Sudan Kusini kufungua shule kuanzia leo, mimba kwa wanafunzi zaongezeka

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wanafunzi Sudan Kusini.jpg

Baada ya miezi 6 ya kukaa majumbani, wanafunzi nchini Sudan Kusini wanarejea darasani kuanzia Jumatatu, Waziri wa Habari wa nchi hiyo amesema.​

Hatua hiyo ya Sudan Kusini inafuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuondoa katazo lililowekwa mwezi Machi na Rais Salva Kiir la kufunga shughuli zote za kielimu ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona.​

Waziri Michael Makuei amesema kuwa uamuzi wa kufungua shule haujafanyika kwa kukurupuka, kwamba umefanyika baada utafiti wa kina uliofanywa na Kikosi Kazi cha Taifa cha COVID-19.​

"[Kikosi Kazi] kimeona kuwa kiwango cha maambukizi kimepungua kwa kiasi kikubwa na hakujaripotiwa kisa chochote cha maambukizi mapya ndani ya wiki kadhaa zilizopita. Baada ya utafiti, imepitishwa kuwa shule na vyuo vitafunguliwa tena kwa muda ambao utapangwa na Wizara ya Mambo ya Jumla na Wizara ya Elimu na mwongozo utatolewa na ofisi za Wizara husika," alisema Waziri Makuei.​

Lakini mwezi Julai, mashirika ya Save the Children na UNESCO yalitaka mataifa duniani kuangalia uwezekano wa kuondoa katazo dhidi ya shughuli za kielimu, yakisema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa watoto wanapata madhara makubwa kutokana na kuendelea kukaa majumbani.

Mashirika hayo yalieleza kuwa watoto wanadhoofu kiafya kutokana na kukosa lishe waliyokuwa wakiipata wakiwa shule huku wengine wakifanyiwa ukatili wa kijinsia.

Mapema mwezi Mei, Wizara ya Elimu nchini humo liliripoti visa 23 vya wasichana kupata mimba katika jimbo la Equatoria Magharibi pekee, huku wengine 125 wakipata mimba katika jimbo la Equatoria Mashariki, kwa mujibu wa Wizara hiyo mwezi Julai.​

Waziri Makuei ameongeza pia kuwa baraza hilo limeondoa ukomo wa muda wa kufanya kazi kuanzia leo ofisi zitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 11 jioni.​

Serikali ya Sudan Kusini ilichukua tahadhari ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, ikiwamo kufunga shule, mipaka, na baadhi ya biashara zisizo za lazima, huku ikiweka katazo la kusafiri baina ya mikoa ya nchi hiyo na kuzuia idadi ya watu katika vyombo vya usafiri wa umma.​

Sudan Kusini imeshuhudia visa 2,578 vya maambukizi ya virusi vya corona, huku watu 49 wakipoteza maisha na wengine 1438 wakipona virusi hivyo.
 
Tunapenda Sudan Kusini. Ni nchi kwa historia yenye mambo mengi. Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia nchi hii.
 
Back
Top Bottom