Suala la Ulinzi Shirikishi ni la Kisheria?

Pilim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
228
150
Kuna jambo hili la ulinzi shirikishi ambalo naona linaendelea kushika kasi katika jamii yetu. Je, lipo kisheria? Kazi ya wizara ya ulinzi ni ipi kama wananchi tunatakiwa kujilinda wenyewe? Kama wanahitaji nguvu kazi zaidi kwanini wasiajiri badala ya kurudisha mzigo kwa wananchi?

Mi nachukizwa sana kudaiwa pesa ya ulinzi huu kila mwezi! Kwa nini wananchi ndo tulipie ulinzi huu wakati tunalipa kodi? Wizara hii ya ulinzi haipewi bajeti yake?

Mwenye uelewa zaidi anisaidie!
 
Kwa mfano; Serikali ijenge hospitali kwenu kijijini, iajiri daktari mmoja, halafu itoe maelekezo ya wanakijiji kutafuta madaktari wengine wa5 na wawewanawalipa wenyewe, nalo hilo litakuwalipo kisheria!!!
 
Mi nafikiri Tanzania tunashindwa kutumia rasirimali watu vizuri. Nilishawahi kutoa pendekezo kwenye bandiko langu nililoliweka baada ya kutoka Rwanda.Vikosi vyote vya ulinzi na usalama vinashirikiana vizuri kulinda raia na mali zao kwa kipindi hiki cha amani,sasa huku unakuta wanajeshi wetu hatumiki hivyo zaidi ya kulinda kambi zao na mipakani.Ninaumia sana huku nilipo kuna kambi ya jeshi lakini kuna vibaka,police ni wachache hawawezi kuzunguka maeneo yote hivyo tumetengeneza vikundi vya ulinzi wenyewe huku tuna majukumu mengine na kibaya zaidi tunawalinda na hao askar usiku badala ya wao kutulinda sisi kwa sababu ndo kazi yao.Serikali fanyieni kazi huu ushauri,watumieni vizur askar wa vikosi vyote ili raia wawe na amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kiongozi! Ukweli kunashida katika kipengere hiki! kama serikal inavyombo vya ulinzi vingi namna hii kwanini mzigo wa kujilinda waurudishe kwetu wananchi? huku siyo kukwepa majukum!!! wangine wanalazimishwa kulala nje, wamefundishwa tu kidogo. huku sikutafuta kutoana kafara?
 
Kuna sungusungu watu kumi kumi kila week inaenda nyumba baada ya nyumba.
Ambae hawawezi ndio hutoa pesa.
 
Ulinzi gani wanamna hii jamani! kama ikienda nyumba moja baada ya nyingine namana hii! huoni kama nilahisi kwa wahalifu kuusoma mzunguko na wakafanya uharifu bilashida yoyote!!!
 
Mi nafikiri Tanzania tunashindwa kutumia rasirimali watu vizuri. Nilishawahi kutoa pendekezo kwenye bandiko langu nililoliweka baada ya kutoka Rwanda.Vikosi vyote vya ulinzi na usalama vinashirikiana vizuri kulinda raia na mali zao kwa kipindi hiki cha amani,sasa huku unakuta wanajeshi wetu hatumiki hivyo zaidi ya kulinda kambi zao na mipakani.Ninaumia sana huku nilipo kuna kambi ya jeshi lakini kuna vibaka,police ni wachache hawawezi kuzunguka maeneo yote hivyo tumetengeneza vikundi vya ulinzi wenyewe huku tuna majukumu mengine na kibaya zaidi tunawalinda na hao askar usiku badala ya wao kutulinda sisi kwa sababu ndo kazi yao.Serikali fanyieni kazi huu ushauri,watumieni vizur askar wa vikosi vyote ili raia wawe na amani.

Sent using Jamii Forums mobile app
wakati wa amani si kwamba majeshi yamelala,kuna kazi ya ulinzi kubwa kuliko wakati wa vita.kuna suala la mafunzo ndani nje ya nchi,kuna masuala ya kujifunza zana mpya kuna mazoezi ya kila siku,tathimin za kazi,mahakama za kijeshi,intelejensia ,mipaka nk.
kwa kifupi jw itolewe wakati maalumu tu hasa majanga sio routine za uraiani,kuwazoeza wanajeshi maisha ya uraiani kuna madhara kimfumo wa jeshi,mfano polisi akija kukukagua utamuhoji je na jw utamuhoji?kwa sheria ipi.
kuna mtu alisema simba akizoea kula nyama ya mtu hataacha na ataona kumtafuta swala ni gharama kumkimbiza kuliko kula binadam.
ulinzi shirikishi ni dhana inayopewa nguvu na katiba kuwa kila mwananchi anapaswa kulinda rasilimali za nchi yake na ndo mlinzi wa kwanza.
lengo la kujilinda maana yake ni kuwa mtaani mnajijua na ni vigumu mharifu kutokea mbali pasipo msaada wa mwenyeji
 
Kuna jambo hili la ulinzi shirikishi ambalo naona linaendelea kushika kasi katika jamii yetu. Je, lipo kisheria? Kazi ya wizara ya ulinzi ni ipi kama wananchi tunatakiwa kujilinda wenyewe? Kama wanahitaji nguvu kazi zaidi kwanini wasiajiri badala ya kurudisha mzigo kwa wananchi?

