Sudan Kusini: Maafisa 27 wa Ikulu waambukizwa virusi vya corona

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,194
Dunia ikiwa katika kizungumkuzi cha kupambana na janga/mlipuko wa gonjwa la corona, maafisa 27 wa Ikulu ya Sudan Kusini wamethibitihswa kuwa wameambukizwa virusi vya corona.

Kufuatia hali hiyo mpaka sasa wamewekwa karantini, Ateny Wek Ateny, ambaye ni msemaji wa Rais Salva Kiir, ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA kwamba walioambukizwa wanatumika katika idara za ulinzi, huduma za mapishi na udereva, pamoja na yeye mwenyewe msemaji wa rais.

Taarifa zaidi zinafahamisha kwamba rais Kiir yupo salama, na kuanzia sasa serikali itadhibiti idadi ya watu wanaopaswa kukutana na kiongozi huyo wa nchi.

Hata hivyo rais huyo atafanya kazi zake akiwa nyumbani ili kueouka maambukizi ya ugonjwa huo, ikumbukwe taifa hilo la Afrika Mashariki limethibitisha kuwa mpaka sasa watu 6,417 wameambukizwa virusi vya corona na wengine 83 wamefariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Source. DW
 
ni Kati ya nchi zinazopitia changamoto Basi ni Sudan,Kwanza bado ni taifa changa then corona,sijui hali ya uchumi itakuwaje huko
 
Back
Top Bottom