Sudan: Omar Bashir alilipwa mshahara wa dola za kimarekani millioni 20 kwa mwezi (zaidi ya Shillingi bilioni 46 za kitanzania)

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,937
25,279
Rais wa Sudan Kusini Omar Al-Bashir alikuwa akipokea mshahara wa kila mwezi wa dola milioni 20 sawa na shillingi bilioni 46 za kitanzania kutoka kwa vyanzo visivyojulikana, hii imebainishwa na kamati ya kupambana na ufisadi ya nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kupambana na Rushwa na Uporaji wa Fedha nchini Sudan Mohamed Al-Fake alieleza mapema Jumanne kuwa kamati hiyo imegundua akaunti kwa jina la Al-Bashir ambayo ilikuwa na mapato ya kila mwezi ya dola milioni 20 hadi baada ya kujiondoa Sudan ya Kusini kujiondoa Sudani.

Mshahara huo unasemekana kupungua polepole hadi kufika dola za Kimarekani milioni 8 , na kushuka mpaka dola za Kimarekani milioni 3.

Ufadhili huo ulisimama tu baada ya Bashir kufukuzwa madarakani na jeshi mnamo Aprili 2019, Akhbar ya Sudan iliripoti.


Source: Sudan’s Bashir received $20m monthly salary
 
Unashangaa Magufuli analipwa milion tisa tu
Dunia haipo sawa
Hiyo inasaidia nini kama bado anaweza kutumia shilingi 1.5 Trillioni bila maelezo yoyote na bila idhini ya bunge. It's utterly nonsense.

After all, hakuna ushahidi wa wazi kuwa mshahara wake ni milioni tisa kwani marais wastaafu hulipwa 80% ya mshahara wa rais muandamizi na haiwezekani kuwa nao wamekatwa mafao yao toka Magufuli aingie madarakani kwani kabla hajawa rais Kikwete alikuwa akijilipa zaidi ya milioni 30 kwa mwezi.

Hapo kwenye mshahara wa rais kuna uongo mwingi sana lkn itakuja kujulikana tu kwani siku zote uongo haidumu.
 
Madikteta huwa wanajali sana maslahi yao, wanakula pepo wakiwa madarakani.
 
Back
Top Bottom