Sudan to Become Africa's Largest Producer of Military Weapons Technology, Planes

you have no idea how -left behind- we are..,yani sometimes nchi pekee tulizoziacha ni zile hazifiki 20 to be honest!!

tuna kazi ngumu..,too bad viongozi wetu ndio hao tena...,nchi nyingine they are really poor but when you look at steps taken by their leaders you can see how well of they can be in 10 years!!

but i'm sad to feel just worse in terms of my country..,yani hata super-market ikizinduliwan prezident na cabinet yoote itakuwepo..,thats just how short minded we are...(our leaders)!!

can they think of a better TZ in 10 to 20 years later???the best they can think about future is 5 years guess what!!election time!!


,,,Yaani ni KWELI kabisa,lakini sasa tufanyeje jamani na ZIMWI hili CCM????Manake hili lijamaa nalo ndio limekamata NJI hii,waalaah kila kitu lenyewe tu,na hata sijui kama wenyewe hawa WAKUBWa huwa wana wivu wanapowaona wenzao wanavyoendeleza NCHI zao,juzi juzi MH.JK si alienda KHARTOUM kwa mwaliko,nadhani aliona kukoje,,Lakin wala roho haziwastuki,Ngoja nikuambie,,,Kama BABA wa MAPINDUZI ya ZANZIBAR Sheikh ABEID A. KARUME angaekuwepo,basi leo ZANZIBAR ingekuwa ULAYA,manake ma barabara yoote aliojenga enzi hizo ndio zinazotumika leo hii zenji,SMZ ya leo imebaki kupiga viraka tu,na wakati ule jamaa alimwaga mi double road karibu mji wote wa ZNZ,,cheki walipokuja jamaa hawa,,,aah,Nafikiri hawa viongozi wetu hawajali saana maendeleo ya NCHI,wao wanajijali wao na familia zao tu,na ndio maana kila baada ya uchaguzi wao wanawaza uchaguzi UJAO na sio maendeleo,,,,,,,SUDAN hiyoo,RWANDA hiyooo,KENYA waleeee,,,UGANDA nao daah hawa hapa kwa KASI kuubwa,sijui tufanye nini.
 
Hii topic imewavuta watu wengi toka nje ya Tanzania kuja kusoma kuna nini.

Kuna kitu nahisi kikipigiwa kelele itabidi kiwekwe kando muda si mrefu!

Happy New Year 2009!
 
wakati mwingine huwa najisikia kutukana au hata kuua...
 
So, tayari tumesahau what Al Bashir is doing in Darfur, kwa sababu ya hayo magorofa. What is development? One economist defined from oxford (Amartya Sen) defined development as freedom. Without freedom, no development! Hayo maghorofa yanawezekana kwa sababu ya ukatili wanaofanya Darfur. What's so special with the buildings? What do they mean to the common mwananchi from Southern Sudan or Darfur? Is that what you want in Bongo, buildings? Think twice!
 
A prestige? To become largest producer of Military weapons in Africa? Do you think Sudan gonna export their military produce to America or Europe or China? Where is the market? This is another sad news for Africa! We are just getting ready to kill ourselves.
 
Ni kweli kabisa nami nilipagawa kuona wenzetu walipiga hatua ila mm baada kupitia hz comments hapo juu nimedata kbs....hawa wa sudan watamuuzia nani?au wametengeneza ajili ya waafrika wa jirani nae ili tuuane vzr ikiwemo darfur?maana sidhani kama atauza hata asia au america kusini....marekani hawezi hata kusogea maaana zimetoka urusi....sasa angalau angeongeza nguvu kwenye vifaa kuchimba madini,mafuta na ma trekta anaweza pata soko la africa.....ila nasi tuwe na wivu wa maendeleo....tujikite kwenye rasilimali zetu dhahabu,mafuta etc tujenge na kuboresha uchumi na per capita income.....hadi lini tutakuwa wasindikizaji na walalamikaji?ina bore jamani
 
