Kuna tofauti gani kati ya Home Theatre na Sub-woofer?

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,698
Pink and Red Beauty Influencer Asymmetrical Overlays Facebook Cover.png

Wakuu mimi siyo mpenzi wa mziki wa sauti ya juu ila ni mpenzi wa vitu vizuri.

Mwanzo nilikuwa nafikiri sub woofer ni mchina tu kumbe kuna sub woofer za brand kubwa tu.

Fikra zangu za kufikiri sub woofer ni mchina zilinifanya nisipende subwoofer kabisa hivyo mimi ni mwendo wa home thatre tu.

Sasa je kuna tofauti gani kati ya subwoofer na hometheatre na je hakun sub woofer zinazokuja complete n deck yake kama home theatre?

MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI
KATIKA MASUALA YA SAUTI NA FILAMU, HII NDIYO TOFAUTI

Kwa kitaalamu kwenye maswala ya sauti za filamu na mUziki Woofer ni loudspeaker, ambayo inauwezo wa kutoa frequency za chini za sauti kwa mujibu wa vipimo vya THX ( hawa ni watengezaji wavifaa vya sauti vyenye uwezo wa Hi-Fi yani high fidelity kwa lugha ya kikwetu kwamba zenye kutoa sauti zinazo akisi uhasiria) speaker zenye kutoa frequency kati ya 80-20Hz hizi ni Woofer au Bass kwa mujibu wa THX na kati ya 20-100Hz hizi ni Woofer kwa viwango vilivyo wekwa kwa matumizi ya Kitaalamu, speaker zenye kutoa frequency kati ya 20-200 hizi ni woofer kwa matumizi ya majumbani, kwakuwa matumizi ya kitaalamu yanahitaji frequency kati ya 20-100Hz hivyo basi speaker zenye kutoa frequencey juu ya hapo hazi tambuliki kama woofer ama bass speaker na hivyo wataalamu wakaamua kuziita ni sub woofer ama sub bass na kwakuwa sound system ambazo zinatengenezwa kwa matumizi ya nyumbani huwa hazitumii gharama kubwa kuliko zinazo tenegenezwa kwa matumizi ya kiprofessional.

Watengenezaji hawaoni haja ya kuunda speaker za woofer ambazo nigharama kwaajili ya matumizi ya nyumbani na hivyo hutumia speaker ambazo hazina uwezo mkubwa wa kukata frequency za kati na za juu na kuziweka kwenye sanduku la mbao ilikuongeza mvumo wa frequency za chini na hivyo kuweza kutengeneza sauti zenye frequence kati ya 200-20Hz ambapo kitaalamu haziwezi kuwa woofer au bass bali huitwa sub woofer au sub bass.

Kwa upande wa Home theater
huu ni mjumuisho wa vifaa vya sauti na picha ambapo kwa pamoja hutengeneza mazingira ya sauiti kama tunazo zisikia kwenye majumba ya sinema ndio maana Home theater pia hufaamika kama Home cinema yani sinema majumbani.

home theater pia inamaana ya sound system ambayo inauwezo wa kufoji sauti za surrounding yani sauti ambazo hufanya msikilizaji kuhisi muelekeo na sehemu sauti inapotokea, mfumbo mdogo kabisa ni wa channel 2.1 ambapo huwa na mid speaker mbili na sub bass au sub woofer moja, mifumo mingine ni kama ile ya 5.1 channel ambayo kwa sasa hadi majumbani watu wanatumia na kuna ya 7.1 channell malanyingi matumizi yake huwa ni sinema.

Sub-woofer ni moja speaker katika set ya home theater maranyingi huwa inajitegemea kwenye chanzo cha nishati ama hutegemea amplifier inayo endesha speaker zingine inatabaia ya kutotoa vizuri frequency za juu na za kati kama vile mazungumzo ama milio ya kengere na inayofanania na hiyo.
Home Threatre ni Spika zinazowekwa ndani ili uweze kupata sauti nzuri na effect zake kwenye 3D. Kwa mfano kama umefunga vizuri Spika zako na ukawa na Screen kubwa, kama mtu anatokea tuseme upande wa kushoto basi utasikia sauti zikitoka pia kushoto na akifika katikati utasikia sauti ipo katikati na akienda kulia na kupotea pia utasikia sauti zipo kulia.

Kwenye majumba ya Cinema, zile Screen zake na kuta za jumba la Cinema zimejazwa Spika ili kuleta hiyo effect ya 3D Sound. Ila kwa sababu gharama ni kubwa sana, nyumbani inaishia kuwa na Spika 5.1 au 7.1 na katika hizo, moja huwa ni ile ya katikati na Subwoofer inakuwa ni uamuzi wa mnunuzi au watengenezaji.

fd766ca9_vbattach205453.jpeg

174487-Behind-A-Movie-Theater.jpg

Hii ni Screen ya IMAX. Ni kubwa na ndefu sana. Ila unaona jinsi Spika zinavyojazwa. Kwa Theatre mpya, zinakuwa nyingi zaidi ila ndogo ndogo.

Kama inavyoonyeshwa kwenye picha ya kwanza, Sub Woofer anaweza kuchangia kwenye Homethreatre kama Subset au akasimama mwenyewe. Kwenye Spika kubwa za Concert za wanamuziki maarufu, Subwoofer zinakuwa chini ili zitetemeshe Bass ya kutosha.

Chini ni kwa ufupi jinsi Sub woofer zinavyotumika kwenye kumbi kubwa. Ni hizo chini.

Subwoofer kwa kawaida wanaigeuza Spika na unakuwa unasikia kwa nyuma ambako kwa kawaida kuna Bass kubwa zaidi. Spika za kawaida zile Spika zake zinakuwa zimeangalia mbele.

170226_in2.jpg

Hapa waweza kuona kuwa upande wa kushoto ni Spika ya kawaida na kulia ndiyo Spika ya Sub Woofer.Ili kuilinda wanaweka tundu la duara au kuweka wavu kama picha ya juu zaidi ya spika za JBL. Hii ya kushoto huwa hawaijali sana kwani hata kuitengeneza ni rahisi. Nadhani materials yanayotumika kwenye Spika ya kulia (Sub Woofer) ni ghali sana. Ndiyo maana Sub woofer zinakuwa ghali mno.

Nategemea utakuwa umeelewa kwa ufasaha tofauti yake na wapi zinatumika na zimetengenezwaje kwa ufupi sana.
PATA UFAHAMU HUU
Sub Woofer ni kifaa kinachojitegemea mara nyingi. Ila kuna watengenezaji walikuwa wakiziweka pamoja na kutumia Sub Woofer kama Amplifier na huku DVD/Bluray ikitumia kama vyanzo vya sauti zote. Sub Woofer ilikuwa na matundu ya kugawa sauti kwa spika nyingine. Wengine walitumia DVD/Bluray kama pia Amlifier/Amplituner yaani inakuwa na Radio. Hapo sasa hata Sub Woofer na yeye aligawiwa sauti ila hakuwa ana umeme wakati ya juu inakuwa inaingiza umeme ili kukuza sauti.

Kuna watu kama ONKYO nimeandika, wao wanatengeneza zaidi Amplifier kwa ajili ya Homethreatre. Spika unaenda kununua unapotaka kutegemea na uwezo wako. DVD/Bluray pia unanunua unapotaka. Mwenyewe natumia ONKYO na kwa kweli ni nzuri sana. Sijanunua Sub Woofer kwani Spika za mbele ni kubwa na zinanipa Bass ya kutosha ingawa si kubwa sana kama ukiwa na Sub Woofer ya ukweli.

Spika nzuri ni ghali sana hasa hawa watu wa JBL, Bose, Martins, QSC nk. Ila kwa ufupi Harman Industr. ambaye ndiye Mama wa hawa akina JBL, Martins, Harman Kardon (Magari), Bang & Olufsen etc ndiyo anatamba sana kwa kuwa na Spika za aina nyingi na za High Quality.
Kwa sasa OWNER ni SAMSUNG ambapo aliinunua kwa Mabilioni kadhaa ya US $.

Onkyo lattest Product katika ubora wake wa 7.2 pamoja na THX yaani THomson Experience ambayo ilitumika mara ya kwanza kwenye Sound system ya film ya Star War. Kitu hicho TX-RZ900. Check CHURA wake alivyoshiba.
SUB-WOOFER INAPIGA BASS PEKE YAKE, HOME THEATRE NI SYSTEM TEGEMEZI
MKuu ngoja nijitahidi kukuelezea hizi vitu at the easiest way possible.
Sub-woofer: Ni speaker inayopiga sauti ya Bass peke yake. Toka zamani sub-woofer zilikuwepo ila tu zilikuwa zinachanganywa na spika nyingi kwenye Box moja. Kwa kadri teknolojia ya sauti ilivyozidi kukua, ikagundulika kwamba pia kuna uwezo wa kuitenga(kuiweka pekeyake) spika ya bass ilikuweza kupata mkito bora zaidi.

Home Theater: Ni system tegemezi ya kuendesha pia kutawanya sauti kutoka kwenye chombo kingine. Home theater pia ili iweze kuitwa hivyo lazima iwe na mkusanyiko wa sipika za aina mbali mbali kama Sub-woofer, spika za kati, na spika za tweeter.

Kwahiyo: Subwoofer ni sipika itowayo sauti ya Bass tuu na yenyewe kama yenyewe haichezi kitu mpaka iunganishwe na kitu kingine... Sijui Umeelewa??

Kuhusu uimara: Kwa kweli ni matumizi yako, Kwa umeme, ziku zote uwe na protection kwa vyombo vyako. Lakini pia katika hivi vyombo kuna swala zima la matumizi ya nyumbani na matumizi ya biashara. Sasa ukinunua chombo cha matumizi ya nyumbani ukakitumia kwenye matumizi ya biashara, hakitakaa sana kitaharibika tuu. Ndiyo maana kuna Kuna vyombo vya kupigia mziki wa biashaya na mziki wa majumbani.

Natumaini sijakukwaza na maneno yangu mengi kama mganga wa kienyeji..!!!
FAHAMU TOFAUTI HII. TUMIA USHAURI HUU UNAPOFANYA MANUNUZI

Sub-woofer ni kweli kabisa kama ulivyoielezea lakini kwa siku hizi "terminology" hiyo hususan hapa kwetu wameifanya kuwa ni (loud speaker) moja inayojumuisha speaker zingine zote (full range drivers) ambazo hujumuisha (sub woofer (kama ulivyoelezea), woofer, tweeter, quack er kwenye jumba moja kama hivi:

View attachment 500425
Ubora wa sub-woofer na ughali wake hutegemea na mtengenezaji (manufacturer) ni nani, zenye ubora na ambazo ni ghali sana ni za akina TL, Tech TRW, Royal device, Paradigm, Bose, JB, na kadhalika ambazo hapa kwetu ukikuta zenye majina hayo dukani uchunguze sana itakuwa ni "fake", sana sana utayakuta kwa watu walionunua nje ya Tanzania na kuzileta.

Home Theater kwa maana yake halisi ni sehemu (chumba / ukumbi) wa nyumbani wa kutazamia sinema (movie) uliokamilika kwa kuwa na "video display" au "video screen" na system ya muziki uliokamilika na kusheheni vionjo vyote "different type of speakers" kama nilivyozitaja hapo juu bila kusahau vionjo kama "surround", "dolby", pro logic, audyssey DSX na kadhalika na vyenye ubora wa "theater quality". Kama hivi:

View attachment 500427

Hii tunayooita siku hizi kuwa ni "home theater" ambayo ni "common" sana huku kwetu hujumuisha "sound system" pekee, hii kwa jina haswa ni "Home Audio system" ambayo husemwa ni "5:1 sound channel system".

Kwa hiyo kwa ufupi, redcarpet, baada ya kuzielewa hizo system, mimi nnakushauri nenda madukani katazame "home audio system" inayoendana na mfuko wako, iwe "sub woofer" au "home audio system" ambayo wengi hapa hujidanganya kuwa ni "home theater". Lakini Home theater per say, ni uongo, si wengi Tanzania hii wanayoweza kuimudu.

Sub woofer yangu hii:
MAANA NYEPESI
For simplest meaning
Haya ma wofer ya kichina ni 2.1 channel music components.
Yaani ni kama system za music za stereo ambazo kuna two tracks of sound zinazo play simultaneous. Ina depend na paning na delay.

Home thieter

Hii ni advanced music component au system ambayo ina 5.1 channel. Yaani kuna track 5 za sound ambazo zina play kwa wakat mmoja.
Ndio maana home thieter ina spika 5 za midi.

Zile spika zinafungwa katika mtindo wa soround ili kutoa mziki ambapo music instruments kila moja inaweza kuwa paned kwenye spika yake

Spika 5 zina mpangilio wake unapokuwa umeziweka chumbani. Na ukifanikiwa kuzipanga vizuri ndio utajua music ni nini na nini maana ya 5.1 channel music.

Speaker 3 za midi hukaa mbele ya chuma au sebule moja kushoto moja kulia na nyingine katikati.
Yaani front left front right na front centre.

Kisha nyuma ya chumba au sebule zinakaa spika mbili moja kushoto na nyingine kulia. Yaani back left na back right.
Kisha kile kinu chake yaani subwoofer yake inakaa mbele katikati pamoja na spika ya front centre.

Kisha sasa tafuta mziki ambao ni 5.1 channel. Unaweza udownload mtandaoni. Hasa ni kwa nyimbo za ulaya na marekani ndio baadhi zina mfumo huu. Baada ya hapo play uo wimbo.

Kama wewe ni mpenzi wa music utasikia mambo ya ajabu ambayo hujawahi kusikia. Maana mziki unapigwa standard pia utasikia effects zikilia katika baadhi tu ya spika. Au unaweza sikia kinanda kinalia spika ya kushoto na guitar linalia kulia, drum za tumba zinalia spika za nyuma basi ni utamu mtupuuuu

Ili upate uhalisia wa music huu inabidi ukae katikati ya chumba au sebule.

Kuna makampuni mengi yanayo tengeneza home thieter. Kuna Sony Samsung na Lg. Hizi ndio popular brands za HT hapa tanzania pia unaweza kuzikuta brand nyingine mitumbani hata madukani.

Music huu usipojua kuufunga hautakuwa na quality yoyote. Itakuwa ni kama subwofer la kichina la sea piano.

Pia kuna advantage ya kutumia hii system maana ina DVD player, USB, Radio, HDMI na amenities nyingine itategemea na technology. So ukinunua hii huna haja ya kununua deki sijuu na nini.

Pia kwa wale wenzangu wa kupenda Muvies hii kitu ni tamu sanaaaaa
Hasa ukiwa na Tv. Ya kama 50 inches af ukae distance fulani af pembeni una coke baridi huku unachek muvie ya 4k resoulution
Hakika ni maisha matamu sana

Pia kama wewe ni gemer
Hii kitu si kuiacha hasa kwa wenye PS 3 na 4 pia na wale wa Xbox pia
Utapata kusikia efects tamu sana za game
SUBWOOFER NI CHEAP KWA KILA KITU UKILINGANISHA NA HOME THEATRE
Home theatre ni multipurpose entertainment systems ambazo zinakuwa na channels 5.1 mpaka 7.1

Hizo channels zinawakilisha mid, high na low.

Namba 5 au 7 inawakilisha idadi ya speaker za mid na high za HT husika yani front, center na back wakati 1 inawakilisha bass ama subwoofer yake.

Kila spika kati ya hizo ina kazi yake ili kufanikisha kutoa sauti iliyokusudiwa na mtengenezaji wa content unayoicheza kwenye HT.

Mfano kama ni movie basi radi itatoka kwenye bass, ndege ataskika kwenye front left, upepo utauskia center, ving'ora vya gari utavisikia back, magazine ikianguka utaiskia front right.

Effect zote zinaweza tokea pamoja ila utashangaa jinsi sauti inavyogawanywa na hapo ndipo utamu wa home theatre ulipo.
Unaweza tumia hometheatre kwa kuinjoy mziki, movie, videos ama games.

Kwa upande wa subwoofer yenyewe huwa haina mbwembwe nyingi. Huwa ni speaker ya low yani inatoa sauti zenye asili ya bass tu ingawa huwa inasindikizwa na mid mbili yani Left & Right hivyo kutengeneza 2.1 channel system.

Sabufa si nzuri sana kulinganisha na hometheatre maana inaweza kuwa inapiga sound flani vizuri ila nyingine zikawa na distortion tofauti na hometheatre ambazo baadhi zina uwezo wa kupiga sounds tofauti yani dynamic sounds. Kifupi subwoofer ni cheap katika kila kitu compared to HT.

Naongea kwa uzoefu, im a sound system enthusiast toka nipo chalii. Sony, JVC, Panasonic, Kenwood ndio walikuwa kiboko in 90's era.

Kwa sasa amebaki Sony na Panasonic pekee ndio waliopo mainstream kwa hometheatre zenye akili kibongo bongo especially ukipata yenye watts 1000.Usinunue takataka ya mkorea LG ama Samsung, wale ni wazuri kwenye display tu.

I recommend Sony maana ndio naitumia sahivi model dav-dz650. spika 2 wima na ndogo 3 unaipata kwa Tsh.750k. Kuna nyengine yake ya 650k ila spika zake ni zile ndogo sio za wima ila watts 1000 pia. Balaa lake utakuja kunipa mrejesho mkuu.

Cheki @nafuu_electronics instagram utapata address ya duka niliponunulia.
 
Home theatre inakuwa imekamilika kwa kila kitu mfano deki, spika za aina zote, remote, pia kwenye home theatre unapata specification zaidi km HDMI port, Bluetooth, FM , na vingine vingi.
 
Home Threatre ni Spika zinazowekwa ndani ili uweze kupata sauti nzuri na effect zake kwenye 3D. Kwa mfano kama umefunga vizuri Spika zako na ukawa na Screen kubwa, kama mtu anatokea tuseme upande wa kushoto basi utasikia sauti zikitoka pia kushoto na akifika katikati utasikia sauti ipo katikati na akienda kulia na kupotea pia utasikia sauti zipo kulia.

Kwenye majumba ya Cinema, zile Screen zake na kuta za jumba la Cinema zimejazwa Spika ili kuleta hiyo effect ya 3D Sound. Ila kwa sababu gharama ni kubwa sana, nyumbani inaishia kuwa na Spika 5.1 au 7.1 na katika hizo, moja huwa ni ile ya katikati na Subwoofer inakuwa ni uamuzi wa mnunuzi au watengenezaji.

fd766ca9_vbattach205453.jpeg

174487-Behind-A-Movie-Theater.jpg

Hii ni Screen ya IMAX. Ni kubwa na ndefu sana. Ila unaona jinsi Spika zinavyojazwa. Kwa Theatre mpya, zinakuwa nyingi zaidi ila ndogo ndogo.

Kama inavyoonyeshwa kwenye picha ya kwanza, Sub Woofer anaweza kuchangia kwenye Homethreatre kama Subset au akasimama mwenyewe. Kwenye Spika kubwa za Concert za wanamuziki maarufu, Subwoofer zinakuwa chini ili zitetemeshe Bass ya kutosha.

Chini ni kwa ufupi jinsi Sub woofer zinavyotumika kwenye kumbi kubwa. Ni hizo chini.

Subwoofer kwa kawaida wanaigeuza Spika na unakuwa unasikia kwa nyuma ambako kwa kawaida kuna Bass kubwa zaidi. Spika za kawaida zile Spika zake zinakuwa zimeangalia mbele.

170226_in2.jpg

Hapa waweza kuona kuwa upande wa kushoto ni Spika ya kawaida na kulia ndiyo Spika ya Sub Woofer.Ili kuilinda wanaweka tundu la duara au kuweka wavu kama picha ya juu zaidi ya spika za JBL. Hii ya kushoto huwa hawaijali sana kwani hata kuitengeneza ni rahisi. Nadhani materials yanayotumika kwenye Spika ya kulia (Sub Woofer) ni ghali sana. Ndiyo maana Sub woofer zinakuwa ghali mno.

Nategemea utakuwa umeelewa kwa ufasaha tofauti yake na wapi zinatumika na zimetengenezwaje kwa ufupi sana.

Wakuu mimi siyo mpenzi wa mziki wa sauti ya juu ila ni mpenzi wa vitu vizuri.
Mwanzo nilikuwa nafikiri sub woofer ni mchina tu kumbe kuna sub woofer za brand kubwa tu.

Fikra zangu za kufikiri sub woofer ni mchina zilinifanya nisipende subwoofer kabisa hivyo mimi ni mwendo wa home thatre tu.

Sasa je kuna tofauti gani kati ya subwoofer na hometheatre na je hakun sub woofer zinazokuja complete n deck yake kama home theatre?
 
Home Threatre ni Spika zinazowekwa ndani ili uweze kupata sauti nzuri na effect zake kwenye 3D. Kwa mfano kama umefunga vizuri Spika zako na ukawa na Screen kubwa, kama mtu anatokea tuseme upande wa kushoto basi utasikia sauti zikitoka pia kushoto na akifika katikati utasikia sauti ipo katikati na akienda kulia na kupotea pia utasikia sauti zipo kulia.
Kwenye majumba ya Cinema, zile Screen zake na kuta za jumba la Cinema zimejazwa Spika ili kuleta hiyo effect ya 3D Sound. Ila kwa sababu gharama ni kubwa sana, nyumbani inaishia kuwa na Spika 5.1 au 7.1 na katika hizo, moja huwa ni ile ya katikati na Subwoofer inakuwa ni uamuzi wa mnunuzi au watengenezaji.

fd766ca9_vbattach205453.jpeg

174487-Behind-A-Movie-Theater.jpg
Hii ni Screen ya IMAX. Ni kubwa na ndefu sana. Ila unaona jinsi Spika zinavyojazwa. Kwa Theatre mpya, zinakuwa nyingi zaidi ila ndogo ndogo.

Kama inavyoonyeshwa kwenye picha ya kwanza, Sub Woofer anaweza kuchangia kwenye Homethreatre kama Subset au akasimama mwenyewe. Kwenye Spika kubwa za Concert za wanamuziki maarufu, Subwoofer zinakuwa chini ili zitetemeshe Bass ya kutosha.

Chini ni kwa ufupi jinsi Sub woofer zinavyotumika kwenye kumbi kubwa. Ni hizo chini.

jbl-pro-srx-7186-18-subwoofer.jpg

Subwoofer kwa kawaida wanaigeuza Spika na unakuwa unasikia kwa nyuma ambako kwa kawaida kuna Bass kubwa zaidi. Spika za kawaida zile Spika zake zinakuwa zimeangalia mbele.

170226_in2.jpg

Hapa waweza kuona kuwa upande wa kushoto ni Spika ya kawaida na kulia ndiyo Spika ya Sub Woofer.Ili kuilinda wanaweka tundu la duara au kuweka wavu kama picha ya juu zaidi ya spika za JBL. Hii ya kushoto huwa hawaijali sana kwani hata kuitengeneza ni rahisi. Nadhani materials yanayotumika kwenye Spika ya kulia (Sub Woofer) ni ghali sana. Ndiyo maana Sub woofer zinakuwa ghali mno.

Nategemea utakuwa umeelewa kwa ufasaha tofauti yake na wapi zinatumika na zimetengenezwaje kwa ufupi sana.
Asante kwa somo zuri mkuu
 
MAREKEBISHO TAFADHALI:
Kwa kawaida namba kubwa inatangulia. Kwa maana hiyo ulitakiwa kuandika 2.1, 5.1, 7.1 nk. Angalia ile picha niliweka juu kuhusu 7.1. Maana ya 1 SUB WOOFER. Mwanzo nilikosea na wewe ulikuwa sawa. My apology!!!!

Sub Woofer zinakuwa zinajitegemea. Ila kuna watengenezaji wengine wanaziunga na Deck yake ya DVD au Bluray yake pamoja na Spika zake zote 5. Ila wengi sasa hizi wameacha na kwa sababu ilikuwa kifaa kimoja kikiharibika basi imekula kwako System nzima.

1245px-5-1-surround-sound.svg.png

Hata hizo unazoziita subwoofer ni home theatre tofauti tu. Kuna
1.2,1.3,1.5 & 1.7 pia kuna 2.7. Yani hiyo moja moja hapo ndio subwoofer za sauti nzito hizo 1,2,3,5,7 ni spika ndogo za sauti nyepesi.
 
Inaweza kuwa hivyo ila SI LAZIMA iwe hivyo. Kwa mfano ONKYO anatengeneza Amplituner za Homethreatre nzuri sana ila si mtengenezaji mzuri wa Spika. Hapo inabidi ukachukua Spika za wataalamu.

Kwenye majumba makubwa maarufu duniani, Spika za MARTIN, kampuni ya UK ndiyo zinatamba sana.

MartinLoganCinema-1.png

Tofauti ni kwamba home theatre iko full ni pamoja na Deck na spika zake zote inakuwa set nzima Sub woofer ni yenyewe tu na Spika zake mbili na yenyewe jumla zinakuwa 3
 
Kwa kawaida namba kubwa inatangulia. Kwa maana hiyo ulitakiwa kuandika 2.1, 5.1, 7.1 nk. Angalia ile picha niliweka juu kuhusu 7.1. Maana ya 1 ni Msikilizaji au mlengwa/walengwa wa sauti ili kufaidi kwa utamu zaidi hizo sauti kwenye 3D.

Sub Woofer zinakuwa zinajitegemea. Ila kuna watengenezaji wengine wanaziunga na Deck yake ya DVD au Bluray yake pamoja na Spika zake zote 5. Ila wengi sasa hizi wameacha na kwa sababu ilikuwa kifaa kimoja kikiharibika basi imekula kwako System nzima.

1245px-5-1-surround-sound.svg.png
Asante kwa marekebisho yake. Ila wengi huwa hawaelewi wanadhani ikiwa na spika tano na kuendelea ndo hometheatre kumbe si kweli ila zote ni home theatre tofauti tu ni idadi ya speaker haijalishi amplifier iwe ya ndani ya ile sub au iwe imeundwa peke yake. Ila tu ikiwa na spika kuanzia tano ndo inakuwa na sound nzuri zaidi ya 3d kwani wakati zinapiga mziki zinakuwa kama zinapokeana beat.
 
Hizo za mchina ni home theatre ila za chini ya kiwango na nyingi ni 2.1 ambazo mchina amemodify kwa kuzuwejea socket ya usb na radio. Ila subwoofer ni speaker inajitegemea designed special kwa ajili ya kutoa bass(low frequences) kwa kuwa kava lake ni gumu na zito tofauti na speaker za kawaida.

Subwoofer inaweza kuwa passive kwa maana inahitaji external amplifier special designed for low frequences, na pia inaweza kuwa active, yaani subwoofer ambayo ina amplifier tayari imetengenezewa .
 
Kuna hizi zinazoitwa Aborder zenyewe zina redio, sehemu ya kuchomeka Card reader na flash na zina vispeaker vyake viwili, nazo ni home theater au sub woofer?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom