lilikuwa na nia mbaya jinsi raia wanavyofikiri sidhani kama wangekubali bosi wao wa muda mrefu kupinduliwa.
Na Umoja wa Africa sidhani kama wanasoma alama za nyakati hata kidogo kwa kukimbilia kuiwekea vikwazo Sudani badala ya kushughulikia mzizi wa fitina. Libya walinyamaza hivyohivyo hadi Gadafi akauwawa kama paka kisha hadi leo hamna msaada wowote wa maana wananchi wa Libya wanaoupata zaidi ya kukumbuka maziwa na asali enzi za Gadafi. Waafrika tufike mahali matatizo yetu tuyatatue wenyewe kwa subira kama Rais wa Ethiopia anavyoonyesha mfano huko Sudani sasa, tusisubiri tena mpaka Marekani na Uingereza waje kufanya kama walivyofanya Libya.
Peter Augustino ni mwandishi katika Blog ya "JIFUNZEUJASIRIAMALI"