Subjects vs Citizens ukweli ni upi?

Ukweli ni kwamba hapa Tanzania Subjects ni wale wote wenye mawazo yanayopinga na ccm na serikali yake wakati citizen ni wanaccm wote. Ndiyo maana unaona citizen kama yule Shija wa Itigi pamoja na kuua anaendelea kuheshimiwa ila subject kama Mbowe ndiyo hivyo tena.
 
Subjects ni mateka ndani ya nchi yao kwa kisingizio cha kuleta maendeleo. CCM haiamini ktk uhuru na maendeleo kuwa ni mapacha wanaofanya watu ndani ya nchi kuwa wazalendo wa kweli.
 
Sisi ni Citizens ambao tuko kwenye transition ya kuwa subjects. Kama ukifuatilia mijadala ya humu JF, utagundua kuwa kuna kundi kubwa la watu ambao wanafikiri wanatetea nchi lakini kumbe wanatetea mtawala au utawala.

Watu wanaotetea mtawala ni subjects bila kujali anatawala au anaongoza. Dr Possi, Dr. Abbas, Masilingi na wengine wengi hawajali kusema uongo ili kumtetea bosi wao.
Subjects kwa sasa ni Mawaziri, Makatibu wakuu, Makamishna, Wakurugenzi, Makatibu Tawala, Wakuu wa Wilaya na Mikoa, sehemu kubwa ya wanachama wa CCM na UVCCM, watu aina ya Musiba, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na idadi kadhaa ya wananchi wa kawsida hasa wasio na elimu na masikini.

Watu waliozoea kuwa Citizens kwa sasa wanaishi bila uhuru, angalau wa kihisia. Uhuru wao unatoweka taratibu na wanalazimishwa kuwa subjects.
Ssali ni gwiji. Huwezi kukariri ukatoka salama kwenye fora anazoandaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona unaahidiwa viwanda na ajira kisha unaletewa ndege na flyover ujue wewe ni subject, si lolote si chochote.
 
Sikuwahi fikiri kama kuna watu outside of TZ wana uelewa mkubwa wa mambo ya hapa nyumbani kuliko sisi!
Na hilo watawala wanalijua ndio maana hawafurahii ziara chokonozi ya Lissu kwani itawachokonoa hao waseme au waulize Yale wanayoyajua.
Sisi ni subjects katika nchi yetu wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
f(subject)=g(kikokoteo kipya)
+ h(sheria ya vyama vya siasa) + z(maandamano tumerudishiwa kikokoteo cha zamani) - i v(1.5T Tsh)

Wanasema ni maziwa(citizens) lakini ukinywa utagundua ni tui la nazi(subjects).
 
"Citizens" should ideally apply in free democratic republics, and "subjects" would be what you would expect in kingdoms like Saudi Arabia, Brunei, and obscure totalitarian regimes like North Korea, Tajikistan and matter of fact, Tanzania.
 
Jibu lako ni lipi sasa umejikita kutoa Maana zaidi toa jibu Maana tuna jua teari tulisha fundishwa shuleni au unahisi ulisoma mwenyewe
Wakati tunatawaliwa na mkoloni sisi tulikuwa ni "subjects" lakini tulipopata uhuru wetu tukawa "Citizens" . Kwenye siasa "subjects" ni watu waliomo kwenye nchi inayotawaliwa bila ya wao kuwa na nafasi ya kushiriki kwenye kufanya maamuzi wao wenyewe yenye manufaa kwa maisha yao na vizazi zijavyo.

Lakini "Citizens" wao ni washiriki wa kwenye kila hatua ya kuendesha nchi yao na wao ndiyo asili ya mamlaka yote. Kwa mfano wananchi wa Uingereza wangekuwa ni "Subjects" wa Tanzania, basi wasingekuwa na uhuru wa kupiga kura ya maoni kuamua kujiondoa Umoja wa Ulaya bila ya Tanzania kukubali. Lakini wao ni "Citizens" wa Uingereza hivyo wana haki ya kujiamulia mambo yao wapendavyo bila ya kuomba ruhusa kwa mtu yeyote yule.

Swali la Shaka lilikuwa linamaanisha kwamba kwa Tanzania waliomo wanaamuliwa mambo na viongozi wao bila ya kuwa na nguvu ya kupinga. Maana "Citizens" wanayo haki ya kuwakatalia wanaowaongoza lakini "Subjects" hawana sifa hiyo. Venezuela wanapambana kutoka kuwa "Subjects" wa Maduro na chama chake na kuwa "Citizens" wa Venezuela.
 
Jibu lako ni lipi sasa umejikita kutoa Maana zaidi toa jibu Maana tuna jua teari tulisha fundishwa shuleni au unahisi ulisoma mwenyewe

Wewe jibu lako ni lipi?
 
"Citizens" should ideally apply in free democratic republics, and "subjects" would be what you would expect in kingdoms like Saudi Arabia, Brunei, and obscure totalitarian regimes like North Korea, Tajikistan and matter of fact, Tanzania.

Balozi ambaye ni senior lawyer anajibu kama mtoto asiyewahi kanyaga shule, nafikiri Masilingi ndo alikuwa wa kwanza ku prove kwamba we are Subjects!!
 
Hahaha yeye mwenyewe balozi ana enjoy favors za kuwa subject. Atajibuje swali gumu kama hilo zaidi ya kutetea.
 
Back
Top Bottom