Ni kwa mujihu wa Sheria za nchi, Tanzania ilipiga Mnada Ng'ombe 1500 na kuteketeza Vifaranga 6,000 walioingizwa nchini kinyume cha sheria kutoka Kenya.
Baada ya matukio hayo, kumekuwepo na maneno maneno ya kutaka kuonesha kuwa Tanzania imekosea, Rais Wetu Magufuli ni mbaya, sijui Mahusiano kati ya Tanzania na Kenya yanaharibika.
Maneno yote haya yanatoka ndani ya nchi yetu na Kenya yenyewe. Nasema maneno haya hayana msingi wowote zaidi ni uchochezi tu, ni kutaka huruma tu kutoka kwa wananchi ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Hivi kwa sababu tu tuna mahusiano mazuri, watu waingie hovyo hovyo nchini bila mpangilio?
Tumesahau kuwa siku zote tumekuwa na ugomvi kati wakulima na wafugaji wetu kwa sababu ya kukosa maeneo ya malisho ya mifugo ya watu wetu?
Kwanini uingizaji huu holela wa mifugo kutoka nje isiwe sababu ya watu wetu kufarakana?
Je, ni kweli kwamba ni mara ya kwanza mifugo hiyo kuingiziwa nchini kinyume au ni mchezo uliozoeleka lakini hakuna aliyejali, na mazoea hayo ndiyo yalitakiwa yaendelee?
Hawa Watanzania wanaoungana na Wakenya kuishutumu nchi yao wana maslahi gani na huo mtazamo wao, ni kutafuta tu umaarufu wa kisiasa au kitu gani? Lini wafugaji wetu walienda na mifugo yao Kenya?
Tumesahau kuwa juzi juzi Wakenya hao hao wa walikataa tusiingize nchini mwao Gesi, hawakuoana hatari ya Mahusiano kuharibika au sisi tunaowashabikia hatukuona athari ya Mahusiano kuharibika?
Wale ambao mlishajivua uzalendo kama akina Mange Kimambi, Kwinyara, Malisa na wengine kwa kisingzio cha hofu ya Mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kuvunjika kaeni na uasi wenu.
Mahusiano yaharibike yasiharibike, lazima kama Nchi ifike mahali tuwe ma misimamo yetu, hakuna kuchezewa tena.
Eti kuna Watanzania wako Kenya, Kenya wakiamua kuwafukuza itakuwaje, Upuuzi kabisa, hivi Kati Tanzania na Kenya ni wapi kuna Wageni zaidi, Watanzania ni wengi Kenya kuliko Wakenya walivyo Tanzania?
Upuuzi huu.