Suala la Tanzania na Kenya, mahusiano mazuri siyo sababu ya kutoheshimu sheria za nchi nyingine

JINOME

JF-Expert Member
May 29, 2017
958
1,424
Ni kwa mujihu wa Sheria za nchi, Tanzania ilipiga Mnada Ng'ombe 1500 na kuteketeza Vifaranga 6,000 walioingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka Kenya.

Baada ya matukio hayo, kumekuwepo na maneno maneno ya kutaka kuonesha kuwa Tanzania imekosea, Rais Wetu Magufuli ni mbaya, sijui Mahusiano kati ya Tanzania na Kenya yanaharibika.

Maneno yote haya yanatoka ndani ya nchi yetu na Kenya yenyewe. Nasema maneno haya hayana msingi wowote zaidi ni uchochezi tu, ni kutaka huruma tu kutoka kwa wananchi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Hivi kwa sababu tu tuna mahusiano mazuri, watu waingie hovyo hovyo nchini bila mpangilio?

Tumesahau kuwa siku zote tumekuwa na ugomvi kati wakulima na wafugaji wetu kwa sababu ya kukosa maeneo ya malisho ya mifugo ya watu wetu?

Kwanini uingizaji huu holela wa mifugo kutoka nje isiwe sababu ya watu wetu kufarakana?

Je, ni kweli kwamba ni mara ya kwanza mifugo hiyo kuingiziwa nchini kinyume au ni mchezo uliozoeleka lakini hakuna aliyejali, na mazoea hayo ndiyo yalitakiwa yaendelee?

Hawa Watanzania wanaoungana na Wakenya kuishutumu nchi yao wana maslahi gani na huo mtazamo wao, ni kutafuta tu umaarufu wa kisiasa au kitu gani? Lini wafugaji wetu walienda na mifugo yao Kenya?

Tumesahau kuwa juzi juzi Wakenya hao hao wa walikataa tusiingize nchini mwao Gesi, hawakuoana hatari ya Mahusiano kuharibika au sisi tunaowashabikia hatukuona athari ya Mahusiano kuharibika?

Wale ambao mlishajivua uzalendo kama akina Mange Kimambi, Kwinyara, Malisa na wengine kwa kisingzio cha hofu ya Mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kuvunjika kaeni na uasi wenu.

Mahusiano yaharibike yasiharibike, lazima kama Nchi ifike mahali tuwe ma misimamo yetu, hakuna kuchezewa tena.

Eti kuna Watanzania wako Kenya, Kenya wakiamua kuwafukuza itakuwaje, Upuuzi kabisa, hivi Kati Tanzania na Kenya ni wapi kuna Wageni zaidi, Watanzania ni wengi Kenya kuliko Wakenya walivyo Tanzania?

Upuuzi huu.
 
Sheria za kila nchi ziheshimiwe. Kuwa na mahusiano mazuri na nchi nyingine ni pamoja na kuheshimu sheria na taratibu za nchi hiyo.
 
Wakenya ni wapuizi sana, tulianzishe tuone kama Dar haijabaki nyeupe maana wamejazana sana humu
 
Ana akili sana ndugu Yangu ya kuwaelewesha wenye akili sawa sawa na kimambi watanzania wadumavu
 
Wakenya watalia Hadi wasage meno ila tukishika wanyama wengine tutafanya kwa mujibu wa sheria za TZ na wao wawe huru kufanya vile iwapendezavyo. Mbona wanalialia kama watoto wakati wapo huru kufanya kwa mujibu wa sheria zao.

Chuma Magufuli aliwakana watanzania waishio Msumbiji kinyume cha sheria ndo sembuse Wanyama.
 
Ni kwa mujihu wa Sheria za nchi, Tanzania ilipiga Mnada Ng'ombe 1500 na kuteketeza Vifaranga 6,000 walioingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka Kenya.

Baada ya matukio hayo, kumekuwepo na maneno maneno ya kutaka kuonesha kuwa Tanzania imekosea, Rais Wetu Magufuli ni mbaya, sijui Mahusiano kati ya Tanzania na Kenya yanaharibika.

Maneno yote haya yanatoka ndani ya nchi yetu na Kenya yenyewe. Nasema maneno haya hayana msingi wowote zaidi ni uchochezi tu, ni kutaka huruma tu kutoka kwa wananchi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Hivi kwa sababu tu tuna mahusiano mazuri, watu waingie hovyo hovyo nchini bila mpangilio?

Tumesahau kuwa siku zote tumekuwa na ugomvi kati wakulima na wafugaji wetu kwa sababu ya kukosa maeneo ya malisho ya mifugo ya watu wetu?

Kwanini uingizaji huu holela wa mifugo kutoka nje isiwe sababu ya watu wetu kufarakana?

Je, ni kweli kwamba ni mara ya kwanza mifugo hiyo kuingiziwa nchini kinyume au ni mchezo uliozoeleka lakini hakuna aliyejali, na mazoea hayo ndiyo yalitakiwa yaendelee?

Hawa Watanzania wanaoungana na Wakenya kuishutumu nchi yao wana maslahi gani na huo mtazamo wao, ni kutafuta tu umaarufu wa kisiasa au kitu gani? Lini wafugaji wetu walienda na mifugo yao Kenya?

Tumesahau kuwa juzi juzi Wakenya hao hao wa walikataa tusiingize nchini mwao Gesi, hawakuoana hatari ya Mahusiano kuharibika au sisi tunaowashabikia hatukuona athari ya Mahusiano kuharibika?

Wale ambao mlishajivua uzalendo kama akina Mange Kimambi, Kwinyara, Malisa na wengine kwa kisingzio cha hofu ya Mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kuvunjika kaeni na uasi wenu.

Mahusiano yaharibike yasiharibike, lazima kama Nchi ifike mahali tuwe ma misimamo yetu, hakuna kuchezewa tena.

Eti kuna Watanzania wako Kenya, Kenya wakiamua kuwafukuza itakuwaje, Upuuzi kabisa, hivi Kati Tanzania na Kenya ni wapi kuna Wageni zaidi, Watanzania ni wengi Kenya kuliko Wakenya walivyo Tanzania?

Upuuzi huu.
Wakafie mbele hao Manyang'au
Nchi yetu si Somalia au Sudani ya Kusini ya kuifanya watakavyo
 
Back
Top Bottom