Sudan kusini ina uwezo wa kupeleka mafuta yake zambia kupitia Dar kwa bomba ikitaka

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Kama sudan kusini ikiunga bomba lake na uganda kupitia Tanga,Tanzania yaweza ongea na Sudan na Uganda na kampuni ya TOTAL kama wakipenda kujengwe bomba toka Tanga hadi Dar esalaam ambapo si parefu ili bomba hilo liunganishwe na lile la mafuta linalopeleka Mafuta ZAMBIA ambalo liko tayari.

Kuunga huko kutaisaidia Sudan kusini na Uganda kuuza mafuta mengine kwa kuyapakia kwenye meli na kupeleka nje ya nchi lakini pia kuyasafirisha hadi zambia.

Nchi hizo mbili zaweza kamata soko la Afrika mashariki yote na kati ikipitisha mafuta yake toka tanga hadi dar es salaam si mbali mtu akitaka kujenga bomba la mafuta ili liunganishwe na lile linaloenda zambia ambalo tayari lipo.

yehodaya123@gmail.com
 
Kama sudan kusini ikiunga bomba lake na uganda kupitia Tanga.Tanzania yaweza ongea na Sudan na kampuni ya TOTAL kama wakipenda kujengwe bomba toka Tanga hadi Dar esalaam ambapo si parefu ili bomba hilo liunmganishwe na lile la mafuta linalopeleka Mafuta ZAMBIA ambalo liko tayari.

Kuunga huko kutaisaidia Sudan kuuza mafuta mengine kwa kuyapakia kwenye meli na kupeleka nje ya nchi lakini pia kuyasafirisha hadi zambia.

Sudan KUSINI YAWEZA kamata soko la Afrika mashariki yote na kati ikipitisha mafuta yake kuja Tanzania

yehodaya123@gmail.com
Kama wakiacha vita na kuwa wazalendo haswa kwa viongozi kunufaika na mikataba ya mafuta badala ya umma
 
Kapalamsenga hilo la vita ni lao na halihusiana na interest yetu ya kiuchumi. Tuwavae chap chap kabla Mkenya hajaweka sumu. Yehodaya this is a brilliant idea wapenyezee wahusika hasa foreign affairs! Tuna competitive advantage ya amani na kuaminika (reliable partner). Lets exploit them to make money badala ya kusifiwa tu.
 
Kumbuka Amerika na China wanainterest kubwa sana katika mafuta ya S.Sudan
 
Yes, kwetu siye hatuhitaji mafuta yao ila transportation charge na kazi kwa bandari zetu kama kwa bomba la mganda! Niliposema tuna competitive advantage ni hizo zitakazowafanya US na China watuunge mkono. Interest zao ni mafuta. Mafuta ya S.Sudan yanapita Sudan ambako ni taabu kwa US. China na ukaribu wake na Sudan bado anahitaji reliable parner na amani. Tanzania wins on those grounds.
 
Sudan Kusini pamoja na Uganda wanaweza kuwa wauzaji wakuu wa mafuta kwa upande wa Afrika Mashariki na Kati, Nchi za pembe ya Afrika.
 
Sina utalaam wa mafuta, mafuta ghafi na haya tunayotumia tofauti yake ni nini? Na hayo ya Uganda kupita tanga ni ghafi ama? Na yatokayo dar kwenda Zambia nayo ni yepi?

Yanayosafirishwa kwa bomba ni mafuta ghafi sio haya tunayotumia.Yanakuwa hayajawa refined kwa matumizi.Nategemea pia serikali ya viwanda ya Magufuli yaweza jenga pia kiwanda cha refinery Tanga na kukifufua kiwanda chetu cha refinery cha Tipper kilichoko Dares salaam ili hayo mafuta ghafi yawe refined hapa hapa nchini kwa ajili ya soko la ndani na nchi za afrika mashariki na kati.Hii itaokoa pesa nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta yaliyosafishwa toka nje ya nchi na yaweza isaidia thamani ya shilingi yetu kuwa imara sana.
 
