Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,602
Katika mambo yote yanayohusu matumizi ya fedha huwa kuna pande mbili. Upande wa mnunuzi wa pesa 'Buy side' upande wa muuzaji wa pesa 'Sell side'. Kwahiyo tayari hii ni transaction kamili kama vile ilivo mtu unavoenda dukani kununua mkate, mnunuzi unahitaji mkate ili ukanywe chai na muuzaji unahitaji kuuza huo mkate ili utengeneze faida. Kwa maana hiyo, kabla pesa haijabadilisha mikono kutoka kwa muuzaji wa pesa kwenda kwa mnunuzi wa pesa, ni lazima kila upande ujue na kujiridhisha ikiwa maslahi yake baada ya mabadilishano hayo kufanyika, yataridhishwa.
Kwa miaka mitano iliyopita hapa Tanzania, kumetokea transactions nyingi ambazo zinahusisha transactions za kiffedha kama nilivoeleza hapo juu. Ila ntatumia mifano miwili ya transactions hizo kwasababu ni masuala mapana yanayogusa hisia za jamii ya watanzania na ni masuala ambayo yana ufanano fulani ukiangalia aina ya maamuzi.
Ukianza na suala la kwanza, la serikali kuwekeza Trillioni 1 kwenye shirika la ndege la ATCL. Kwanza kabisa hapa tunaona muuzaji wa pesa ni Serikali na mnunuzi wa pesa ni ATCL. Sasa kwenye transaction ya aina hii, ingepaswa Serikali kama muuzaji wa pesa au mwekezaji, ni lazima kwanza angetakiwa kupata taarifa halisi za kifedha za kampuni ya ATCL.
Na ukishapata taarifa za kifedha za kampuni zitakueleza wazi na kukupa taarifa nyingi sana. Kama;
So somo hapa ni kwamba, kwenye situation ambayo kampuni inakuwa ipo hohe hahe, kwenye mabadilishano ya pesa, mwekezaji ndio unapaswa kuwa makini Zaidi kuliko mnunuzi wa pesa ‘kampuni’. Kwa hiyo kwenye suala la serikali kuwekeza kwa ATCL, ni serikali ndio wangepaswa kuwa Zaidi ya makini, kwasababu upande wa mnunuzi wa pesa ‘ATCL’ sote tunajua ni shirika ambao lilikuwa tayari ni mfu.
Ukija kwenye suala la pili, la klabu ya Simba kuuza hisa zake asilimia 49 kwa mwekezaji Mo Dewji kwa kiasi cha Bilioni 20. Hapa pia tunaweza kuona upungufu wa tathmini ya kifedha ambao naona kabisa kuna upande kwenye hii transaction umepoteza.
Utofauti kidogo wa uwekezaji wa serikali kwa ATCL ambapo tunaona all parties of transactions ni serikali. Kwenye suala la Simba, all parties of transactions ni sekta binafsi, Mo Dewji akiwa ‘muuzaji wa pesa’ na Simba wakiwa ni ‘wanunuzi wa pesa’ huku makubaliano yao yakiwa nu kubadilishana hizo hisa asilimia 49.
Na wanasimba tunatakiwa tuelewe, Mo Dewji ni mwekezaji kama wawekezaji wengine, na yupo pale kwa ajili ya maslahi. Inaweza isiwe kwenye monetary terms, kama directly kuchukua cash za Simba kwa sababu ni mwekezaji, ila itakuwa kutumia mgongo wa brand ya Simba kutangaza biashara zake. So ana win vikubwa kwengine.
Hivo basi, tukiangalia thinking process ya suala la serikali na ATCL, nataka nitoe mawazo yangu kuhusu hili la Simba.
Watu wanauliza, na mimi nauliza, ni njia zipi zilitumika kufika kwenye thamani ya hisa za Simba asilimia 49 kuuzwa kwa Bilioni 20?
Mi nahisi, kwa sababu Simba ni klabu ya sisi wanachama, ambao pia tunahaki na klabu yetu ya Simba, kabla ya huu mchakato, ingepaswa klabu ya Simba ifanye IPO ambayo ingekuwa ni document itayoeleza lengo la kuuza hisa asilimia 49 na hapo hapo IPO ingeonesha wazi, hizo pesa zingetumika kwa ajili ya matumizi yapi.
