Suala la 'viboko' kwanini waathirika wakuu wa kadhia hii ni walimu wa shule za msingi?

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
236
imeshakuwa kama desturi kila mwaka kuripotiwa tukio la mwalimu kuchapwa 'viboko' ama kunaswa 'vibao' na wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo maofisa elimu, walimu wakuu, watendaji mbali mbali wa serikali na wazazi.

Aidha kadhia hii imeshamiri sana kwa shule za msingi huku wahanga wakubwa wakiwa ni walimu wa ngazi ya cheti almaarufu kama grade A.

Na hapa chini ni kielelezo cha baadhi ya matukio ya walimu kucharazwa viboko ambayo yamewahi kuripotiwa nchini;

1. Mwaka 2017, mwalimu mkuu wa shule ya msingi migango wilayani biharamulo alimchapa viboko mwalimu mwenzake. Katika tukio hilo la aina yake mwalimu mkuu huyo alimchapa viboko mwalimu mwenzake mbele ya wanafunzi kwa madai kwamba aliiba sahani tano pamoja na nusu kilo ya sukari ambavyo vilikuwa vimetolewa kwaajili ya mahafari ya darasa la saba.
Katika kutekeleza adhabu hiyo, mwalimu mkuu alimfunga mwalimu mwenzake kwenye mti ulioko mbele ya shule hiyo na kuanza kumchara bakora saa nane za mchana huku wanafunzi wakiwa nje wanashuhudia.

2. Mwaka 2016, mwalimu mmoja wa shule ya msingi ikombolinga alizabwa makofi na ofisa elimu wa wilaya(msingi) mbele ya walimu wenzake kwa sababu ya kuchelewa katika semina ya mafunzo ya KKK licha ya mwalimu huyo kujitetea kuwa alitokea mbali na hakuwa amelipwa pesa ya nauli.

3. Mwaka huo huo wa 2016, afisa elimu(msingi) wa wilaya ya sumbawanga alimshambulia kwa makofi mwalimu mmoja wa shule ya msingi kianda akiwa darasani mbele ya wanafunzi. Mbali na kumuadhibu mwalimu huyo pia ofisa elimu aliwaamuru walimu wote shuleni hapo kuokota mbigili 'miba' iliyokuwa imetapakaa shuleni hapo kwa madai kuwa ni uchafu.

4. Mwaka 2015, walimu watatu wa jinsia ya kike wa shule ya msingi mwabagole iliyopo wilayani kwimba mkoa wa mwanza walivamiwa, kushambuliwa na kupigwa viboko na wazazi baada ya watoto wao kupewa adhabu ya viboko kwa kuvunja sheria za shule baada ya wanafunzi hao kushangilia wenzao waliokuwa wakipigana wakati wa mapumziko.

5. Mwaka 2020, Ofisa elimu wa kata ya useya wilaya ya mlele alimcharaza mwalimu mmoja wa shule ya msingi useya. Katika tukio hilo, ofisa elimu alimfuata mwalimu huyo nyumbani kwake majira ya saa saba mchana na kumcharaza viboko zaidi ya vinne matakoni kwa madai kwamba hakufika shuleni.

6. Mwaka 2009, mkuu wa wilaya ya bukoba aliwaamuru askari wa jeshi la polisi kuwacharaza 'viboko' jumla ya walimu 32 wa shule tofauti za msingi wilayani humo kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba.

7. Mwaka 2014, mzazi ambaye ni baba wa mwanafunzi alishambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wawili wa shule ya msingi Nzogimlole iliyopo wilayani nzega mkoani Tabora kupinga kitendo cha mwalimu mmoja shuleni hapo kumrudisha mwanawe kushona sare(kaptura) ya shule iliyokuwa imechanika vibaya sana kiasi cha sehemu za siri kuonekana.

Mwaka huu sijui ni zamu ya mwalimu nani kuchapwa mboko...Hahaha!! Nachomekea tu ndungu zangu tuendelee na mjadala

Ikumbukwe kuwa kutumia kiboko au makofi kumuadhibu mwalimu ni kinyume kabisa na taratibu za kiutumishi pia ni kuvunja sheria za nchi kwa kujichukulia sheria mkononi kwani adhabu zote zinapaswa kutolewa kwa kufuata taratibu na kwa kuzingatia misingi ya kisheria.

Kadhalika, matumizi ya kiboko au makofi si tu kinadhalilisha bali pia kinavunja heshima na kushusha morali ya walimu(wahanga) kwani wawapo madarasani kutekeleza wajibu wao huishia kuchekwa na kudharauliwa na wanafunzi wao.

Sasa basi, Kufuatia vitendo hivyo kujirudia mara kwa mara nimeona leo nililete hapa jamvini tulijadili kwa mapana tujue ni sababu zipi hasa hupelekea walimu hao kuadhibiwa kwa viboko, mitama na makofi.

Kwa kuanzia ningeomba kujua ni kwanini katika kadhia hii ya viboko wahanga wakubwa ni walimu wa shule za msingi tofauti na ilivyo kwa walimu wa shule za sekondari?

Je walimu hawa hawana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu haki zao za kiutumishi?

Je walimu hawa wanakiuka sana taratibu na kanuni za kiutumishi hivyo inawalazimu maofisa elimu, walimu wakuu na wadau wengine wa elimu kutumia adhabu ya viboko na makofi kama huruma ya kuwanusuru kufukuzwa ama kuachishwa kazi?
 
Walimu ndio kundi kubwa zaidi la waajiriwa wa serikali halafu ndio wamekubali kutumiwa na CCM miaka yote, sasa mtu ukishamzoea ukaujua udhaifu wake kumchapa viboko ni jambo dogo sana, anakuwa tu kama mtoto wako coz siku zote anaishi kwa kufuata maelekezo yako.
 
4. Mwaka 2015, walimu watatu wa jinsia ya kike wa shule ya msingi mwabagole walivamiwa, kushambuliwa na kupigwa viboko na wazazi baada ya watoto wao kupewa adhabu ya viboko kwa kuvunja sheria za shule baada ya wanafunzi hao kushangilia wenzao waliokuwa wakipigana wakati wa mapumziko.

5. Mwaka 2020, Ofisa elimu wa kata ya useya wilaya ya mlele alimcharaza mwalimu mmoja wa shule ya msingi useya. Katika tukio hilo, ofisa elimu alimfuata mwalimu huyo nyumbani kwake majira ya saa saba mchana na kumcharaza viboko zaidi ya vinne matakoni kwa madai kwamba hakufika shuleni.

6. Mwaka 2009, mkuu wa wilaya ya bukoba aliwaamuru askari wa jeshi la polisi kuwacharaza 'viboko' jumla ya walimu 32 wa shule tofauti za msingi wilayani humo kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba.

7. Mwaka 2014, mzazi ambaye ni baba wa mwanafunzi alishambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wawili wa shule ya msingi Nzogimlole iliyopo wilayani nzega mkoani Tabora kupinga kitendo cha mwalimu mmoja shuleni hapo kumrudisha mwanawe kushona sare(kaptura) ya shule iliyokuwa imechanika vibaya sana kiasi cha sehemu za siri kuonekana.

Mwaka huu sijui ni zamu ya mwalimu nani kuchapwa mboko...Hahaha!! Nachomekea tu ndungu zangu tuendelee na mjadala

Ikumbukwe kuwa kutumia kiboko au makofi kumuadhibu mwalimu ni kinyume kabisa na taratibu za kiutumishi pia ni kuvunja sheria za nchi kwa kujichukulia sheria mkononi kwani adhabu zote zinapaswa kutolewa kwa kufuata taratibu na kwa kuzingatia misingi ya kisheria.

Kadhalika, matumizi ya kiboko au makofi si tu kinadhalilisha bali pia kinavunja heshima na kushusha morali ya walimu(wahanga) kwani wawapo madarasani kutekeleza wajibu wao huishia kuchekwa na kudharauliwa na wanafunzi wao.

Sasa basi, Kufuatia vitendo hivyo kujirudia mara kwa mara nimeona leo nililete hapa jamvini tulijadili kwa mapana tujue ni sababu zipi hasa hupelekea walimu hao kuadhibiwa kwa viboko, mitama na makofi.

Kwa kuanzia ningeomba kujua ni kwanini katika kadhia hii ya viboko wahanga wakubwa ni walimu wa shule za msingi tofauti na ilivyo kwa walimu wa shule za sekondari?

Je walimu hawa hawana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu haki zao za kiutumishi?

Je walimu hawa wanakiuka sana taratibu na kanuni za kiutumishi hivyo inawalazimu maofisa elimu, walimu wakuu na wadau wengine wa elimu kutumia adhabu ya viboko na makofi kama huruma ya kuwanusuru kufukuzwa ama kuachishwa kazi?
Walimu wanapaswa kutambua kuwa si chama chao CCW ama vyama vya wafanyakazi vinaweza kulinda hadhi na utu wao. Ni lazima nao wawe na "professional body" ambayo itakuwa ndiyo msingi mkuu wa hadhi na maadili yao ya kazi

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Walimu ndio kundi kubwa zaidi la waajiriwa wa serikali halafu ndio wamekubali kutumiwa na CCM miaka yote, sasa mtu ukishamzoea ukaujua udhaifu wake kumchapa viboko ni jambo dogo sana, anakuwa tu kama mtoto wako coz siku zote anaishi kwa kufuata maelekezo yako.
Da,yaani wewe.
 
imeshakuwa kama desturi kila mwaka kuripotiwa tukio la mwalimu kuchapwa 'viboko' ama kunaswa 'vibao' na wadau mbali mbali wa elimu wakiwemo maofisa elimu, walimu wakuu, watendaji mbali mbali wa serikali na wazazi.

Aidha kadhia hii imeshamiri sana kwa shule za msingi huku wahanga wakubwa wakiwa ni walimu wa ngazi ya cheti almaarufu kama grade A.

Na hapa chini ni kielelezo cha baadhi ya matukio ya walimu kucharazwa viboko ambayo yamewahi kuripotiwa nchini;

1. Mwaka 2017, mwalimu mkuu wa shule ya msingi migango wilayani biharamulo alimchapa viboko mwalimu mwenzake. Katika tukio hilo la aina yake mwalimu mkuu huyo alimchapa viboko mwalimu mwenzake mbele ya wanafunzi kwa madai kwamba aliiba sahani tano pamoja na nusu kilo ya sukari ambavyo vilikuwa vimetolewa kwaajili ya mahafari ya darasa la saba.
Katika kutekeleza adhabu hiyo, mwalimu mkuu alimfunga mwalimu mwenzake kwenye mti ulioko mbele ya shule hiyo na kuanza kumchara bakora saa nane za mchana huku wanafunzi wakiwa nje wanashuhudia.

2. Mwaka 2016, mwalimu mmoja wa shule ya msingi ikombolinga alizabwa makofi na ofisa elimu wa wilaya(msingi) mbele ya walimu wenzake kwa sababu ya kuchelewa katika semina ya mafunzo ya KKK licha ya mwalimu huyo kujitetea kuwa alitokea mbali na hakuwa amelipwa pesa ya nauli.

3. Mwaka huo huo wa 2016, afisa elimu(msingi) wa wilaya ya sumbawanga alimshambulia kwa makofi mwalimu mmoja wa shule ya msingi kianda akiwa darasani mbele ya wanafunzi. Mbali na kumuadhibu mwalimu huyo pia ofisa elimu aliwaamuru walimu wote shuleni hapo kuokota mbigili 'miba' iliyokuwa imetapakaa shuleni hapo kwa madai kuwa ni uchafu.

4. Mwaka 2015, walimu watatu wa jinsia ya kike wa shule ya msingi mwabagole iliyopo wilayani kwimba mkoa wa mwanza walivamiwa, kushambuliwa na kupigwa viboko na wazazi baada ya watoto wao kupewa adhabu ya viboko kwa kuvunja sheria za shule baada ya wanafunzi hao kushangilia wenzao waliokuwa wakipigana wakati wa mapumziko.

5. Mwaka 2020, Ofisa elimu wa kata ya useya wilaya ya mlele alimcharaza mwalimu mmoja wa shule ya msingi useya. Katika tukio hilo, ofisa elimu alimfuata mwalimu huyo nyumbani kwake majira ya saa saba mchana na kumcharaza viboko zaidi ya vinne matakoni kwa madai kwamba hakufika shuleni.

6. Mwaka 2009, mkuu wa wilaya ya bukoba aliwaamuru askari wa jeshi la polisi kuwacharaza 'viboko' jumla ya walimu 32 wa shule tofauti za msingi wilayani humo kutokana na wilaya hiyo kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba.

7. Mwaka 2014, mzazi ambaye ni baba wa mwanafunzi alishambulia kwa kuwacharaza viboko walimu wawili wa shule ya msingi Nzogimlole iliyopo wilayani nzega mkoani Tabora kupinga kitendo cha mwalimu mmoja shuleni hapo kumrudisha mwanawe kushona sare(kaptura) ya shule iliyokuwa imechanika vibaya sana kiasi cha sehemu za siri kuonekana.

Mwaka huu sijui ni zamu ya mwalimu nani kuchapwa mboko...Hahaha!! Nachomekea tu ndungu zangu tuendelee na mjadala

Ikumbukwe kuwa kutumia kiboko au makofi kumuadhibu mwalimu ni kinyume kabisa na taratibu za kiutumishi pia ni kuvunja sheria za nchi kwa kujichukulia sheria mkononi kwani adhabu zote zinapaswa kutolewa kwa kufuata taratibu na kwa kuzingatia misingi ya kisheria.

Kadhalika, matumizi ya kiboko au makofi si tu kinadhalilisha bali pia kinavunja heshima na kushusha morali ya walimu(wahanga) kwani wawapo madarasani kutekeleza wajibu wao huishia kuchekwa na kudharauliwa na wanafunzi wao.

Sasa basi, Kufuatia vitendo hivyo kujirudia mara kwa mara nimeona leo nililete hapa jamvini tulijadili kwa mapana tujue ni sababu zipi hasa hupelekea walimu hao kuadhibiwa kwa viboko, mitama na makofi.

Kwa kuanzia ningeomba kujua ni kwanini katika kadhia hii ya viboko wahanga wakubwa ni walimu wa shule za msingi tofauti na ilivyo kwa walimu wa shule za sekondari?

Je walimu hawa hawana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu haki zao za kiutumishi?

Je walimu hawa wanakiuka sana taratibu na kanuni za kiutumishi hivyo inawalazimu maofisa elimu, walimu wakuu na wadau wengine wa elimu kutumia adhabu ya viboko na makofi kama huruma ya kuwanusuru kufukuzwa ama kuachishwa kazi?
Watumishi wa umma hasa walimu ni kikundi cha watu wasioelewa. Hawa ni watu mfu wasiojua hakizao
 
Acha wachapwe wafidie posho za kusimamia "uchafuzi" kila baada ya miaka mi5 na matendo wanayofanyaga ...
kuficha karatasi za "kula" chupini!!
 
Back
Top Bottom