Sudan yakanusha madai kuhusika katika mapigano yanayojiri nchini Libya au kutuma mamluki nchini humo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Naibu Mkuu wa Kamati ya Kisiasa ya Baraza la Mpito la Uongozi nchini Sudan amekanusha madai kuwa nchi hiyo inahusika katika mapigano yanayojiri nchini Libya au kutuma mamluki nchini humo.

Luteni Jenerali Yasir al Atta ambaye ni Naibu Mkuu wa Kamati ya Kisiasa ya Baraza la Mpito la Uongozi la Sudan lenye uhusiano mkubwa na nchi za Misri, Saudi Arabia na Imarati jana Alhamisi alikanusha madai yanayosema Sudan inashiriki katika mapigano ya ndani nchini Libya na kudai kuwa, Khartoum inataka kushirikiana kiuchumi na nchi jirani.

Al Atta ameongeza kuwa Sudan haitaingia vitani huko Libya hata kama suala hilo litahusu kuunga mkono juhudi za Kiarabu, Kiafrika au kimataifa. Kuhusu Sudan kutuma mamluki huko Libya kwa ajili ya kuwasaidia wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar, mjumbe huyo wa Baraza la Uongozi la Serikali ya Mpito ya Sudan amesema: Sudan haijawahi wala haitatuma mamluki kupigana nchini Libya. Ameongeza kuwa mamluki waliopo sasa huko Libya wametoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaeleza kuwa, wanajeshi elfu moja wa Sudan wa vikosi vya radiamali ya haraka tarehe 25 mwezi Julai mwaka jana walitumwa Libya kwa amri ya Muhammad Hamdan Dagalo Naibu Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan.
 
Haiwezi wala haitatokea sudan kutuma mamluki kupigana nchini Libya ama taifa lolote la kiislamu.

Hayo yote ni kuwachonganisha tu
 
Back
Top Bottom