Suala la uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa linalofanywa na RITA pamoja na HELB limekaaje?

Witmak255

JF-Expert Member
Feb 5, 2019
3,264
5,403
Jana mchana ninepigiwa simu na ndgu yangu ambae amemaliza kidato Cha sita hivi majuzi, amerudi kijijini kwa Wazazi wake baada ya kumaliza masomo yake ya advance. Alinipigia kuniomba nimsaidie Tsh 15,000/= ambayo ataitumia Kama nauli na malipo ya kuhakiki cheti chake Cha kuzaliwa ili aweze kuomba mkopo wa elimu ya juu mda ukifika.

Binafsi sikujua Kama Kuna Jambo hili, Ni Jambo jema kwa nchi na Wala Sina Sina shaka nalo kabisa, Ilinibidi niingie kwenye website ya hizi taasisi nipate habari zaidi, nikakuta ni kweli.

Kilichonishangaza, unaruhusiwa kuhakiki kwenye ofisi ya wilaya uliyochukulia tu na Kama uko mbali na ofisi uliyochukulia basi unawasilisha nakala yako ya cheti uliyoiscan kwa email ya ofisi husika baada ya kufanya malipo bank kwa account uliyoelekezwa ya Tsh 3000/= then ndio maombi yako yanafanyiwa kazi.

Imebidi niujiulize, Ina maana RITA wameshindwa nini kulink database yao ya majina ya watu waliowapa vyeti bodi ya mikopo? Hawa HELB wao wangeingiza namba za vyeti tu kwenye system, then system inaverify Kama cheti ni chenyewe au feki,... otherwise watuambie Kama hiki pia ni chanzo Cha mapato, haiwezekani ulipie kwenye kuomba cheti halafu waliokupa cheti waitishe UHAKIKI tena wakutoze pesa nyingine?

Kwa ulimwengu wa Sasa nisingetememea mtu aliyepata cheti Cha kuzaliwa NANJILINJI, halafu kimaisha Yuko MWANZA imlazimu tena kusafiri kwenda NANJILINJI kwa kukihakiki, Ina maana RITA hawana database ya vyeti wanavyotoa? Kama wanayo kwa nini asihakiki huko aliko?, Kwa nini tupeane gharama na usumbufu usiokuwa na sababu Wala maana.

Then kwa nini huu uhakiki unatozwa pesa? Kwa nini isiwe bure? Hivi vyeti vinachukuliwa kwenu RITA kwa malipo ya pesa kulingana na umri wa mhusika, why mumtoze pesa tena kuhakiki cheti mlichokitoa kwa malipo? Yaani NECTA au chuo nilichosoma wahitaji kufanya uhakiki wa cheti walichonipa, wanitoze pesa?

Serikali inapaswa kuangalia Sera zake kwa raia, sio kila Kitu kumkamua mnyonge, Uhakiki RITA ulipiwe, kuapply mkopo ulipie haijalishi utapata au la..!, Ni zaidi ya unyonyaji

Hili zoezi lingeweza kufanywa vizuri Sana hata bila malipo ya aina yeyote na kwa urahisi zaidi, najua kabisa pale RITA na bodi ya mikopo Kuna ma System Adminstrator tena wabobezi kabisa wangeweza kufanya hii kazi kwa system tu.. otherwise mumeamua kwa makusudi kuongeza mapato kwa kuwakamua hawa wanyonge wenu.
 
Serikali na taasisi zake kawaida hazifanyi biashara bali hutoa huduma...

Ila siku hizi ni tofauti sana, serikali na taasisi zake zimeanza kufanya biashara ili kuongeza pato la ndani...


Cc: mahondaw
 
Inasikitisha nchi kutegemea makaratasi kutunza kumbukumbu kwa karne hii, ndio maana hakuna mawasiliano kati ya sekta moja na nyingine na pia kila siku zoezi linarudiwa tena na tena.
 
Inasikitisha nchi kutegemea makaratasi kutunza kumbukumbu kwa karne hii, ndio maana hakuna mawasiliano kari ya sekya moja na nyingine na pia kila siku zoezi linarudiwa tena na tena.
Ndio nashangaa makuu, au wameamua kwa makusudi kuongeza mapato. Sitaki kuamini Kama mpka Sasa mifumo yetu ya makaratasi
 
Naona mkuu
Wameanza hii system since 2017, Kama umesoma diploma inabidi kile cheti tena kifanyie verification fee yake 10k.

Bado wanasisitiza vyeti viwe certified, muhuri wa mahakama not less 10k.

Tanzania is nothing but bandit.
 
Wameanza hii system since 2017, Kama umesoma diploma inabidi kile cheti tena kifanyie verification fee yake 10k.

Bado wanasisitiza vyeti viwe certified, muhuri wa mahakama not less 10k.

Tanzania is nothing but bandit.
Mimi nadhani hii ni njia ya kukusanya mapato, yaani NACTE Wana majina yote ya waliosoma diploma, RITA wanayo yote ya vyeti vya kuzaliwa katika system zao wanashindwaje kulink database zao na bodi ya mikopo system yenyewe ikafanya verification,...Nini maana ya matumizi ya tehama maofisini?
 
Mimi nadhani hii ni njia ya kukusanya mapato, yaani NACTE Wana majina yote ya waliosoma diploma, RITA wanayo yote ya vyeti vya kuzaliwa katika system zao wanashindwaje kulink database zao na bodi ya mikopo system yenyewe ikafanya verification,...Nini maana ya matumizi ya tehama maofisini?
Ni njia yakukusanya mapato yes. But on the other hand inaweka limitation kwa wanaopata vyeti kwa panya route.
 
Back
Top Bottom