Kama sudan kusini ikiunga bomba lake na uganda kupitia Tanga,Tanzania yaweza ongea na Sudan na Uganda na kampuni ya TOTAL kama wakipenda kujengwe bomba toka Tanga hadi Dar esalaam ambapo si parefu ili bomba hilo liunganishwe na lile la mafuta linalopeleka Mafuta ZAMBIA ambalo liko tayari.

Kuunga huko kutaisaidia Sudan kusini na Uganda kuuza mafuta mengine kwa kuyapakia kwenye meli na kupeleka nje ya nchi lakini pia kuyasafirisha hadi zambia.

Nchi hizo mbili zaweza kamata soko la Afrika mashariki yote na kati ikipitisha mafuta yake kuja Tanzania

CHEKI ramani ya Tanzania toka tanga hadi dar es salaam si mbali mtu akitaka kujenga bomba la mafuta ili liunganishwe na lile linaloenda zambia ambalo tayari lipo.

political-map-of-Tanzania.gif

yehodaya123@gmail.com
 
Mafuta ya Uganda ambayo wanataka kupitisha kwa bomba kwenda Tanga ni ghafi yanatakiwa kwenda kusafishwa ili wapate aina tofauti za
Mafuta ambayo tunazifahamu kama desel,petro, mafuta ya taa na kadhalika kwa maana nyingine bado yajawa tayari ya matumizi na bomba la mafuta la tazama hili lina pitisha mafuta ambayo tayari yamesha safishwa yapo tayari kwa matumizi sasa ndoto ya kuunganisha haiwezekani kwa kuwa ni aina tofauti
 
bomba la mafuta la tazama hili lina pitisha mafuta ambayo tayari yamesha safishwa yapo tayari kwa matumizi sasa ndoto ya kuunganisha haiwezekani kwa kuwa ni aina tofauti

Mkuu bomba la mafuta la TAZAMA linasafirisha mafuta ghafi(crude oil) ambayo hayajasafishwa.Yanaenda safishiwa Zambia.na ya Uganda na sudan pia yatakuwa CRUDE OIL.Hivyo yote yakitoka SUDAN kusini na Uganda yaweza safirishwa bomba la TAZAMA bila shida
 
Kapalamsenga hilo la vita ni lao na halihusiana na interest yetu ya kiuchumi. Tuwavae chap chap kabla Mkenya hajaweka sumu. Yehodaya this is a brilliant idea wapenyezee wahusika hasa foreign affairs! Tuna competitive advantage ya amani na kuaminika (reliable partner). Lets exploit them to make money badala ya kusifiwa tu.
Uganda anapitisha mafuta yake, unataka aache mwengine apitishe au wafanye zamu, kwani yeye akikuuliza hawezi peleka huko Zambia. Kujaribu sio mbaya wadau waweza fuatilia
 
Yanayosafirishwa kwa bomba ni mafuta ghafi sio haya tunayotumia.Yanakuwa hayajawa refined kwa matumizi.Nategemea pia serikali ya viwanda ya Magufuli yaweza jenga pia kiwanda cha refinery Tanga na kukifufua kiwanda chetu cha refinery cha Tipper kilichoko Dares salaam ili hayo mafuta ghafi yawe refined hapa hapa nchini kwa ajili ya soko la ndani na nchi za afrika mashariki na kati.Hii itaokoa pesa nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza mafuta yalitosafishwa toka nje ya nchi na yaweza isaidia thamani ya shilingi yetu kuwa imara sana.
Asante! Kama Kiwanda kipo tufanye kufufua tu ili tuweze kufanya biashara, tayari tunae Zambia, na majirani wote watakua wateja wetu, tununue mafuta ya Uganda turefine then tuuze hapa ndani na nje! Najua pia nasi tunayo mengi tu ila tuanze na yao kwanza
 
YEHODAYA, huu mradi kwa sasa ni mgumu au hauna faida kwa South Sudan, bomba la Uganda litakuwa na uwezo wa kupitisha pipa 200,000 kwa siku, South Sudan wenyewe wana uwezo wa kupitisha zaidi ya pipa 200,000 peke yao, sasa kuwaambia watumie bomba moja na Mganda lenye uwezo huo ni sawa kuwaambia wapunguze production. Kama lobbying inabidi ifanyike kabla ya ujenzi wa bomba la Uganda ili design na uwezo wa bomba uwe mkubwa zaidi ya hili wanalotegemea kujenga. Kwa hali ilivyo Uganda hawezi kukubali ku delay bomba lake ili zianze lobbying nyingine ambazo hana interest kubwa.
 
