Sudan: Wanafunzi wanne wauawa katika maandamano dhidi ya uhaba wa mkate na mafuta. Mazungumzo ya kuwapa raia madaraka yakwama

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Wanafunzi wanne ni miongoni mwa Waandamanaji watano waliouawa kwa kupigwa risasi jana wakati vyombo vya usalama vikitawanya maandamano ya kulalamikia uhaba wa mkate na mafuta

Maafisa wametangaza amri ya kutotoka nje usiku katika miji minne kufuatia vifo hivyo katika mji wa Al-Obeid wa jimbo la Kordofan ya Kaskazini huku shule zote za eneo hilo zikishauriwa kusitisha shughuli za masomo

Wakati hayo yanatokea jana, Viongozi wa maandamano na Watawala wa Kijeshi wanatarajiwa kufanya mazungumzo mapya leo kuhusu kipindi cha uongozi wa mpito nchini humo

Mazungumzo hayo yanajumuisha masuala kama mamlaka ya baraza tawala liitakaloundwa, namna ya kutumia vikosi vya usalama na iwapo kuwe na kinga dhidi ya Majenerali wa Kijeshi kutokana na machafuko yanayohusiana na maandamano
====

UPDATE
Viongozi wa maandamano Sudan wamefutilia mbali mazungumzo yaliyopangiwa kufanyika kati yao na majenerali wa kijeshi wanaoiongoza nchi, huku mamia ya wanafunzi wakishiriki maandamano kupinga mauaji ya wanafunzi wenzao

Wanafunzi hao waliyovalia sare zao za shule na kubeba bendera ya nchi yao Sudan, walisema kwa sauti "kumuua mwanafunzi ni sawa na kuliua taifa” wakati walipoandamana Mashariki mwa mji wa Burri kupinga mauaji ya wanafunzi wenzao watano waliouwawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano dhidi ya uhaba wa mkate na mafuta nchini humo.

Maandamano mengine pia yalifanyika katika maeneo tofauti katika mji Mkuu wa KhartoumWaandamanaji walililaumu jeshi linaloogopewa kwa mauaji ya wanafunzi hao.

Sudan, Unruhen (Getty Images/H. E.-Tabei)
Baadhi ya waandamanaji Sudan mjini Khartoum

Mauaji hayo yalitokea siku moja kabla ya viongozi wa maandamano kufanya mazungumzo na jeshi juu ya sehemu iliyobakia ya kurejesha utawala wa kiraia baada ya pande hizo mbili kukubaliana kugawana madaraka mapema mwezi huu.

Lakini Taha Osman mpatanishi anaetokea vuguvugu la maandamano amesema mazungumzo hayo kamwe hayatofanyika hii leo maana kundi lao bado lipo Al Obeid na litarejea hii leo usiku.

Mpatanishi mwengine aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mazungumzo hayo yatarejea pindi patakapokuwa na utulivu, maana mazungumzo ndio njia pekee ya kupata suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaolikumbwa taifa hilo kwa sasa.

Jeshi lalaani mauaji ya wanafunzi Sudan

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la kijeshi linaloiongoza Sudan Jenerali Abdel Fattah al Burhan ameyalaani mauaji ya wanafunzi hao watano.

"Kile kilichotokea Al-Obeid kinasikitisha, kuua raia ni uhalifu usiyokubalika unaohitaji uajibikishwaji wa haraka," alisema mwenyekiti huyo alipozungumza na waandishi habari.

Sudan Militärrat Abdel Fattah al Burhan (picture-alliance/AA)
Mwenyekiti wa Baraza la kijeshi linaloiongoza Sudan Jenerali Abdel Fattah al Burhan

Huku hayo yakiarifiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia watoto UNICEF limeitolea wito serikali ya Sudan kufanya uchunguzi wa mara moja juu ya mauaji ya watoto hao na kuwawajibisha wote waliyohusika.

Madaktari wanaofungamanishwa na vuguvugu la maandamano wamesema zaidi ya watu 250 wameuawa hadi sasa katika maandamano yaliyogeuka na kuwa vurugu tangu mwezi Desemba wakati maandamano ya kwanza kabisa yalipoibuka dhidi ya rais aliyeondolewa Omar al Bashir.

Baraza la kijeshi limekuwa likishikilia madaraka nchini Sudan tangu jeshi hilo lilipomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu nchini humo Omar al Bashir mnamo Aprili 11.
 
Wameyataka wenyewe, wasingemng'oa Raisi wao yasingetokea yote haya. Tatizo hawajifunzi kwa mataifa mengine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom