Subirini kauli za vitisho, kiburi na majigambo kutoka kwa waliokosa maarifa na hatimaye kuwafanya wapinzani wawe "desperate"

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Baada ya mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari, kinachofuata ni wale vibaraka kuja na kauli za vitisho, kiburi, ubabe na majigambo katika kumjibu Mbowe.

Kauli ya Mbowe sasa ndio itakuwa mtaji wa watu kutafuta vyeo na uteuzi badala ya wao kutafakari na kukiri katika nafsi zao kuwa Boss wao ndio chanzo cha kumfanya Mbowe na wenzake waishiwe uvumilivu na kufikia kusema aliyoyasema leo hii.

Kitendo cha kuwafunga jela na kuwadhalilisha kama walivyolalamika,ndio kimewafanya wafikie ukomo wa uvumilivu na sasa wako desperate kufanya lolote kwa gharama yoyote na mimi sitowalaumu kwa lolote watalofanya na matokeo yake kwani ndio kilichokuwa kinatafutwa.

Hata hivyo, Corona ndio inaweza ikaepusha balaa hili japo kwa muda kwani wapinzani hawawezi kushinikiza mikutano na maandamano iwapo serikali itapiga marufuku mikusanyiko kwani hata wao wanaelewa watakosa support iwapo kutakuwa na mazingira kama hayo.

Pia, Mataifa ya nje yanayopinga huu ukandamizaji nayo yatatumia mwanya huu kutoa support kwa wapinzani hasa pale mabavu ya dola yatakapotumika bila busara.

Nimalizie kwa kusema: Mungu huwa na makusudi yake kwa kila jambo.
 
Hii issue walipewa nafasi kuimaliza wenyewe mapema wakashindwa kuitumia hiyo nafasi, sasa now imegeuka mtego kwao; waache uonekane umewaogopa au wapelekeni jela muendelee kunyooshewa vidole na mataifa wahisani.

Wakiwapeleka jela wamewaonea, sheria za Tanzania zinaruhusu mikutano ya siasa.

Kweli siasa inahitaji akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari, kinachofuata ni wale vibaraka kuja na kauli za vitisho, kiburi, ubabe na majigambo katika kumjibu Mbowe.

Kauli ya Mbowe sasa ndio itakuwa mtaji wa watu kutafuta vyeo na uteuzi badala ya wao kutafakari na kukiri katika nafsi zao kuwa Boss wao ndio chanzo cha kumfanya Mbowe na wenzake waishiwe uvumilivu na kufikia kusema aliyoyasema leo hii.

Kitendo cha kuwafunga jela na kuwadhalilisha kama walivyolalamika,ndio kimewafanya wafikie ukomo wa uvumilivu na sasa wako desperate kufanya lolote kwa gharama yoyote na mimi sitowalaumu kwa lolote watalofanya na matokeo yake kwani ndio kilichokuwa kinatafutwa.

Hata hivyo, Corona ndio inaweza ikaepusha balaa hili japo kwa muda kwani wapinzani hawawezi kushinikiza mikutano na maandamano iwapo serikali itapiga marufuku mikusanyiko kwani hata wao wanaelewa watakosa support iwapo kutakuwa na mazingira kama hayo.

Pia, Mataifa ya nje yanayopinga huu ukandamizaji nayo yatatumia mwanya huu kutoa support kwa wapinzani hasa pale mabavu ya dola yatakapotumika bila busara.

Nimalizie kwa kusema: Mungu huwa na makusudi yake kwa kila jambo.
Wamewekewa mtego wa kirahisi sana !
 
Back
Top Bottom