Suala la Wamachiga: Hayati Magufuli asitumike kama gold standard

Freemanson_tz

New Member
Oct 25, 2021
2
1
Habari JF

Wiki kadhaa zilizopita Serikali ilianzisha kampeni ya kuhakikisha maeneo yetu yanarejea katika hali nzuri kwa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara maarufu kama wamachinga wanawekewa uratatibu mzuri wa kufanya biashara zao huku mazingira yakibaki safi na salama kwa ajili ya matumizi na watu wengine.

Kabla ya kufikiria dhana ya kuwapanga wamachinga ni vizuri kufahamu sifa za machinga; Machinga hasa ni mfanyabiashara wa aina gani ?

1. Mfanyabiashara ambaye hataki kuwa rasmi ili kukwepa taratibu za kodi.
2. Mfanyabiashara ambaye anataka kutumia eneo lolote walipo watu wengi kuuza bidhaa huku akiweza kuhamahama kutokana na kuhama kwa wanunuzi

Hivyo kutokana na sifa hizo, Wapo viongozi waliowaagiza machinga kufanya biashara popote bila kubughudhiwa na hivyo kupelekea kukomaa na kukua kwa kundi hili katika maeneo ya mjini.
 
Wa bongo kwa kujitoa ufahamu utawaweza?

Na sema hivi waindolewe tu hakuna namna

Afu acheni kujifanya MNA mapenz sana na marehemu
 
Vijina wetu wana nia njema, hawataki kukaa bila kufanya kazi. Ndiyo maana wanaamua kujishughulisha na umachinga. Hili ni jambo jema ambalo Serikali ilitumie kama furusa vijana hawa iwatumie kuzalisha mali badala ya kuchuuza mali kutoka viwanda vya nje. Serikali iweke mikakati inayotekelezeka kwa haraka sana ya kuwatumia vijana hawa kuzalisha mali tutakazotumia sisi na nyingine kuuza nje tupate fedha za kigeni.

Serikali ijikite kuwawezesha vijana kuzalisha mali tena kwa utaratibu usiowakuwafanya ni watu wabaya badala ya kuwaanda kuwa wachuuzi wa mali za viwanda vya nje. Nidhani kwa kufanya hivyo, tutakuwa tunaanda kizazi bora sana cha kizalendo kwa kupenda na kulinda nchi yetu.
 
Back
Top Bottom