Kupitia IPO hiyo tungepata pia kujua taarifa za kifedha za Simba ili tuweze kufanya tathmini ya kifedha ili tuweze kujua ikiwa kuna gap kwenye operations na kwa kiasi gani na ni vip gap hilo litaweza kuwa financed. Kupitia taarifa za kifedha, ndipo haswa klabu ya Simba ingeweza kufanya makadirio ya thamani halisi ya kampuni ya Simba ikiwa kama walikuwa na nia ya kufanya mauzo ya hisa za Simba.
Sijawahi ona duniani, kampuni inauza hisa halafu wanasema pesa zinatumika ku finance operations kama kulipa mishahara na kufanya usajili. Mara nyingi, mauzo ya hisa ama kukusanya pesa huwa inatakiwa pesa hiyo ifanye uwekezaji wa muda mrefu, maana yake ni kwamba, kwa klabu kama Simba, ningetegemea, walivo off-load karibu nusu ya hisa za kampuni, basi wangepata pesa za kujenga uwanja wa kisasa ila sioni hilo likitokea.
Leo hii ‘Muuzaji wa pesa’ anazungumza kwenye media as if kwamba yeye anatoa msaada kwa Simba, unajiuliza ina maana Simba walikuwa hohe hahe? Hivi ni kweli klabu ya Simba walikuwa hawana vyanzo vingine vya pesa? Hivi ni kweli thamani ya Klabu ya Simba ambayo ina mashabiki Zaidi ya Milioni 30 nchi hii ni Bilioni 40?
Hivi kweli watu, wanavoipenda Simba, kama wangesema leo hii wanaenda kuweka hisa kwenye IPO tuzigombanie, ikiwa wangejitokeza watu kama 200,000 na kila mtu akatoa 100,000 ina maana hiyo tayari ni uwekezaji wa MO Dewji kwa Simba.
Na hawawazi kutokea watu laki mbili tu kugombani hisa za Simba, unazungumzia watu Zaidi ya milioni moja ambao wamezagaa kwenye viunga vya nchi hii. Unazungumzia watu milioni moja wenye uwezo wa kuwekeza laki mbili kwa klabu ya simba. Unazungumzia thamani ya zaidi ya Bilioni 200 ambazo zingeweza kupatikana.
Maana yake ni kwamba. Klabu ya Simba wangepaswa kufanya hizi tathmini zote za uthamani wao kabla ya kuamua kufanya walichofanya. Simba is worth more than 200 Billion. Na mi nakuambia kama akili ingetumika vizuri, Simba kuuza hisa zao 49% wangetakiwa sasahivi wafikiria kujenga uwanjwa kama ule Benjamin Mkapa.
Anyway, mtasema nna wivu na kijiba cha roho kwa klabu ya Simba na Mo. Ila mimi ntazidi kuongea maana kuna mambo ya kijinga na ya hovyo sana nchi hii. Hii inaumiza moyo. Haiwezekani tuendelee kuruhusu huu upumbavu kwenye hili taifa, Lazima tuendelee kuhoji.
N.Mushi

- Suala la serikali kuwekeza takribani zaidi ya Trillioni 1 kwenye shirika la ndege la ATCL
- Suala la klabu ya michezo ya Simba kuuza takribani asilimia 49 ya hisa zake kwa mwekezaji Mo Dewji.
Ukianza na suala la kwanza, la serikali kuwekeza Trillioni 1 kwenye shirika la ndege la ATCL. Kwanza kabisa hapa tunaona muuzaji wa pesa ni Serikali na mnunuzi wa pesa ni ATCL. Sasa kwenye transaction ya aina hii, ingepaswa Serikali kama muuzaji wa pesa au mwekezaji, ni lazima kwanza angetakiwa kupata taarifa halisi za kifedha za kampuni ya ATCL.
Na ukishapata taarifa za kifedha za kampuni zitakueleza wazi na kukupa taarifa nyingi sana. Kama;
- Je? Business model ya kampuni ni sahihi? Ikiwa tutawaongezea Trillioni moja kama assets kwa njia ya kununua ndege mpya, je kuna uwezekano ukaleta tija kwenye kampuni?
- Je? Menejimenti ya kampuni ni watu wanaoweza ku meneji amana za Zaidi ya Trillioni moja?
- Je? Kampuni ina madeni mengine ambayo yanaweza ku impact kufanya core business yake?
- Je? Kwa mwenendo wa cashflow za kampuni, ni sahihi kuanza na Trillioni moja kwa mkupuo ama kuanza taratibu na ku monitor hali ya kibiashara ya kampuni?