Suala la wasiwasi Zanzibar: Waziri Kitwanga kafanya maigizo au ndio uwezo wake?

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,606
4,262
Jana nilipata kutizama taarifa ya habari kupitia kituo cha television cha ITV. Pamoja na mambo mengine ilikuwepo habari iliyohusu ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndai Mheshimiwa Charles Kitwanga visiwani Zanzibar ambapo alikwenda kujionea hali ya mambo kuelekea uchaguzi unaotarajia kufanyika tarehe 20 March.

Kutokana na malalamiko ya hapa na pale juu ya askari polisi na vikosi vingine vilivyopo Pemba kunyanyasa watu kwa kuwapiga pamoja na mambo mengine, mheshimiwa waziri 'alijiridhisha' kwamba hali hiyo haipo kabisa na kila kitu ni shwari. Sababu ya kujiridhisha huko ni kwa kuwa katika ziara yake hakuona hata tukio moja la polisi kumpiga mwananchi yeyote. Suala la kujiuliza ni kwamba, hivi ni kweli alitegemea kabisa polisi wafanye vitendo hivyo akiwepo kisiwani humo, au alisema hivyo tu kisiasa kama namna ya maigizo? Ziara yake haikuwa incognito, alikwenda rasmi na kila alipokwenda aliambatana na msafara wa kiwaziri, alitegemea hayo yangeweza kufanyika mbele yake? Na hata kama kuna ambaye amefanyiwa kitendo hicho dakika chache kabla ya kufika anadhani kuna ambaye angejitokeza hadharani? Nilijikuta nashangaa baada ya kulithibitishia taifa kuwa matendo hayo hayapo kwa sababu tu 'yeye hakuyashukudia kwa macho yake'

Baada ya hapo wakaelekea kwenye msitu wa Ngezi ambako inasemekana kuna watu wamekimbilia na wamejificha huko kwa kuhofia usalama wao katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Kwa maneno yake alikwenda huko ili kukutana 'na watu hao' ili apate 'kuwahakikishia usalama wao na kuwashawishi warudi makazini kwao wapige kura kwa amani na waendelee na maisha yao kama kawaida'. Kama kawaida alikwenda na msafara mkubwa uliohusisha askari polisi pamoja na viongozi wengine. na hapa pia akatoa kauli kuwa uvumi huo ni uongo, na kwamba hakuna watu katika msitu huo kwa sababu hajawaona watu hao katika msitu huo. Suala la kujiuliza ni je, alitegemea watakuja kumpokea kwa mabango wakati wameyakimbia makazi yao? (assuming kweli wapo watu hao). Na ziara yao kwenye msitu huo ilikuwa thorough kiasi gani hadi kujiridhisha kwamba hapakuwa na watu?

Kifupi, binafsi sipo Zanzibar kwa hiyo sina hakika juu ya hali ya amani na usalama huko ukiachilia yale niyapatayo kupitia vyombo vya habari. Kwa hiyo sina hakika kama kweli askari wanapiga watu au hawapigi. na sina hakika kama wapo watu wanaoishi msituni au kama hawapo. Lakini kauli za waziri alizotoa kwa kutumia ushahidi hafifu namna ile zimenifanya nijiulize kama alikuwa anafanya maigizo ya kisiasa kama kawaida au kama ndio uwezo wake wa kufikiri na kupambanua mambo ulipofikia?
 
Pamoja na ukweli kuwa kuna juhudi kubwa zinafanywa na serikali kubana matumizi ya fedha za umma, upande wa siasa bado matumizi yanatesa. Ziara ya wazir huyo ni maigizo ya kisiasa ktk ubora wake. Watu waliojificha msituni(kama wapo na palikuwa na nia ya kuthibitisha) unawatafuta kwa gari? Tatizo la zanzibar linafunikwa, tena kwa nguo. Tuuonao ni moshi, nguo zitawaka na zimamoto watakuta majivu.
 
Pamoja na ukweli kuwa kuna juhudi kubwa zinafanywa na serikali kubana matumizi ya fedha za umma, upande wa siasa bado matumizi yanatesa. Ziara ya wazir huyo ni maigizo ya kisiasa ktk ubora wake. Watu waliojificha msituni(kama wapo na palikuwa na nia ya kuthibitisha) unawatafuta kwa gari? Tatizo la zanzibar linafunikwa, tena kwa nguo. Tuuonao ni moshi, nguo zitawaka na zimamoto watakuta majivu.
Wamekwenda wakasimama somewhere huko msituni halafu akasema hakuna watu humu. Yaani alitegemea watakuja kumlaki kwamba mkombozi kaja? Haikumwingia akilini kwamba watu hao waliokimbia makazi yao watakaposikia viongozi wanakuja watakimbilia ndani ya msitu zaidi?
 
Back
Top Bottom