Suala la wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo au la, ni suala la 'kisera'.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaaandika Markus Mpangala

Suala la wanafunzi wanaopata ujauzito kuendelea na masomo au la, ni suala la 'kisera'. Ni sera ndio zinazungumza hayo masuala na sio kauli za jukwaani.

Andaa sera, peleka mjadala bungeni, wananchi wajadili, sheria ziwekwe. Pamoja na mambo mengi sana, yanayohitaji 'sera' na/au kuwekewa sheria. Ukiongoza nchi kwa kauli za jukwaani, unaenda kufeli!

Moja kati ya kauli zisizo na msingi zinazotumika kipindi hiki ni kauli ya "katika utawala wangu"! Tunarudi katika enzi za ujima wakati dola zikiongozwa kwa katiba isiyoandikwa! Maneno ya mtu mmoja kwa watu milioni 50! Teh!
 
Sera zilizopo anaepata Mimba haendeleinna Masomo ya Shule ya Msingi na Sekondari!

Inawezekana hujawahi kusoma hizo sera hata kwny Barua ya kuchaguliwa Shule ya Secondari 'Join Instructions' Hilo suala lipo na hata kwny Sera zetu lipo!

Jitihada zilikuwa kubadilisha hiyo sera ili iruhusiwe Wamama Watoto na Wasichana wasome darasa Moja nashukuru Rais wetu kakataa hilo
 
Kwani hilo swala ni jipya?Au ni upuuzi wa NGOs tu.

Hizi NGOs ndio zinatuwekea uchafu wa matangazo kwenye TV...eti watoto wanafeli kwa kukosa pedi...dada zetu na mama zetu waliofaulu bila pedi walifanyaje?
 
Back
Top Bottom