Sudani Kusini: Jini lililokosa wa kulirudisha kwenye chupa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
351
866
SUDANI KUSINI JINI LILILOTOLEWA KWENYE CHUPA NA LILILOKOSA WAKULIRUDISHA.

NA: Comred Mbwana Allyamtu.

Nimeanza kujiuliza maswali mawili matatu hivi wakati juzi nilipo tazama televisheni na kuona machafuko yakiludia tena huko Sudani kusini tena mara hii wakizichapa ikulu ya Juba yani kwenye makazi ya Rais Sarva Kirr. Ndipo nilipo jiuliza maswali ivi ni nini hasa huko Sudani kusini?

Na je nani wakuliludisha jini hili la sudani kusini kwenye chupa? Na
Je ni damu ya John Garang inayowaandama wasudani kusini?.

Wakati najiuliza maswali haya nikaona kunahaja ya kumfahamu zaidi John Garang ili tuone je ni kweri ni damu yake ndio inayo waandama?

JOHN GARANG DE MABIOR NI NANI?

Dkt John Garang de Mabior Alizaliwa 23 Juni 1945 na kufariki -
30 Julai 2005 alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na kiongozi wa zamani wa waasi wa Sudan People's Liberation Army.

Chimboko lake John Garang.
Kutoka kabila la Dinka Garang alizaliwa katika familia maskini katika kijiji cha Wanglei huko Bor, Sudan, katika ukanda wa upper Nile ya Sudan (kwa sasa Jonglei State). Kwa kuachwa yatima akiwa na umri wa miaka kumi, alilipiwa karo ya shule na mmoja wa jamaa zake, na kwenda shule Wau na kisha Rumbek.

Mwaka wa 1962 alijiunga na vita vya kwanza vya wenyewe kwa wenyewe Sudan lakini kwa sababu alikuwa mchanga sana, viongozi walimshauri yeye na wenzake kutafutilia elimu. Kwa sababu ya mapigano yaliyokuwa yakiendelea, Garang alilazimishwa kuhudhuria elimu yake ya Sekondari nchini Tanzania.

Baada ya kushinda udhamini, aliendelea na kuweza kupata shahada ya ya kwanza ya BA katika uchumi mwaka wa 1969 kutoka Grinnell College, Iowa, USA. Huko alijulikana sana kwa kupenda kusoma vitabu kwake ilikuwa ni utamaduni kujisomea vitabu.

Alipewa udhamini mwingine kufanyaa masomo na kuhitimu katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, lakini aliamua kuchagua kurudi Tanzania na kusomea Uchumi wa kilimo katika chuo kikuu cha UDSM katika Afrika Mashariki kama Thomas J. Watson alivyo eleza kwenye kitabu chake cha "Fellow" katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Akiwa UDSM, alikuwa mwanachama wa University Students' African Revolutionary Front.

Hata hivyo, punde Garang aliamua kurejea Sudan na kujiunga na waasi Kuna ripoti nyingi za makosa zinazodai kwamba Garang alikutana na kufanya urafiki na Yoweri Museveni, rais wa sasa wa Uganda, wakati huo; ingawaje Garang na Museveni walikuwa wanafunzi wa UDSM katika miaka ya 1960, hawakuhudhuria wakati mmoja.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimalizika baada ya Mkataba wa Addis Ababa wa 1972 na Garang, kama waasi wengine, aliwekwa katika jeshi la Sudan.

Kwa miaka kumi na moja, alifanya kazi kama askari na kupanda kutoka safu ya Kapteni hadi Kanali baada ya kufanya Infantry Officers Advanced Course katika Fort Benning, Georgia. Katika kipindi hiki alichukua ruhusa ya kimasomo ya miaka minne na akapata Shahada ya Masters katika Uchumi wa Kilimo na Ph.D. katika uchumi kutoka Iowa State University, huko matekani na baada ya kuandika kitabu juu ya maendeleo ya kilimo ya Sudan Kusini.

Kufikia 1983, Knl Garang alikuwa akitumika kama mwalimu mwandamizi katika Shule ya jeshi iliyokuwa Wadi Sayedna kilomita 21 kutoka kitovu cha (Omdurman) ambapo aliwaelekeza makadeti kwa zaidi ya miaka 4 na baadaye yeye akateuliwa kutumika katika idara ya kijeshi katika idara ya utafiti wa kijeshi katika Makao Makuu ya Jeshi mjini Khartoum.

Aamua kusaliti jeshi na kuwa Kiongozi wa waasi Mwaka wa 1983, Garang alikwenda Bor, kwa minajili ya kupatanisha askari wa serikali ya kusini wapatao 500 katika Battalion 105 ambao walikuwa wakipinga kuwekwa doria katika vituo vya kaskazini.

Hata hivyo, Garang tayari alikuwa mmoja wa baadhi ya maafisa waliokuwa na njama katika amri ya Kusini kwa ajili ya kupanga kuhama Battalion 105 na kuunga mkono waasi waliopinga serikali. Wakati serikali iliposhambulia Bor mwezi wa Mei, Battalion ilijitoa nje, Garang akaenda kwa njia nyingine na kujiunga nao katika ngome ya waasi nchini Ethiopia.

Kufikia mwisho wa Julai, Garang alileta askari waasi zaidi ya 3000 chini ya utawala wake kupitia vuguvugu mpya la Sudan People's Liberation Army / Movement (SPLA / M), ambalo lilikuwa linapinga utawala wa kijeshi na kutwaliwa kwa sehemu kubwa ya nchi na Uislamu, na kuzihimiza ngome nyingine za jeshi kuasi dhidi ya sheria ya Kiislamu juu ya nchi na serikali.

Hatua hii ilikuwa ndio mwanzo unaokubaliana wa Vita Kuu vya Pili vya weneyewe kwa wenyewe vya Sudan, ambavyo vilisababisha vifo milioni mmoja na nusu katika kipindi cha miaka ishirini ya migogoro. Ingawa Garang alikuwa Mkristo na eneo kubwa la kusini mwa Sudan sio la Waislamu (wengii ni animist), mwanzoni hakuzingatia masuala ya kidini katika vita.

SPLA ilipata msaada wa Libya, Uganda na Ethiopia. Garang na jeshi lake walidhibiti sehemu kubwa ya mikoa ya kusini mwa nchi, iliyoitwa Sudan Mpya . Yeye alidai kuwa 'ujasiri wa askari wake kutoka kwa "uthibitisho kwamba sisi tunapambana vita vya haki. Hilo ni jambo ambalo Sudan Kaskazini na watu wake hawana. " Wakosoaji walipendekeza motisha za fedha kwa uasi wake, wakibainisha kuwa kiasi kikubwa cha mafuta ya Sudan kiko katika kusini mwa nchi. Garang alikataa kushiriki katika serikali ya mpito mwaka wa 1985 au uchaguzi wa 1986, na kubaki akiwa kiongozi wa waasi.

Hata hivyo, SPLA na serikali zilitia saini mkataba wa amani tarehe 9 Januari 2005 mjini Nairobi, Kenya. Tarehe 9 Julai 2005, aliapishwa kama makamu wa rais, cheo cha pili kwa ukuu katika nchi, kufuatia sherehe ambapo yeye na Rais Omar al-Bashir walitia saini katiba ya kugawana madaraka. Yeye pia alikuwa kiongozi wa utawala wa kusini mwa Sudan yenye uhuru mdogo kwa miaka sita kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya uwezekano wa Kuganywa.

Hakuna Mkristo au mtu kutoka kusini aliwahi kushikilia cheo cha juu kama hicho serikalini. Akizungumza baada ya sherehe, Garang alisema, "Mimi nawapongeza watu wa Sudan, hii si amani yangu au amani ya al-Bashir, ni amani ya watu wa Sudan."

Kama kiongozi, sifa za kidemokrasia za John Garang zilitiliwa mashaka mara nyingi. Kwa mfano, kulingana na Gill Lusk "John Garang hakuvumilia upinzani na mtu yeyote aliyehitilafiana naye aidha alifungwa jela au kuuawa". Chini ya uongozi wake, SPLA ilishutumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu. Itikadi za SPLA zilikuwa za uvuli kama Bw Garang mwenyewe. Aligeuka kutoka kwa mrengo wa Marxism hadi kupata msaada kutoka kwa Wakristo wenye siasa kali kutoka Marekani.

Idara ya Taifa ya Marekani ilisema kuwa kuwepo kwa Garang katika serikali kungesaidia kutatua Mgogoro wa Darfur magharibi mwa Sudan, lakini wengine waliona madai haya kuwa "matumaini kupita kiasi".