Mi nachukizwa sana kudaiwa pesa ya ulinzi huu kila mwezi! Kwa nini wananchi ndo tulipie ulinzi huu wakati tunalipa kodi? Wizara hii ya ulinzi haipewi bajeti yake?

Mwenye uelewa zaidi anisaidie!
kuajiri watu wengi maana yake kuwa na uwezo wa kulipa stahili,swali la kujiuliza je bajeti yetu inatosha?kuajiri walimu wengi na askari wengi je kipi kipaumbele?kupanga ni kuchagua.
watu wengi hatuhudhurii vikao vya maamuzi hasa mikutano mikuu ya vijiji na mitaa,hapo ndio sehem sahihi ya kuanzia
kuna sera ya kuwa na jeshi dogo la kisasa ili kupunguza gharama,hivyo tufikirie kuwa unapokuwa na wafanyakazi wachache lazima uwa overload,je kazi za kambini zimekwisha mpaka waanze za uraiani?
 
wakati wa amani si kwamba majeshi yamelala,kuna kazi ya ulinzi kubwa kuliko wakati wa vita.kuna suala la mafunzo ndani nje ya nchi,kuna masuala ya kujifunza zana mpya kuna mazoezi ya kila siku,tathimin za kazi,mahakama za kijeshi,intelejensia ,mipaka nk.
kwa kifupi jw itolewe wakati maalumu tu hasa majanga sio routine za uraiani,kuwazoeza wanajeshi maisha ya uraiani kuna madhara kimfumo wa jeshi,mfano polisi akija kukukagua utamuhoji je na jw utamuhoji?kwa sheria ipi.
kuna mtu alisema simba akizoea kula nyama ya mtu hataacha na ataona kumtafuta swala ni gharama kumkimbiza kuliko kula binadam.
ulinzi shirikishi ni dhana inayopewa nguvu na katiba kuwa kila mwananchi anapaswa kulinda rasilimali za nchi yake na ndo mlinzi wa kwanza.
lengo la kujilinda maana yake ni kuwa mtaani mnajijua na ni vigumu mharifu kutokea mbali pasipo msaada wa mwenyeji
Fikra potofu hivi jw ndo hahojiwi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuajiri watu wengi maana yake kuwa na uwezo wa kulipa stahili,swali la kujiuliza je bajeti yetu inatosha?kuajiri walimu wengi na askari wengi je kipi kipaumbele?kupanga ni kuchagua.
watu wengi hatuhudhurii vikao vya maamuzi hasa mikutano mikuu ya vijiji na mitaa,hapo ndio sehem sahihi ya kuanzia
kuna sera ya kuwa na jeshi dogo la kisasa ili kupunguza gharama,hivyo tufikirie kuwa unapokuwa na wafanyakazi wachache lazima uwa overload,je kazi za kambini zimekwisha mpaka waanze za uraiani?
Nilitegemea sera ya kuwa na jeshi dogo isingeendani na kukwepa majukum! nikiri tu kwamba nikweli kwenye mikutano ya vijiji wengi hatuendi tunaishia kudaiwa pesa tu na hii maranyingi ni kwasababu ya kazi zetu! Lakini pamoja na hayo mchango mkubwa wa wananchi katika kuimalisha ulinzi ungetakiwa ufanyike kwa wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi,siyo wananchi waunde jeshilingine et kisa jeshi lililopo halitakiwi kuwa kubwa. Tungetumia technologia ya habari vizuri na wanaohusika na ulinzi wakazingatia kanuni zao juu ya kumlinda mtoa taarifa ingekuwa vizuri kuliko kututaka wananchi tuanze kulala nje et tunalinda!
Natamani serikal ihurumie wananchi kwa kuto kuwaweka kwenye risk kwa kiasi hiki! Hizo kazi za kambini hazitokuwa na maana kama raia hawatakuwa na amani.
 
Aisee nilishwaambia hapo mtaani asije akajichanganya mtu kuniambia habari za ulinzi shirikishi,kama ni hela nitatoa lkn habari za kulinda kwa zamu hio kwangu haipo.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Nchi ya viwanda itatoka wapi kama mchana mtu anashinda kazini afu usiku kucha eti akalinde mtaani kwake.

Hio kesho yake hapo kazini sijui utafanya kazi au utashinda unalala tu sababu ya uchovu wa kulinda usiku kucha.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 
Aisee nilishwaambia hapo mtaani asije akajichanganya mtu kuniambia habari za ulinzi shirikishi,kama ni hela nitatoa lkn habari za kulinda kwa zamu hio kwangu haipo.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
Ha,ha,ha, Utafanyeje na walinzi ndo hao! je siku ukiibiwa, wakati pesa yao unatoa kila mwezi utafanyeje?
 
Aisee mkuu waibe tu, saa 12 asubuhi uko road kwenda ofisini urudi hom saa 1 jioni then baadae mtu aniambie habari za kulinda.

Mi niliwaambia kama kuna kijana anaweza akalinda kwa niaba yangu hela ipo wakajifanya wanavunga walivyoona niko serious kutokuhusika na ulinzi wao ikabidi vijana waje niwape hela walinde tu.

Back
Top Bottom