Subtitles za Kiswahili kwa movies na series zote zinapatikana

Jan 2, 2022
6
8
Kwema wakuu!

Faida ya kuangalia Movie au Series ni kuelewa kiundani neno kwa neno na Story nzima. Kwa wale wapenda Movies na Series kutoka nje ya nchi ambazo hawatumii Kiswahili kama lugha mama, wanaelewa ugumu wa kushindwa kuelewa kinachoendelea kwenye Movie au Series husika sababu tu ya lugha.

Kuna Movies na Series nyingi ambazo mtazamaji anashindwa kupata radha kamili sababu ya lugha ngumu au umahiri mdogo kwenye lugha husika.

Mfano movie kama Inception, Interstellar au Tenet na nyingine nyingi za aina hiyo. Ila kama ingekuwa kwa Lugha mama ya Kiswahili basi asingebanduka kwenye kiti.

Utengenezaji wa Subtitles ni kazi ngumu kidogo hivyo utapata subtitles zako ndani ya masaa kadhaa baada ya malipo. Cha kufanya ni wewe unanipa jina la movie au kipande cha Series husika unafanya malipo alafu mimi nitakutumia kazi yako ndani ya muda wa makubaliano.

Utafanya malipo kabla ili kuepuka matapeli ambao watakuwa unawatumia kazi lakini hawafanyi malipo, Na pia malipo yatategemea na urefu wa Movie au kipande cha Series husika.

Kwa wale Watafsiri movies/Series hii itawarahisishia kutafsiri na kueleweka kwa ufasaha na watazamaji na kwa Wauzaji Movies na Series hii itaboost uuzaji sababu mteja atakuwa anaelewa Story kiundani zaidi.

Kwa wahitaji wote wa Subtitles zilizotafsiriwa kwa umahili wa hali ya juu kutoka Kiingereza, Kijapan, Kikorea, Kichina kwenda Kiswahili fasaha na rahisi kueleweka na kila mtu mnakaribishwa.

Kuwa na siku njema!
 
Mkuu ninachokijua mimi wabongo wanaelewa lugha zote. Zamani kipindi tunatumia deki za VHS tulikuwa tunaangalia movie za kihindi kwenye mabanda na tùnaelewa bila hizo subtitles. Tena unakuta mtu anakusimulia mwanzo mwisho.
 
Mkuu Mlatino Zeshalo.

ni kweli usemacho lakini kuna tofauti kubwa kati ya kuelewa kwa matendo na kuelewa kila neno na kinachoendelea kwenye movie.

Jaribu kuchukua movie yoyote unayoona umeielewa vizuri bila kutambua lugha husika alafu uweke subtitles za kiswahili, ni lazima uone na kujua mambo mapya ambayo huku yatambua mwanzo.
 
Yan kitendo cha kucopy Srt za movie na kuzipaste kwenye google translater ndo uwacharge watu pesa??? Kwel bongo kila kitu ni hela
Umejuaje kama nacopy mkuu?

Hapana bali naandika mwenyewe na kutafsiri mwenyewe neno kwa neno kwa kiswahili cha kawaida...

Situmii Google Translator au kama ni hivyo basi subtitles za kiswahili zingekuwa zimejaa kila sehemu na kila mtu angekuwa anafanya hata ww..

Kuandika mistari 3000 ya maneno sio kazi ndogo hivyo huwezi kufanya bure,, na kingine sio wote n wavivu kama wewe hvyo ni busara kukaa kimya na kupita kama hujapendezwa...
 
Umejuaje kama nacopy mkuu?

Hapana bali naandika mwenyewe na kutafsiri mwenyewe neno kwa neno kwa kiswahili cha kawaida.

Situmii Google Translator au kama ni hivyo basi subtitles za kiswahili zingekuwa zimejaa kila sehemu na kila mtu angekuwa anafanya hata ww..

Kuandika mistari 3000 ya maneno sio kazi ndogo hivyo huwezi kufanya bure,, na kingine sio wote n wavivu kama wewe hvyo ni busara kukaa kimya na kupita kama hujapendezwa.
Kuna watu hawawezi kukuelewa ila mimi nakuele2a. Google translator hata Google wenyewe hawaitumii kutafsiri data za search engine yao. Wanalipa watu kufanya hiyo kazi. Kwa hapa Tanzania wana ofisi pale posta chini ya kampuni ya Kenya inaitwa DDD kwa ajili ya kutafsiri results za kugoogle kwa kiswahili fasaha, na pia kureview results ambazo zimetafsiriwa tayari.

Hivyo huwezi tafsiri kila kitu kwa G translator
 
Umejuaje kama nacopy mkuu?

Hapana bali naandika mwenyewe na kutafsiri mwenyewe neno kwa neno kwa kiswahili cha kawaida...

Situmii Google Translator au kama ni hivyo basi subtitles za kiswahili zingekuwa zimejaa kila sehemu na kila mtu angekuwa anafanya hata ww..

Kuandika mistari 3000 ya maneno sio kazi ndogo hivyo huwezi kufanya bure,, na kingine sio wote n wavivu kama wewe hvyo ni busara kukaa kimya na kupita kama hujapendezwa...
Sawa mkuu. Mvivu mimi nakaa kimya sasa
 
Kuna watu hawawezi kukuelewa ila mimi nakuele2a. Google translator hata Google wenyewe hawaitumii kutafsiri data za search engine yao. Wanalipa watu kufanya hiyo kazi. Kwa hapa Tanzania wana ofisi pale posta chini ya kampuni ya Kenya inaitwa DDD kwa ajili ya kutafsiri results za kugoogle kwa kiswahili fasaha, na pia kureview results ambazo zimetafsiriwa tayari.
Hivyo huwezi tafsiri kila kitu kwa G translator
Pamoja sana mkuu kwa kuwa na uelewa chanya juu ya hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom