SUDAN KUSINI : Waasi wamshilikilia Rubani na ndege ya Tanzania

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Waasi watiifu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais, Riek Machar wanamshikilia ofisa wa Serikali Jimboni Liech, Kusini mwa nchi baada ya ndege ya kukodi kutoka Tanzania kutua kwenye ardhi ya waasi eneo la Gautier, Jumanne

Msemaji wa SPLA-IO Jimboni Unity, James Yoach jana alithibitishia radio Tamazuj kwamba wanamshikilia Kamishna wa Kaunti ya Panyijiar, Peter Gatkoi na ndege hiyo ya kukodi kwenye uwanja mdogo wa Ganyiel

"Desemba 27, ndege hiyo ya Tanzania ilikuja Juba, ikiwa imembeba Kamishna wa Panyijiar, Peter Gatkoi na kutua kwenye uwanja mdogo wa Ganyiel", alisema Yoach

"Hatujamuua mtu huyo", alisema."Tunamshikilia tu na ndege, hivyo wako kwenye mikono salama baada ya kutua kwenye eneo letu, Kamishna huyo anafuatana na walinzi watatu na Rubani,"aliongeza

Ofisa huyo wa waasi alisema watachunguza suala hilo, "Maafisa wetu watachunguza suala hilo, tunataka kujua zaidi kutoka kwao kwa sababu Panyijiar ni eneo letu, tutalichunguza, kwasababu ndege hiyo ilitoka Juba na kutua kwenye eneo letu," alisema

Yoach alisema Maafisa wa SPLA-IO wanajadiliana na kampuni inayomiliki ndege hiyo,"Nakuhakikishieni kwamba rubani yuko salama na watu wetu wanajadiliana na kampuni inayomiliki ndege hiyo ili rubani aachwe pamoja na ndege yake,"alisema
c27f5881b8abb71cdd74dff739dc1bc7.jpg
Agosti, waasi wa Sudan Kusini walikamata ndege ya kukodi kutoka Kenya na mfanyakazi wake mjini Yuai kwenye Kaunti ya Uror Jimboni Jonglei.

Chanzo : JamboLeo
 
Susan kusini watanzania wamekamatwa, Malawi nako kimenuka.

Tukimbilie wapi siye?????
 
Walienda kufanya nini huko Sudan kusini hawajui kuwa hayo ni maeneo hatari zaidi kwa binadamu...mtu anakupa dili mwende huko au kwa Boko haramu au kwa Alishababu hapo sonaria si bora ubaki Bongo tuu unakuna Nazi...
 
Back
Top Bottom