Sudan yafunga mpaka wake na Ethiopia kutokana na mapigano yanayoendelea Tigray

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Sudan imeamua kufunga mpaka wake na Ethiopia baada ya mvutano kati ya serikali ya shirikisho na utawala wa mkoa wa Tigray.

Kulingana na shirika rasmi la habari la Sudan, Fethurrahman al-Emin, gavana wa jimbo la Kesele kwenye mpaka wa Eritrea na Ethiopia, amesema kwamba baada ya mapigano huko Ethiopia, wameamua kufunga mpaka na nchi hii ya mashariki hadi hapo amri itakapotolewa.

Akisisitiza kuwa hakuna mtu yeyote mwenye silaha ataruhusiwa kuingia katika ardhi za Sudan, Gavana Emin amebainisha kuwa wataunda tume juu ya suala la raia watakaokimbilia katika ardhi yao.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza mnamo Novemba 4 kwamba waliamua kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Tigray People's Liberation Front (TPLF), ambayo "ilishambulia na kufanya vita" kwa vitengo vya jeshi la kitaifa, na kuamuru jeshi kupindua utawala wa mkoa wa Tigray.

Mara tu baada ya tangazo hilo, Baraza la Mawaziri la Ethiopia lilitangaza hali ya dharura ya miezi 6 katika mkoa wa Tigray.

Katika mkoa ambao laini zote za simu na mtandao zilikatwa, kikosi maalum cha jeshi kilianzishwa kusimamia hali ya hatari.

Inahofiwa kuwa uamuzi wa Ahmed utasababisha mzozo wa muda mrefu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Tigray, ambapo wanamgambo wamekuwa wakijaribu kuleta vita kwa miaka mingi.
 
Back
Top Bottom