Hilo bomba bado halijaanza kujengwa.Kuna nafasi ya kufanyia marekebisho kama ukubwa wa bomba nk ili ku-mu accomodate sudan kusini kama ikikubalika na wahusika na wawekezaji wa hilo bomba.
 
Sina utalaam wa mafuta, mafuta ghafi na haya tunayotumia tofauti yake ni nini? Na hayo ya Uganda kupita tanga ni ghafi ama? Na yatokayo dar kwenda Zambia nayo ni yepi?
Ni hayo hayo ghafi, ncho zote husafirisha mafuta kwenye mabomba yakiwa ghafi kuepuka kuhujumiwa njiani
 
Mafuta ya Uganda ambayo wanataka kupitisha kwa bomba kwenda Tanga ni ghafi yanatakiwa kwenda kusafishwa ili wapate aina tofauti za
Mafuta ambayo tunazifahamu kama desel,petro, mafuta ya taa na kadhalika kwa maana nyingine bado yajawa tayari ya matumizi na bomba la mafuta la tazama hili lina pitisha mafuta ambayo tayari yamesha safishwa yapo tayari kwa matumizi sasa ndoto ya kuunganisha haiwezekani kwa kuwa ni aina tofauti
Ulichokisema sio kweli.

Mafuta ya Zambia ni mafuta ghafi, hayajasafishwa bado
 
Kama sudan kusini ikiunga bomba lake na uganda kupitia Tanga,Tanzania yaweza ongea na Sudan na Uganda na kampuni ya TOTAL kama wakipenda kujengwe bomba toka Tanga hadi Dar esalaam ambapo si parefu ili bomba hilo liunganishwe na lile la mafuta linalopeleka Mafuta ZAMBIA ambalo liko tayari.

Kuunga huko kutaisaidia Sudan kusini na Uganda kuuza mafuta mengine kwa kuyapakia kwenye meli na kupeleka nje ya nchi lakini pia kuyasafirisha hadi zambia.

Nchi hizo mbili zaweza kamata soko la Afrika mashariki yote na kati ikipitisha mafuta yake toka tanga hadi dar es salaam si mbali mtu akitaka kujenga bomba la mafuta ili liunganishwe na lile linaloenda zambia ambalo tayari lipo.

yehodaya123@gmail.com
Hapo lazima tutengeneze mshiko wa kutosha, tujenge viwanda vya kusafisha mafuta, ili mafuta yote ghafi kutoka hizo nchi yasafishiwe hapa kwetu.
 
Hilo bomba bado halijaanza kujengwa.Kuna nafasi ya kufanyia marekebisho kama ukubwa wa bomba nk ili ku-mu accomodate sudan kusini kama ikikubalika na wahusika na wawekezaji wa hilo bomba.
YEHODAYA , si rahisi kama hivyo, kubadilishia design ya bomba inamaanisha vilevile unaongeza gharama ya mradi wa bomba la Uganda to Tanga, ni nani wa kuongeze hiyo, si Uganda wala Total ambao ni wanufaika wa hilo suala la Sudan Kusini, hapa haujaanza kuongelea ujenzi wa bomba kutoka Sudan Kusini hadi Uganda.
Pili, kuna suala la muda hapa, Uganda wanataka kuanza production, usitegemee wa delay mradi wao ili kutufurahisha sisi. Tukubali tulichopata na tukubali makosa yetu ya kutojipanga tangu mwanzo, vingenevyo tulitakiwa kuwa na hizi plan kabla, na sio kusubulia mwisho wa mazungumzo ya deal la Uganda ndio tunaanza kufikiria opportunity nyingine ambazo hatuna uwezo nazo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom