Suali kuhusu zile kazi za EAC zilizotangazwa hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suali kuhusu zile kazi za EAC zilizotangazwa hapa

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mtanzania in exile, Feb 27, 2012.

 1. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Habari zenu wandugu,

  Niliangalia yale matangazo ya EAC yaliyoletwa hapa na nimeona kazi moja ambayo ningelipenda mno kupeleka maombi yangu. Tatizo ni kuwa tangazo linasema maombi yapelekwe kwa The Secretary General, East African Community lakini hakuna jina la huyo The secretary general, jee kuna yeyete anaelijua jina kamili la mheshimiwa huyu?

  Mara nyingi nimeambiwa ni muhimu sana unapoandika barua za maobi u-address kwa jina la mhusika na niepuke kabisa mtindo wa kuandika to whom it may concern, au dear sir/madame na ndio maana natafuta jina la mhusika.

  ahsanteni
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Jina la nini wewe address ,Secretary General inatosha.
   
 3. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu anaitwa Amb. Dr. Richard Sezibera ila sina uhakika na huo mtazamo wako kwamba kinachohitajika ni kuadress kwa jina lake napata wasiwasi manake kwa kawaida mtu kama huyo unapo adress kwa jina lake una maanisha kuwa hiyo barua ni binafsi and not official kwamba imfikie yeye in person; sasa kazi zilizotangazwa si private issue ni mambo ya kiofisi na maana halisi ya kuadress via SG ni kwamba yeye ndo mtendaji mkuu hivyo hayo ni mambo ya kiitifaki; I suggest utumie adres kama ilivyoelekezwa
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mtu anatafuta kubebwa
   
 5. j

  jobseeker Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikubaliani nawe, Maofisi mengi duniani huchukia mno maombi yanayotumwa bila ya ku-address jina la mhusika. Kama huamini tembelea site za kazi mtandaoni na usome advice zao. Labda Tanzania hilo haliko lakini kwengine ni la muhimu sana. Kama alivyosema mtoa maoni utumiaji wa maneni to whom it may concern au dear sir/madame ni ishara ya barua yako kutupwa pakachani moja kwa moja, THAT IS FACT!!!!
   
 6. Buggy

  Buggy JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 239
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  acha ushamba wa kuomba kazi wewe! jina la nini unatafuta, nyie ndio mnaotoa rushwa kwenye kuomba kazi. fuata maelekezo kama yalivyotolewa kwenye nafasi za kazi!
   
 7. j

  jobseeker Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushamba? don't make me laugh! sina tabia ya kudharau watu lakini kama wa kuitwa mshamba hapa basi ni wewe na sio mleta maoni. Kuwa muungwana na usiwe mtu wa dharau kwani mshamba sio mtu? plus alichosema huyu ndugu ni standard ya sehemu nyingi duniani, unapeleka maombi kwa mhusika na baraua unaanza kwa kuadress jina la mhusika.
   
 8. S

  Sanga n. Member

  #8
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo ndo uhalisia.
  Ukiandika jina la muhusika inakuwa private.

  Assume umeandika jina ka muhusika na muhusika hayupo nafasi imekaimiwa; ina maana barua hiyo haitashughulikiwa mpaka arudi muhusika.

  Pia ikitokea uliyemwandika jina kapata uhamisho ghafla hiyo barua itashughulikiwa na nani?

  Tuache kupotosha umma. Ahsanteni.
   
 9. msani

  msani JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  achana na jina ngd yangu,je akibadilishwa ghafla au unadhani hiyo ni ofisi yake binafsi?hata km ni binafsi kuna kufa,je hapo na barua yako ya maombi haitakuwa na maana tena,kuwa makini
   
 10. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #10
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaribu kufuatilia vizuri kuhusu Elimun ya huyo mtu aliyekushauri kuwa kwenye official letter kuna sehemu ya kuweka jina la mtu badala ya cheo chake. Mimi elimu nyangu ni ndogo san ila nahisi huyo aliyekushauri anataka upate moja kati ya mambo yafuatayo.
  1. Kukosa na kutoitwa kwenye masalia kwa kigezo cha kutofuata maelekezo, kumbuka Intructions is part of examinations
  2. Kukosa nafasi ya kazi kwa kigezo cha ubinafsi, i.e wewe haupo tayari barua yako kushuhulikiwa na mwandamizi mwangine kwenye ofisi husika zaidi ya huyo uliyempendekeza.
  3. Kuonyesha kwamaba huna imani kabisa na watumishi wengine ndani ya ofisi husika.
  4. Mkono wa rushwa kwa huyo mhusika wako. etc, etc. etc

  Hivyo basi kwa ushauri wangu wa dhati wewe fuatilia kwa ukaribu elimu ya huyo mtu aliyekushauri kwani hakutakii mema, Na unapofuatilia usiogope cheo chake kwani yawezekana amepewa na Shangazi yake ila kichwa ni kitupu.