Imekuwaje tena mjadala ulioanzishwa na CIA mwaka 2007 wakati wa matayarisho ya kuigawa Sudan umerudishwa tena leo 2011.
Lakini twajua ni kwa vile lengo la awali limetimia,sasa limepatikana jukwaa la Sudan ya kusini kuipiga Sudan na kuisambaratisha kama vile ilivyo Pakistan.Ni hatua baada ya hatua kuupiga uislamu kabla kuitangazia Makka uadui.Taarifa zipo kwamba majeshi ya nchi nyingi za Afrika yako katika harakati za kivita maeneo ya waislamu hasa Somalia na Sudan.Si kwa amri zao moja kwa moja bali za vinara wa vita hii.
Mafanikio yamepatikana lakini Jee itawezekana?.
 
Nimefika sasa hivi kutoka Sudan. Nashuhudia hayo maendeleo ni kweli. Tena yangekuwa maradufu lau si kwa vipingamizi vya uchumi ambavyo Marekani na rafiki zake wameiwekea Sudan. Vipingamizi vya Marekani ni kwa sababu mbili kuu:-Al Bashir ameishirikisha China pekee katika mafuta ya Sudan-Siasa za Sharia ya Kiislamu Maendeleo makubwa ya Sudan na yale ya Iran yanaonesha wazi wazi kuwa Nguvu za Madola ya Magharibi zinakwenda kwisha. Katika miaka ya sabini, nchi haithubutu kukosana na madola ya Magharibi halafu ikaweza kuendelea au hata kujilisha. Hivi sasa kuna sehemu mbadala za kupata mahitajio yote ya nchi. Marekani yenyewe sasa ndiyo inayojidhuru kwa kuweka vikwazo vya uchumi kwani inajiondoa yenyewe kwenye lucrative deals na kuwaachia Wachina, Wamalaysia, Wahindi n.k.Huku kufilisika kwa Marekani kuangaliwe kwa tafsiri hii. Marekani haiwezi ushindani wa kibiashara na by extension Ulaya. Na ndiyo maana uchochezi wa migogoro ya vita umezidi mno katika wakati huu, hicho ndiyo wanachokiweza zaidi!
 
Nataka kumjibu Skills4ever. Kwanza ondoa hiyo Avatar ya mhuri wa rais wa Marekani- katika miaka ya 70 na 80 hata 90, hayo nimaendeleo. Hivi sasa ni ushamba.
Pili unauliza Sudan itauza wapi silaha? Ndugu yangu katika masoko yote soko la silaha ndiyo lenye fedha zaidi na ambalo litakuwepo milele. Si lazima kuuza mbali, humu humu Afrika kutakuwa na masoko. Wengine watanunua kwa ajili ya kuzatiti usalama wao, na wengine watanunua kwa kupigana.
Pili, maendeleo mengi ya tekinolojia, hasa ya vifaa, utakuta yameanza kwenye sekta ya jeshi na usalama. Kusema hivyo namaanisha, mara nyingi unapokuwa mweledi wa kutengeneza vifaa vya kijeshi ndipo hatimaye utaweza kutengeneza teknolojia ya kiraia (civilian technology). Vitu ingi uvionavyo hii leo, tv, computers,radio, simu za mkononi, nguvu za nuklia kwa kutoa umeme na madawa.....zote zilianza kama vifaa vya kijeshi. Kwa hiyo Sudan haifanyi makosa inafuata mkondo wa maendeleo ya kiteknolojia uliopitwa na wengi. Tulichelewa ni sie tu na karibuni tutashika mkia hata Afrika. By the way, umeona jinsi Equatoria Guinea inavyokuja? Na hiyo haikuwa ikilinganishwa hata na mkoa uliochelewa Tanzania kama vile Kigoma katika miaka ya 70!
 
Back
Top Bottom