Suala la wastaafu kutolipwa kiinua mgongo(Pensheni) kwa wakati

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Katika biashara yangu ya ujasiriamali nimetokea kuwakopesha sana walimu na hivi karibuni nilikopesha walimu wanaokaribia kustaafu na wamekuwa wanastaafu lkn hawalipi rejesho.

Sasa katika hawa niliowakopesha nimewauliza mbona Rais aliwahi kutoa maelekezo penshni zisichelewe inakuwaje?

Majibu yao sasa - Rais ndiyo kasababisha hatulipwi na tena wanadai hali ilivyo waliostaafu kuanzia Mwezi wa saba Mwaka jana hawatalipwa kwa sababu fedha zinatumika kwenye uchaguzi na Serikali haina fedha.

Sasa hayo sijui ni ya ukweli?
 
Jiwebni jiwe tu, hata nchi inakopelekwa hakuna anayejua. Tuseme ukweli nchi kama Tanzania tunaongoza na..... afu tufanikiwe hahahahaha
 
Tueleze jina lako na unapatikana wapi tukushitaki kwa ile kesi isiyo na dhamana
Unakuta mstaafu kaacha ATM card na namba za siri kwa mkopeshaji mzigo ukitoka jamaa anachana tu ATM card anatoa fedha mstaafu anaambulia kiduchu huu ni utakatishaji.
 
Niseme tu mambo kama haya ya kuwazulumu wastaafu na kutowajali waliotumikia kwa uamnifu mkuu Leo ni mafukara hata uwezo wa kununua ndala hawana japo walikuwa mabosi na nafasi za kuwawezesha kukwapua makazini yamewavunja sana moyo wazee wetu hii ndio imepelekea vijana wa sasa hizi kuwa ni wakwapuaji wakubwa wa kutupwa kwa msaada wa ushauri wa wazee wetu waliostaafu na kutelekezwa kwamba zubaa shangaa yatakukuta kama sie hii serikali haina wema.

Ni maneno yakatishayo na kuumiza lkn ndo ukweli wenyewe,laiti kama tungewajali wastaafu waishi vyema kwa utumishi wa uaminifu waliotumika ingesaidia sana hasa vizazi vya sasa kuongeza tija na uaminifu kazini.

Sio ya kizazi cha sasa MTU anakwapua parefu kuliko hata pension yake akijua akibambwa atakaa ndani tena vizuri kwa uhujumu uchumi hata kama ni miaka 10 akitoka yuko vizuri anasimamia miradi yake tu
 
Unakuta mstaafu kaacha ATM card na namba za siri kwa mkopeshaji mzigo ukitoka jamaa anachana tu ATM card anatoa fedha mstaafu anaambulia kiduchu huu ni utakatishaji.
Hili wanalo sana waalimu vijijini aisee hadi huruma.
 
Hivi hao wastaafu mnaowasema wanakopeshwa kwa lazma au wanaenda wenyewe? Kwanza hao ni wasomi mfano walimu kwanini wasitumie akil zao kujua kwamba hizo hela znariba kubwa? Vile vile mabenki mbona yanatoa mikopo ya wastaafu kwa riba ndogo kabisa kwann wasiende huko wahangaike na hela za moto? Hapa kuna tatizo kwenye wasomi wetu pili kuna tatizi kubwa kwenye serikali coz kwa nn mtu aliyetumikia taifa kwa miaka pengne zaidi ya 30 na baada ya kustaafu ashindwe kununua hata ndala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipato duni cha walimu fursa kwa wakopeshaji, riba wanagonga mpaka 50%
 
Maana wakopeshaji mnasababisha wastaafu kufariki mnapuna pesa zao nyingi kwa riba nyongaji
Ukimaliza kumlaumu yeye sasa hamia kwa Wanaokopa nao uwalaumu na uwapatie ushauri mbadala nini cha kufanya.
 
Ila muwe na subira kwa sababu kuna juhudi zinaonekana tayari zinafanyika, soon kila kitu kitakuwa sawa.

Wale waliotajwa na msiba kumkwamisha Mkuu wameshaanza kushughulikiwa.

Wameshaitwa kwenye kamati ya Mzee Filipu mambo yatanyooka sasa mpaka mtashangaa...sio mikopo ya Wanafunzi, pensheni, ajira zitakuwa nje nje.

Kwa kifupi tunasema yajayo yanafurahisha.
 
Ila muwe na subira kwa sababu kuna juhudi zinaonekana tayari zinafanyika, soon kila kitu kitakuwa sawa.

Wale waliotajwa na msiba kumkwamisha Mkuu wameshaanza kushughulikiwa.

Wameshaitwa kwenye kamati ya Mzee Filipu mambo yatanyooka mpaka mtashangaa...sio mikopo ya Wanafunzi, pensheni, ajira zitakuwa nje nje.

Kwa kifupi tunasema yajayo yanafurahisha.
Upo huko nini mkuu - kwa maana unatuletea stori za jikoni kabisa!
 
Back
Top Bottom