  Kila la kheri kwenye ufuatiliaji wako.
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Naona kuna wadau kadhaa wamemkosoa mtoa mada kuhusu kuandika jina la muhusika. In short, kwa namna fulani mtoa mada yupo sahii lakini katika mazingira ya kazi iliyotangazwa hatakuwa sahii. Ni kweli kabisa kwamba inakuwa much better kama utam-adress mtu kwa jina lake lakini hii inaleta sense kwa kazi ambazo hazijatangazwa. Maana ya hii kitu ni kwamba, barua husika ni lazima itamfikia mlengwa (Ofisini, kwavile adress ni ya ofisi) moja kwa moja. Lazima tukumbuke kwamba, application/CV nyingi ambazo tunazituma bila kazi kutangazwa huwa haziwafikii walengwa (decision makers). Hivyo basi, uki-adress barua/CV kwa jina la muhusika basi ni lazima itapitia mikononi mwake kwavile itadhaniwa ni personal letter. Muhusika akiichana, anakuta anakumbana na CV....na kwavile imefika moja kwa moja kweke, ni lazima atatafuta jina la mtumaji wa hiyo CV kwa imani kwamba lazima atakuwa anamfahamu. Sasa hapo kuna mawili....hata kama atagundua ameingizwa choo cha kike; layout ya CV inaweza kumvutia kupoteza angalau sekunde tano zaidi kuiangalia. Katika kuangalia huko, si ajabu akapendezewa na content iliyomo! Tusisahau kwamba, ofisi nyingi huwa zinakuwa na vacant positions ambazo hazijatangazwa rasmi, au bosi hajachukua maamuzi ya ku-declare upungufu wa mtu kwenye nafsi fulani!! So, this impressive CV inapomkuta decison maker, inaweza kumfanya akumbuke kwamba kuna nafasi inatakiwa kuzibwa! Lakini hata kama kwa wakati huo hamna nafasi, kuna uwezekano Bosi huyu akaipeleka CV husika kwa HR. Katika hali ya ubinadamu, HR huyu anaweza kuzani kwamba kv CV imetoka kwa bosi, basi inatakiwa kupewa special attention! Hivyo basi, kwa job seekers, hiyo ni one of the job search technique....uki-adress moja kwa moja kwa say "Head of Depart" au "General Manager" na mambo mengine kama hayo wakati hamna kazi iliyotangazwa basi kuna uwezekano mkubwa wa CV yako kuishia kwenye dustbin wakati tayari bosi mkuu ameshafikiria suala la kuongeza mtu mwenye sifa kama za huyo ambae CV yake ipo kwenye dust bin!
   
 12. Myelife

  Myelife Senior Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Angalieni mambo haya,,, ktk interview utaulizwa ,,, je unamfahamu mtu yeyote ktk office hii, je utajibu nini, km hapana utaambiwa mbona barua yako imemtaja mh kwa jina, then unaweza kupoteza chansi km utasema simjui utakuwa umedanganya kwani barua yako uliadress kwake,, pili office ni jopo la watu wanaobeba majukumu yenye vision moja! Mfano president office haina maana raisi yupo ktk hiyo office, sasa km barua zinatakiwa kwenda kwa PS office ya raisi ni ruksa kuadress barua kwa raisi maana ndo mwenye office, au PS wakati huwa ma PS wanaweza kuwa 3 pamoja na kaimu, mwisho kutofuata maelekezo ni dalili ya kutupwa nje ktk mtihani, mwisho nikushauri appl letter yako usimtaje mtu, ila ktk interview kama unajua interviewer wako basi ni vema umuadress kwa jina to make more passionate, lkn kumtaja ktk barua ni hatari kwa nafasi yako, kumbuka ktk oral interv ,, interviewer anazo docs zako zote mezani.
   
Loading...