Subash Patel: Press Conference!

Apr 27, 2006
26,588
10,375
Haya wakuu nimepata hii SMS muda mchache sana uliopita, vipi imekaaje?:-

1. Subash Patel amefanya Press Conf leo saa tano Dar es Salaam.

2. Hakukuwa na taarifa zilizoeleweka kwani kwanza ilielezwa kwamba ingefanyika White Sand, baadaye kempiski lakini kote huko haikufanyika, ikafanyikia ofisini kwake (sijui wapi).

3. Inasemekana amejitetea kuhusu Mchuchuma na kusema yeye ana mahusiano na Mengi kibiashara kwa kuwa amenunua viwanda vya Mengi na huwa anatangaza ITV na hivi karibuni amelipa mamilioni kwa ITV.

4. Hakutukana na kurusha makombora kama RA, nanadhani wamejifunza.
 
Alieyzungumza ni public relations officer wake, Abubakary Mlawa. Ni kweli amekanusha kuhusiana na masuala ya Kiwira. Cha msingi alichokisema nu kwua kampuni ya Subhash MM Steal Resources Public ilishiriki katika kandarasi huko Mchuchuma kwa kufuata taratibu zote. Amsema Shubhash ni clean na bado anaendelea na biashara zake clean ba kumtaka Mengi kama ana ajenda yake aseme mja kwa moja na si kupakazia watu.
Hayo ndiyo niliyoyapata kutoka kwenye press conference hiyo
 
Sasa Mengi alipe hiyo Shilimgi moja .Kwa kumzushia mtu uwongo ,na kama aliyosema Mengi kwa huyu ni uwongo basi Mengi anaweza kwenda lupango.
 
Sasa Mengi alipe hiyo Shilimgi moja .Kwa kumzushia mtu uwongo ,na kama aliyosema Mengi kwa huyu ni uwongo basi Mengi anaweza kwenda lupango.

Patel? nawe unaamini kabisa aliyo yasema hivo coldly namna hii? Mwizi mkubwa, mwaka huu lazima wakome kutuibia they will face it!

By theway ulisha wahi kuona mwizi yeyote anaye kiri moja kwa moja hata akibanwa? hata huwa akizidiwa wana msingizia shetani kwamba kawasababishia. Patel yuko katika njia hiyo hiyo..
 
Sasa Mengi alipe hiyo Shilimgi moja .Kwa kumzushia mtu uwongo ,na kama aliyosema Mengi kwa huyu ni uwongo basi Mengi anaweza kwenda lupango.

Ndo maana Nyerere aliweka shule za ngumbalu, zilisaidia sana wananchi kujua kilichokuwa kinafanyika nchini, sasa hivi hizi shule hakuna, ndo maana watu wengi utindio wa ubongo umeongezeka.
 
FROM MWANANCHI

Subash Patel: Tofauti za kibiashara zisiwe chanzo cha malumbano

Boniface Meena

BAADA ya kimya kingi, mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Subhash Patel, jana aliibuka na kujibu tuhuma za ufisadi papa zilizotolewa na mfanyabiashara mwenzake, Reginald Mengi huku akisema kuwa kama kuna tofauti, basi "zitatuliwe kibishara na si kuchafuana".

Patel anakuwa mtu wa tatu kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na Mengi dhidi ya watu watano aliowaita kuwa ni mafisadi papa, akidai kuwa ni miongoni mwa watu 10 wanaoifilisi nchi.

Wengine ni mfanyabiashara Rostam Aziz, ambaye mbali na kukanusha tuhuma dhidi yake, alimwaga mlolongo wa tuhuma dhidi ya Mengi na kuwasilisha vielelezo ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili ianze kumchunguza.

Mwingine ni mfanyabiashara Yusuf Manji, ambaye siku ya tuhuma alijibu kwa kifupi tu kwamba Mengi ana wivu, chuki na ubaguzi na mwishoni mwa wiki aliwasilisha malalamiko kwenye Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akidai mwenyekiti huyo wa IPP hakumtendea haki alipomwaga tuhuma kwenye televisheni yake na hivyo anataka kituo hicho kifungiwe kwa wiki moja.

Jana ilikuwa zamu ya Patel ambaye alikanusha tuhuma na kudai kwamba kama kulitokea matatizo katika uhusiano wake na Mengi kibiashara, basi hakuna budi kuyatatua kibiashara na si kwa kuchafuliana majina.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, ofisa uhusiano na mawasiliano wa kampuni inayoimilikiwa na mfanyabiashara huyo ya Motisun Holdings Limited, alisema Patel hana kampuni ambayo imewahi kupewa mradi wowote kati ya eneo la mradi wa chuma wa Liganga na makaa ya mawe ya Mchuchuma.

"Kuhusu tuhuma alizotoa Mengi katika mradi wa chuma wa Liganga na makaa ya mawe ya Mchuchuma, si Patel wala kampuni yake yoyote iliyopewa mradi wowote katika eneo la mradi wa makaa ya mawe," alisema ofisa huyo, Aboubakary Mlawa.

Alifafanua kuwa kilichopo ni kwamba moja ya kampuni za Patel iitwayo MM Steel Resources Public Limited ndiyo iliyoshiriki katika zabuni ya kutafuta mwekezaji wa ndani Aprili mwaka 2008 ili awe na ubia na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), katika kuzalisha na kuendeleza mradi wa kuzalisha chuma kiitwacho 'sponge' na siyo kampuni iliyotajwa na Mengi na vyombo vyake vya habari.

Kuhusu tuhuma za kutoa rushwa kwa wanakijiji wa vijiji mbalimbali ambavyo havikutajwa na Mengi, Mlawa alisema kuwa Patel hajawahi kutoa rushwa kwa wanakijiji wa kijiji chochote katika sehemu yoyote ya Tanzania.

Alibainisha kuwa anachofanya Patel ni kutumia haki aliyonayo kusaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kijamii hapa nchini.

"Makampuni yametoa misaada mbalimbali ya maendeleo na ya kijamii inayozidi thamani ya Sh800 milioni," alisema.

Kuhusu umiliki wa gazeti la Sauti Huru, ofisa huyo alisema kuwa Patel hamiliki, hafadhili, wala hana hisa katika gazeti hilo wala chombo kingine chochote cha habari kama Mengi anavyomtuhumu.

Akizungumzia madai ya kutorosha fedha nje ya nchi, alisema Patel hajawahi kufanya kitu kama hicho kwa kuwa anatambua hilo ni kosa la jinai kwa sababu yeye ni Mtanzania.

Alisema kuwa kutokana na tuhuma hizo Patel angependa kujua ni nini hasa kiini cha kuchafuana majina na kuchonganishana kwa jamii kunakofanywa na Mengi dhidi yake.

Alisema kuwa bado hajafikia uamuzi wa kwenda mahakamani, lakini akiamua atakwenda kwenye chombo hicho cha sheria.
 
Mlawa, Mlawa, Mlawa... kweli uko tayari kwa hili? haya shauri yako.
Simjibii Mlawa ila yeye ni mtumishi wa Patel kama watumishi wengine yeye ni pro kazi yake ni kusafisha. Kazi ambazo waandishi wa petty cash journalism wanazitafuta angalau waondokane na kuchumia juani. Hiyo job itamfikisha mahali pazuri zaidi mbele ya safari, si unaona alipo pro wa RA.

Mlawa chapa kazi huo ndio uzalendo uzalendo wa kweli usio angalia rangi ya mtu. Mtumikie kafiri upate mradi wako. Kazi ni kazi, bora mkono uende kinywani. Chumia tumbo mwanangu, wenzako wanakula mapande ya nyangumi, kula papa kula mwanangu kabla nyangumi hajameza papa wote.
 
tutaonana wabaya hayaaaa.....:)
 
Alieyzungumza ni public relations officer wake, Abubakary Mlawa. Ni kweli amekanusha kuhusiana na masuala ya Kiwira. Cha msingi alichokisema nu kwua kampuni ya Subhash MM Steal Resources Public ilishiriki katika kandarasi huko Mchuchuma kwa kufuata taratibu zote. Amsema Shubhash ni clean na bado anaendelea na biashara zake clean ba kumtaka Mengi kama ana ajenda yake aseme mja kwa moja na si kupakazia watu.
Hayo ndiyo niliyoyapata kutoka kwenye press conference hiyo

Je na wewe ulipokea bahasha? na mlikuwa na nini ndani yake?
 
cha kujiuliza KUBENEA wa MWANAHALISI kwa nini alichomoa press conference ya kuumaliza Rostam wiki iliyopita?

halafu mnataka kutuambia eti wengine wako clean

tukianza kufumuana kutakuwa hakukaliki humu
 
cha kujiuliza KUBENEA wa MWANAHALISI kwa nini alichomoa press conference ya kuumaliza Rostam wiki iliyopita?

halafu mnataka kutuambia eti wengine wako clean

tukianza kufumuana kutakuwa hakukaliki humu

usizungumzie vile vibasha halali vya usafiri, hii ni deal kubwa la kuchumia tumbo. Kubenea kwenye somo hili, lazima afunge mdomo, RA kalimlipua yuko payroll ya Mangi, bado kanyamaza.nilisema kwa waandishi wa petty cash journalism, huu ni mwaka wa mavuno.
 
cha kujiuliza KUBENEA wa MWANAHALISI kwa nini alichomoa press conference ya kuumaliza Rostam wiki iliyopita?

halafu mnataka kutuambia eti wengine wako clean

tukianza kufumuana kutakuwa hakukaliki humu

Tunacho hitaji ni kuwaweka hadharani manyangumi na mapapa ila kauli ya vitisho vya kutokalika itatufanya tukuwekee alama za (???????)
 
Back
Top Bottom