tibwilitibwili
Senior Member
- Sep 12, 2006
- 181
- 10
SERIKALI imekiri kupokea barua ya Umoja wa Waislamu wa Arusha (AMU) iliyoandikwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, na kuahidi kuwa italijadili kwa kina suala hilo.
Umoja huo juzi ulimwandikia barua Masha ukimuomba achukue hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa polisi waliowakamata wanachama wanane wa umoja huo wakati wa ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani, kwa madai ya kutaka kuvuruga ziara hiyo.
Akizungumza na HabariLeo Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamisi Kagasheki, alikiri wizara yake kuipokea barua hiyo, lakini haikuweza kuijadili kutokana na kutingwa na kazi. Barua hii ni kweli imefika ofisini leo (jana) na nimeitazama kwa haraka tu, ila Waziri hakuwapo ndiyo karudi, mimi mwenyewe nilikuwa nashughulikia mkutano wa Kamati ya Taifa ya Huduma za Jamii, ila lazima nikirudi niipitie tuweze kuijadili na viongozi husika, alisema Kagasheki.
Alisema jambo hilo si la kuchukulia juu juu, kwa kuwa kila upande yaani wananchi na polisi una taarifa zake, hivyo ni heri kwanza lijadiliwe ndipo ufumbuzi wake upatikane. Hili jambo si la kurukia, hawa ni raia watakuwa na story yao na sisi Serikali tuna yetu na isitoshe huwezi kumtuhumu mtu mpaka iwe approved ndio maana ninasema tutalitazama, alisema.
Watu hao wanane walikamatwa Februari 17, mchana nyumbani kwa Katibu wa chama hicho, Mohamed Akida, wakituhumiwa kutaka kuvuruga ziara ya Bush na hivyo katika barua ya Umoja huo, wameomba polisi waliohusika wachukuliwe hatua, ikiwa ni pamoja na kukiri kosa.
Katika barua hiyo, Mwenyekiti anaeleza kuwa maofisa wa Polisi wakiongozwa na Ofisa wa ngazi ya wilaya mwenye cheo cha juu walifika nyumbani kwa Katibu wao na kuwataka watu waliokuwepo hapo waende Kituo Kikuu cha Polisi kujieleza kwa kufanya kikao haramu.
Tulimweleza Ofisa huyo kuwa kikao kile kilikuwa mwendelezo wa kikao cha Februari 13, ambacho kiliahirishwa kutokana na idadi ya wajumbe wanaohitajika kutofikia na tulimwonyesha ajenda zake lakini hakutaka kutusikiliza, ilisomeka sehemu ya barua hiyo. Mwenyekiti huyo alisema walipofikishwa kituoni waliandika maelezo na baadaye waliswekwa rumande hadi Jumatatu ya Februari 18 saa 12.30 za jioni, walipoachiwa wakati ziara ya Rais huyo wa Marekani ikiwa imemalizika.
Tukiwa kituoni tuliomba tupewe nafasi ya kuonana na viongozi wa Polisi mkoani hapa, tukakataliwa na kuelezwa kuwa sisi ni magaidi wa mtandao wa kundi hatari la Al-qaeda, ilisema barua hiyo.
Sisi hapa tunasema tumeonewa. Majina yetu yamepakwa matope. Kila mahali tunapopita watu wanatuona kama washari na wengine wanatukejeli kama magaidi wa kundi la Al-qaeda, hasa baada ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai kukiri kwenye vyombo habari kuwa kuna watu wamekamatwa Arusha na Dar es Salaam kwa ugaidi, iliendelea kusomeka barua hiyo.
Chama hicho kinalalamika kuwa kitendo hicho kimewadhalilisha sana kwa kuwa kiroho magaidi wanatambulika kama watu wanaofanya vitendo vya kishetani ambavyo vinawatisha watu ...na sisi tunatumia fursa hii Jeshi la Polisi lisafishe majina yetu.
Chama hicho cha Umoja wa Waislamu wa Arusha kilianzishwa miaka miwili iliyopita na kupatiwa hati ya usajili namba 14,590 na madhumuni yake ni kuwaunganisha waumini wa dini hiyo katika masuala mbalimbali hasa kiroho na kijamii.
Source: HabariLeo