KIFO CHAKE CHENYE UTATA

Mwishoni mwa Julai 2005, Garang alikufa baada ya ndege ya rais wa Uganda aina ya helikopta Mi-172 aliyokuwa akisafiria kuanguka. Alikuwa anarudi kutoka mkutano Uliokuwa unajulikana kama "Rwakitura" na mshirika wake wa muda mrefu Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Hakuiambia serikali ya Sudan kwamba alikuwa anaenda mkutano huu na hivyo basi hakuchukua ndege ya rais. Shirika la televisheni la kitaifa kwanza lilisema kuwa ndege iliyombeba Garang ilikuwa imetua salama, lakini Abdel Basset Sabdarat, Waziri wa Habari wa nchi, alikwenda kwenye televisheni masaa kadhaa baadaye kukataa ripoti hiyo. Kwa kweli, ilikuwa ni Yasir Arman, msemaji wa SPLA / M ndiye aliiambia serikali kuwa ndege iliyombeba Garang iliwasili salama ili kuokoa muda kwa ajili ya mipangilio ya ndani katika SPLA kabla ya kifo chake kujulikana.

Ndege ya Garang ilianguka siku ya Ijumaa na hivyo ilibakia kuwa iliyotoweka hadi Jumamosi iliyofuata na wakati huu wote serikali ilidhani bado alikuwa Sudan Kusini. Mapema baadaye, taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Sudan Omar el-Bashir alithibitisha kuwa helikopta ya rais wa Uganda ilianguka katika "mojawapo ya mlima iliyoko kusini mwa Sudan kwa sababu ya kutoona vizuri na kusababisha kifo cha Dkt John Garang De Mabior, wenzake sita na wafanyikazi saba wa ndege hiyo ya Uganda."

Mwili wake ulibebwa kwa ndege hadi New Site, makazi yaliyoko kusini mwa Sudan karibu na eneo la ajali, ambamo wapiganaji waasi wa zamani na wafuasi raia walikusanyika kutoa heshima zao kwa Garang. Mazishi ya Garang yalifanyika tarehe 3 Agosti mjini Juba.

Mjane wake, Nyandeng Rebecca De Mabior, aliahidi kuendelea na kazi yake akisema "Katika utamaduni wetu sisi husema, ukimuua simba dume, utaona atakachofanya simba wa kike." pamoja na kifo chake chenye utata kulizua Maswali kuhusu kifo Serikali ya Sudan na kiongozi wa SPLA walilaumu hali ya hewa kwa ajali hiyo. Hata hivyo, kuna tashwishi katika ukweli wa jambo hili, hasa miongoni mwa safu-na-faili za SPLA.

Yoweri Museveni, rais wa Uganda, anadai kwamba uwezekano wa "sababu za nje" kuhusika usingeweza kuondolewa. Athari ya kifo chake juu ya kifo chake kwa amani ya Sudani kusini Garang Akionekana kuchangia pakubwa katika kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, madhara ya kifo cha Garang kwa mpango wa amani yalikuwa wazi.

Serikali ilitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, ambayo hayakuzuia vurugu kubwa mjini Khartoum na vifo vya angalau vijana 24 hivi kutoka Sudan Kusini waliowashambuliwa watu kutoka Sudan kaskazini na kupigana na vikosi vya usalama.

Baada ya siku tatu za ghasia, vifo viliongezeka hadi kufikia 84 Migogoro pia iliripotiwa katika maeneo mengine ya nchi. Viongozi wakuu wa SPLM, pamoja na Halifa wa Garang Salva Kiir Mayardit, walisema kwamba mchakato wa kutafuta amani ungeendelea.

Wachambuzi walipendekeza kwamba kifo kingeleta aidha demokrasia mpya ya uwazi katika SPLA, ambayo baadhi ya watu walikosoa kwa kuongozwa sana na Garang, au kuzuka kwa vita vya wazi kati ya makundi mbalimbali ya kusini yaliyokuwa yameletwa pamoja na Garang.
Kwa mtazamo huu tunaweza kuona je ni kweri damu ya Garang inawaandama wa Sudan kusini? Kama ndio sasa nini kifanyike?
Na kama hapana je Sudan kusini ni kweri ni jini lilokosa wakuliludisha kwenye chupa?

Ebu tuangalie sasa vuguvugu la machafuko ya juzi.. Kabla hatuja anza kujua kwanini mgogoro wa juzi umejiludia tena kwa mara nyingine kwa sura ileile ebu tutazame mgogoro wa mwanzo ulivyo anza kati ya Salva Kirr na Riack Machar.

MGOGORO WA KISIASA KATI YA RIAK MACHAR NA SALVA KIRR

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametangaza habari ya kugunduliwa njama ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli nchini humo. Kiir ametangaza kuwa vikosi vya usalama vya Sudan Kusini vimefanikiwa kugundua na kuzima njama za jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali yake.

Katika hali ambayo hakuna taarifa za uhakika na kamili zilizopatikana hadi sasa kuhusu njama za jaribio hilo la mapinduzi, weledi wa mambo wanaamini kuwa kitendo hicho kimetekelezwa katika muendeleo wa mashindano ya kuwania madaraka huko Sudan Kusini.

Rais Salva Kiir Mayardit amesisitiza kuwa Rick Machar Makamu wake wa zamani ni miongoni mwa watu waliotiwa mbaroni kwa tuhuma za kupanga jaribio hilo la mapinduzi ya kijeshi. Rick Machar ambaye alifukuzwa kazi tarehe 25 mwezi Julai mwaka jana kwa amri ya Rais wa Sudan Kusini, alikuwa tayari ametangaza nia yake ya kuwa mgombea katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo mwakani, kabla ya hata ya kuuvuliwa. Weledi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa Rick Machar ameuvuliwa uongozi ili kufuta upinzani wa shakhsiya huyo kwa Salva Kiir Mayardit katika uchaguzi ujao.

Baadhi ya duru za habari zilionyesha kutiwa shaka na hatua ya kufutwa kazi Makamu wa Rais Rick Machar na mawaziri wengine wawili wa serikali ya Sudan Kusini na kuhoji kama ilikuwa ni ya kulifanyia marekebisho baraza la mawaziri au kuanza mgogoro wa kisiasa nchini humo. Kwa mtazamo huo, vita vya kuwania madaraka kati ya mwanasiasa Rick Machar na Rais Salva Kiir Mayardit, vinaonekana kuwa na historia ya tangu huko nyuma.

Vita vya kuwania madaraka kati ya mahasimu hao wawili wa zamani huwenda vikaisababishia mgogoro wa muda mrefu Sudan Kusini nchi iliyoasisiwa hivi karibuni.

Sudan Kusini ilitangazwa kuasisiwa na kuwa nchi huru tarehe 9 mwezi Julai mwaka 2011. Weledi wa mambo wanaamini kuwa kujitenga Sudan Kusini na Sudan ni matokeo ya ushawishi wa Marekani na utawala wa Kizayuni pande ambazo zilifanya kila zilichoweza kuigawa vipande Sudan lengo likiwa ni kudhamini maslahi haramu ya Washington na utawala unaopenda kujitanua wa Tel Aviv.

Sasa je kwa marekani na Israel kuamua kulitoa jini hili kwenye chupa je limekosa wa kuliludisha?. Tuendelea kuona namna ujasusi wa Mosad (Israel) na CIA ya marekani ilivyo shiliki kutoa jini hili kwenye chupa *(Jamuhuri ya Sudan huko mwazo kabla ya kuitenga na kuwa nchi huru)*

Hasa ikizingatiwa kwamba utajiri mkubwa wa maliasili ya mafuta ya Sudan upo Sudan Kusini na nchi hiyo inahitaji taasisi za mafuta zilizoko Sudan kwa ajili tu ya kuchimba na kupitishia mafuta ghafi yake.

Utawala ghasibu wa Israel daima umekuwa ukitoa zingatio maalumu kwa bara la Afrika na maeneo yake ya kiistratejia. Nchi kama Uganda, Kenya na Ethiopia ni miongoni mwa waitifaki wa Israel katika eneo la Mashariki mwa Afrika zenye nafasi muhimu katika siasa za nje za utawala wa Kizayuni.

Katika mgawanyo wa kijiografia wa bara la Afrika, eneo linalozijumuisha Sudan, Kenya, Uganda na Tanzania pamoja na nchi nne za eneo la Pembe ya Afrika, zinajulikana kwa jina la "Afrika Mashariki Kubwa." Eneo hilo pia limekuwa na nafasi makhsusi katika siasa za nje za Marekani.

Hii ni kwa sababu Afrika Mashariki Kubwa kwa kuwa na Ghuba ya Aden, bahari Nyekundu na ya Hindi linatambuliwa kuwa mhimili mkuu wa njia za kimataifa za biashara ya mafuta. Kwa hiyo si jambo lililo mbali kwamba mkono wa Marekani na utawala wa Kizayuni ukawa uko nyuma ya pazia katika matukio ya ndani yanayojiri hivi sasa huko Sudan Kusini. Kwa mantiki hii kuna uwezekano mkubwa hata mgogoro wa juzi ni mwendelezo wa ukachero wa marekani na Israel. Lakini pamoja na kujijuza haya yote bado naendelea kujiuliza je ni nini hasa kincho wafanya wasudani kuwe mahali isiyo salama kabisa?

Ebu tuangalie historia yake na tuone je kunauhusiano wowote na kwa kile kinachoendelea huko Sudan kusini?

SUDANI KUSINI NA HISTORIA YAKE

*Historia ya kale*

Kuna nyaraka chache sana za historia ya mikoa ya kusini mpaka mwanzo wa utawala wa Misri upande wa kaskazini mapema 1820 na baadaye kuendelezwa kwa biashara ya utumwa kuingia kusini.

Kabla ya wakati huo, habari zote zinapatikana kwa misingi ya historia simulizi . Kulingana na mila hizo, watu wa Niloti (Wadinka , Nuer , Shilluk ) na wengine waliingia kusini mwa Sudan kwa mara ya kwanza wakati fulani kabla ya karne ya 10 .

Katika kipindi cha kati ya karne ya 15 na karne ya 19 , uhamiaji wa makabila, hasa kutoka eneo la Bahr al Ghazal , ulileta watu hawa katika maeneo yao ya sasa. Makabila yasiyo Niloti yaani
Waazande , ambao waliingia Sudan Kusini katika karne ya 16 , waliunda jimbo kubwa zaidi katika kanda hii.

Katika karne ya 18 , watu wa Avungara waliingia na kwa haraka wakaweka mamlaka yao juu ya Waazande. Utawala wa Avungara ulikaa kwa muda bila kupingwa mpaka kuwasili kwa Waingereza mwishoni mwa karne ya 19 .

Vizuizi vya kijiografia viliwalinda watu wa kusini kutokana na kuenea kwa Uislamu, na kuwawezesha kurejesha turathi zao za kijamii na kitamaduni na urithi wao wa kisiasa na taasisi za kidini.

Misri , chini ya utawala wa Khedive Ismail Pasha , ilijaribu kwa mara ya kwanza kuikoloni kanda hiyo katika miaka ya 1870 , na kuanzisha jimbo la Equatoria katika sehemu ya kusini. Gavana wa kwanza wa Misri alikuwa Samwel Baker , aliyeanza kuhudumu mwaka 1869 , akifuatiwa na Charles George Gordon mwaka 1874 na Emin Pasha mnamo 1878 .

Maasi ya Mahdist ya miaka ya 1880 yaliuyumbisha mkoa huu mchanga, na Equatoria ilikoma kuwepo kama milki ya Misri mwaka 1889 . Makazi muhimu katika Equatoria yalikuwa pamoja na Lado , Gondokoro, Dufile na Wadelai.

Sudan Kusini ilitawaliwa kama eneo la pekee wakati wa ukoloni wa Kiingereza hadi 1947 ilipounganishwa na kaskazini kama nchi moja bila kuwauliza wenyeji. Ndani ya Sudan huru Wakati wa uhuru wa Sudan mwaka 1956 viongozi wa kusini walidai haki ya kujitawala ndani ya taifa jipya, lakini mapatano yalishindikana na hali hiyo ilisababishwa kutokea kwa vita Iliyo julikana kama vita ya *Anyanya* kati ya 1956 na 1972 .

Baada ya kipindi cha amani, vita vilianza upya mwaka 1983 wakati
kanali John Garang alipounda SPLA dhidi ya badiliko la Sudan kutangazwa kama nchi ya Kiislamu. Vita hivyo vya pili vilikwisha mwaka 2005 kwa mkataba wa amani ulioacha kusini kama sehemu ya kujitawala ndani ya Sudan hadi ipigwe kura juu ya swali la kujitenga au kubakia sehemu ya Sudan kaskazini ambayo iliyopangwa kwa mwaka 2011.

Nchi imeathiriwa vibaya na vita vya kwanza vya Anya-nya na vya pili vya Anya-Anya na pia Vita vya Pili vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Sudan vya SPLA / M kwa karibu miaka 21 tangu historia ya mwanzo wa SPLA / M mwaka wa 1983 - na kupelekea kutelekezwa vibaya, ukosefu wa miundomsingi ya maendeleo, na uharibifu mkubwa na kuhama kutoka makazi yao.

Zaidi ya watu milioni 2.5 wameuawa, zaidi ya milioni 5 kuachwa bila makao na wengine kuwa wahamiaji wa ndani, na kuwa wakimbizi kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na sababu zingine zinazohusiana na vita.

Baada ya kifo cha John Garang, majeshi ya Southern Sudan Army na South Sudan Defense Force (SSDF) yalisitisha uhasama wao na kuungana mnamo Januari 2006 , chini ya Azimio la Juba. SSDF ilianzishwa na Makamu wa Rais wa sasa wa Sudan Kusini, Dkt. Riek Machar .

Chini ya Azimio la Juba, Jenerali Matip akawa Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan Kusini, na vikosi vyake vya SSDF kuingizwa katika Jeshi la Sudan Kusini, na kuongezea safu yake kutoka 50,000 hadi 309,000. Jumla ikawa askari 359,000. Wote sasa ni jeshi moja linalojulikana kama Jeshi la Sudan Kusini.

Jenerali Oyay Deng Ajak aliteuliwa kuwa Ofisa-mkuu-wa-Watumishi wa Jeshi la Sudan Kusini, hadi Mei 2009 wakati alipompisha Meja Jenerali James Hoth Mai Mbali na Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Sudan Katiba ya Mpito ya Sudan Kusini ya 2005 iliwekwa kuwa sheria kuu ya Sudan Kusini.

Katiba imeweka Tawi Kuu linaloongozwa na Rais ambaye ni Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali, na Kamanda Mkuu wa Sudan People's Liberation Army . John Garang, mwanzilishi wa SPLA / M alikuwa Rais wa kwanza hadi kifo chake tarehe 30 Julai 2005 .
Salva Kiir Mayardit , naibu wake, aliapishwa kama Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na Rais wa Serikali ya Sudan Kusini tarehe 11 Agosti 2005. Riek Machar aliingia mahala pake kama Makamu wa Rais.

Nguvu za kuunda sheria ziko mikononi mwa serikali na Bunge la pamoja la Sudan Kusini Katiba pia imeweka mahakama huru, chombo cha juu kabisa kikiwa Mahakama Kuu .

Mnamo Januari 2011 wakazi wa Sudan Kusini walipiga kura juu ya swali la kujitenga na Sudan wakaamua karibu kwa kauli moja (98.83%) kuwa nchi huru. Tofauti kubwa kati ya pande hizo ilikuwa kwamba katika Sudan yenyewe idadi kubwa ya watu wamekuwa
Waislamu na utamaduni wao una mchaganyiko wa tabia za Kiarabu na Kiafrika pamoja na usambazaji mkubwa wa lugha ya Kiarabu.

Kumbe kusini kuna Waislamu wachache, wengi ni wafuasi wa dini za jadi au ni Wakristo. Kiuchumi na kielimu kusini wako nyuma sana kulingana na kaskazini. Nazani sasa tunaanza kupata picha ya kwanini Riak Machar na Salva Kirr wanamivutano ya kisiasa.

Nchi ina muundo wa shirikisho Tangu upatikane uhuru, nchi imeendelea kuvurugwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Riack Machaer na Salva Kirr na kwa sasa inashika nafasi ya kwanza katika orodha ya nchi dhaifu duniani kiuchumi Hata hivyo mnamo Machi 2016 nchi imekubalika kama mwanachama wa sita wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Je nini madhara ya Sudani kusini katika jumuiya ya Afrika mashaliki?........ Tutaendele na makala hii wakati mwingine kwenye sehemu ya pili ya muendelezo tuone je kwa hilo linalo endelea Sudani kusini mataifa ya Afrika mashaliki yanaathilika?

" Mungu bariki Afrika, Mungu bariki waafrika, Mungu bariki fikra za waafrika"


57250d2fe0b8cd85a87e83af72f0f86d.jpg
db85aa5905c3816108a05a793b0c012b.jpg
 
Hiyo nchi inasikitisha mno,walichokuwa wanakitaka wamepewa lakini wameshindwa kuiendesha,wamebaki kuuana wenyewe kwa wenyewe...ni heri irudi kwa BASHIR
 
Asante kwa uchambuzi nimeisoma post yako mstari kwa mstari nimeelewa na kulewa, sisi watu weusi sijui hii shida nini chanzo. Tumwachie Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom