Suala la wamachinga naona serikali inakosea, naiomba inisikilize

Hapa ndipo penye wapiga Kura na utulivu wa nchi unapatikana ,ukilikwaza hili kundi kubwa la vijana wenye nguvu na wenye mahitaji muhimu ni kujipalia kaa la moto,vijana hawa ndio huangusha serikali karibu zote duniani.
Wengi wao ni wasomi ambao wamekosa ajira,sasa wameamua kupoza machungu kupitia umachinga.
Serikali ilamua kuhamia Dodoma ili Jiji la Dar-es-saalam liwe la kibiashara,nashangaa viongozi kuingangania Ikulu ya mkoloni badala ya ile tumejenga kwa nguvu zetu ,hasa kiranja mkuu.

Wamachinga wataigharimu serikali ya CCM muda ujao kwa kuwasikiliza ma-tycoons.

Serikali isiwandoe kwa mkupuo, iwaondoe kwa mafungu kama inataka salama pia ihakikishe inapowapeleka panafaa na mzunguko wa biashara upo, rejeeni yaliyotokea Zambia pamoja na Rais Lungu kuwa na vikosi vyote, why not TANZANIA.

Wakunielewa kanielewa, wale wakuziba pamba maskioni endelea
Ccm haiitaji kura yako kubaki madarakani, unajidanganya bure.

Naunga mkono mia kwa mia wamachinga watupishe, wengine tumeacha kwenda kariakoo kwa sababu yao hakuna pa kupita.
 
Nadhani tusimamie sheria inasemaje. Tukisema tufurahishe nafsi then hakuna sheria itakayofanya kazi.


Sheria ya halimashauri ipo wazi kuwa yale mazingira sio sahihi kwaajiri ya shughuli za machinga. Kinachotokea pale ni uvunjifu ule ule wa sheria kama ule wanaofanya mafisadi serikalini.

Sasa nashangaa watu kama wewe mleta mada unakuja na topic kama hizi ambazo zinatetea ukiukwaji wa sheria.

So sheria wakivunja viongozi kelele kibao ila raia ni sawa kuvunja sio?!
Issue sio kuruhusu kuvunja sheria bali ni namna ya kuhandle hii issue ,serikali yenyewe imelea uvunjaji wa sheria mpaka imekua mazoea,sasa kinachosema ni umakini kwenye kulitatua
 
Naomba nikusahihishe, serikali ya chama cha mapinduzi huwa haikosei na haijawahi kukosea..hii mijitu ya CDM itoke imefunga njia za wananchi.
 
CCM haitegemei Kura kushinda, inabebwa na tume ya uchaguzi ,police na UVCCM waliojivika usalama wa taifa
 
Back
Top Bottom