Sudan yasitisha mkataba wa kujenga kituo cha kijeshi cha Russia kwa sababu ya Marekani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Sudan yasitisha mkataba wa kujenga kituo cha kijeshi cha Russia kwa sababu ya Marekani

Apr 29, 2021 03:43 UTC

[https://media]

Vyombo vya habari vya Russia vimetangaza kuwa, mkataba wa kujenga kituo cha kijeshi cha nchi hiyo nchini Sudan umesimamishwa na serikali ya Khartoum.

Kwa mujibu wa vyombo hivyo, sababu ya Sudan kuchukua hatua hiyo imetajwa kuwa ni makubaliano mapya ambayo nchi hiyo imefikia na Marekani katika uga wa mashirikiano ya kiufundi na kijeshi.

Hata hivyo serikali ya Khartoum bado haijatoa tamko rasmi kuhusu kusimamishwa utekelezaji wa makubaliano hayo iliyokuwa imefikia na serikali ya Moscow ya kuasisi kituo cha jeshi la wanamaji la Russia kandokando ya mji mkuu Khartoum.

Novemba 12, 2020 waziri mkuu wa Russia Mikhail Mishustin alithibitisha kusainiwa rasimu ya makubaliano ya kujenga nchini Sudan kituo cha kikosi cha wanamaji cha nchi hiyo cha shughuli za maandalizi na masuala ya uendeshaji.

[https://media] Mikhail Mishustin

Russia na Sudan zilifanya mazungumzo kuhusu rasimu ya mkataba huo; na Khartoum ikaafiki pendekezo la Moscow la kujenga kituo cha jeshi lake la wanamaji cha masuala ya uendeshaji na kupanua miundomsingi yake kwa ajili ya ukarabati wa manowari za Russia na kuwatengea eneo la mapumziko mabaharia wa meli za kijeshi za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Russia itaruhusiwa pia kuweka manowari zake za atomiki katika kituo hicho cha shughuli za kikosi chake cha wanamaji.

Miongoni mwa vipengele vya hati ya makubaliano hayo ni Russia kupatiwa bila malipo eneo maalumu la ardhi kwa ajili ya kujenga kituo hicho cha kijeshi; na kwa upande wake, Moscow itahakikisha inaipatia Sudan silaha na zana za kijeshi ikiwemo mitambo ya ulinzi wa anga kwa ajili ya kulinda kituo chake hicho.../

Tags
 
Back
Top Bottom