Suala la serikali kununua ndege na suala la Dewji kununua hisa za simba yana ufanano wa maamuzi yanayofanyika bila tathmini ya kifedha

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Katika mambo yote yanayohusu matumizi ya fedha huwa kuna pande mbili. Upande wa mnunuzi wa pesa 'Buy side' upande wa muuzaji wa pesa 'Sell side'. Kwahiyo tayari hii ni transaction kamili kama vile ilivo mtu unavoenda dukani kununua mkate, mnunuzi unahitaji mkate ili ukanywe chai na muuzaji unahitaji kuuza huo mkate ili utengeneze faida. Kwa maana hiyo, kabla pesa haijabadilisha mikono kutoka kwa muuzaji wa pesa kwenda kwa mnunuzi wa pesa, ni lazima kila upande ujue na kujiridhisha ikiwa maslahi yake baada ya mabadilishano hayo kufanyika, yataridhishwa.

Kwa miaka mitano iliyopita hapa Tanzania, kumetokea transactions nyingi ambazo zinahusisha transactions za kiffedha kama nilivoeleza hapo juu. Ila ntatumia mifano miwili ya transactions hizo kwasababu ni masuala mapana yanayogusa hisia za jamii ya watanzania na ni masuala ambayo yana ufanano fulani ukiangalia aina ya maamuzi.
  1. Suala la serikali kuwekeza takribani zaidi ya Trillioni 1 kwenye shirika la ndege la ATCL
  2. Suala la klabu ya michezo ya Simba kuuza takribani asilimia 49 ya hisa zake kwa mwekezaji Mo Dewji.

Ukianza na suala la kwanza, la serikali kuwekeza Trillioni 1 kwenye shirika la ndege la ATCL. Kwanza kabisa hapa tunaona muuzaji wa pesa ni Serikali na mnunuzi wa pesa ni ATCL. Sasa kwenye transaction ya aina hii, ingepaswa Serikali kama muuzaji wa pesa au mwekezaji, ni lazima kwanza angetakiwa kupata taarifa halisi za kifedha za kampuni ya ATCL.

Na ukishapata taarifa za kifedha za kampuni zitakueleza wazi na kukupa taarifa nyingi sana. Kama;
  • Je? Business model ya kampuni ni sahihi? Ikiwa tutawaongezea Trillioni moja kama assets kwa njia ya kununua ndege mpya, je kuna uwezekano ukaleta tija kwenye kampuni?
  • Je? Menejimenti ya kampuni ni watu wanaoweza ku meneji amana za Zaidi ya Trillioni moja?
  • Je? Kampuni ina madeni mengine ambayo yanaweza ku impact kufanya core business yake?
  • Je? Kwa mwenendo wa cashflow za kampuni, ni sahihi kuanza na Trillioni moja kwa mkupuo ama kuanza taratibu na ku monitor hali ya kibiashara ya kampuni?
Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo huwa yanategemewa kwa mtu yeyote anayeuza pesa ‘Mwekezaji’ na ni aina ya mambo tuliyategema kufanyika kabla la serikali kuamua ku sacrifice taxpayers money kwenye kampuni ambayo mimi binafsi sina uhakika Zaidi ya asilimia moja ikiwa ndani ya miaka 10 ijayo itaweza hata kufika hata level ya ku break-even. Ni kama serikali ilitupa pesa, coz ‘you cannot ride a dead horse’.

So somo hapa ni kwamba, kwenye situation ambayo kampuni inakuwa ipo hohe hahe, kwenye mabadilishano ya pesa, mwekezaji ndio unapaswa kuwa makini Zaidi kuliko mnunuzi wa pesa ‘kampuni’. Kwa hiyo kwenye suala la serikali kuwekeza kwa ATCL, ni serikali ndio wangepaswa kuwa Zaidi ya makini, kwasababu upande wa mnunuzi wa pesa ‘ATCL’ sote tunajua ni shirika ambao lilikuwa tayari ni mfu.

Ukija kwenye suala la pili, la klabu ya Simba kuuza hisa zake asilimia 49 kwa mwekezaji Mo Dewji kwa kiasi cha Bilioni 20. Hapa pia tunaweza kuona upungufu wa tathmini ya kifedha ambao naona kabisa kuna upande kwenye hii transaction umepoteza.

Utofauti kidogo wa uwekezaji wa serikali kwa ATCL ambapo tunaona all parties of transactions ni serikali. Kwenye suala la Simba, all parties of transactions ni sekta binafsi, Mo Dewji akiwa ‘muuzaji wa pesa’ na Simba wakiwa ni ‘wanunuzi wa pesa’ huku makubaliano yao yakiwa nu kubadilishana hizo hisa asilimia 49.

Na wanasimba tunatakiwa tuelewe, Mo Dewji ni mwekezaji kama wawekezaji wengine, na yupo pale kwa ajili ya maslahi. Inaweza isiwe kwenye monetary terms, kama directly kuchukua cash za Simba kwa sababu ni mwekezaji, ila itakuwa kutumia mgongo wa brand ya Simba kutangaza biashara zake. So ana win vikubwa kwengine.

Hivo basi, tukiangalia thinking process ya suala la serikali na ATCL, nataka nitoe mawazo yangu kuhusu hili la Simba.

Watu wanauliza, na mimi nauliza, ni njia zipi zilitumika kufika kwenye thamani ya hisa za Simba asilimia 49 kuuzwa kwa Bilioni 20?

Mi nahisi, kwa sababu Simba ni klabu ya sisi wanachama, ambao pia tunahaki na klabu yetu ya Simba, kabla ya huu mchakato, ingepaswa klabu ya Simba ifanye IPO ambayo ingekuwa ni document itayoeleza lengo la kuuza hisa asilimia 49 na hapo hapo IPO ingeonesha wazi, hizo pesa zingetumika kwa ajili ya matumizi yapi.

Kupitia IPO hiyo tungepata pia kujua taarifa za kifedha za Simba ili tuweze kufanya tathmini ya kifedha ili tuweze kujua ikiwa kuna gap kwenye operations na kwa kiasi gani na ni vip gap hilo litaweza kuwa financed. Kupitia taarifa za kifedha, ndipo haswa klabu ya Simba ingeweza kufanya makadirio ya thamani halisi ya kampuni ya Simba ikiwa kama walikuwa na nia ya kufanya mauzo ya hisa za Simba.

Sijawahi ona duniani, kampuni inauza hisa halafu wanasema pesa zinatumika ku finance operations kama kulipa mishahara na kufanya usajili. Mara nyingi, mauzo ya hisa ama kukusanya pesa huwa inatakiwa pesa hiyo ifanye uwekezaji wa muda mrefu, maana yake ni kwamba, kwa klabu kama Simba, ningetegemea, walivo off-load karibu nusu ya hisa za kampuni, basi wangepata pesa za kujenga uwanja wa kisasa ila sioni hilo likitokea.

Leo hii ‘Muuzaji wa pesa’ anazungumza kwenye media as if kwamba yeye anatoa msaada kwa Simba, unajiuliza ina maana Simba walikuwa hohe hahe? Hivi ni kweli klabu ya Simba walikuwa hawana vyanzo vingine vya pesa? Hivi ni kweli thamani ya Klabu ya Simba ambayo ina mashabiki Zaidi ya Milioni 30 nchi hii ni Bilioni 40?

Hivi kweli watu, wanavoipenda Simba, kama wangesema leo hii wanaenda kuweka hisa kwenye IPO tuzigombanie, ikiwa wangejitokeza watu kama 200,000 na kila mtu akatoa 100,000 ina maana hiyo tayari ni uwekezaji wa MO Dewji kwa Simba.

Na hawawazi kutokea watu laki mbili tu kugombani hisa za Simba, unazungumzia watu Zaidi ya milioni moja ambao wamezagaa kwenye viunga vya nchi hii. Unazungumzia watu milioni moja wenye uwezo wa kuwekeza laki mbili kwa klabu ya simba. Unazungumzia thamani ya zaidi ya Bilioni 200 ambazo zingeweza kupatikana.

Maana yake ni kwamba. Klabu ya Simba wangepaswa kufanya hizi tathmini zote za uthamani wao kabla ya kuamua kufanya walichofanya. Simba is worth more than 200 Billion. Na mi nakuambia kama akili ingetumika vizuri, Simba kuuza hisa zao 49% wangetakiwa sasahivi wafikiria kujenga uwanjwa kama ule Benjamin Mkapa.

Anyway, mtasema nna wivu na kijiba cha roho kwa klabu ya Simba na Mo. Ila mimi ntazidi kuongea maana kuna mambo ya kijinga na ya hovyo sana nchi hii. Hii inaumiza moyo. Haiwezekani tuendelee kuruhusu huu upumbavu kwenye hili taifa, Lazima tuendelee kuhoji.

N.Mushi
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,430
2,000
Ningependa uelezee vizuri hapo kwa Mo ni vipi ana win pakubwa, kwa sasa kama nijuavyo, Mo ndie analipa mishahara ya wachezaji, anasajili wachezaji, anaweka timu kambini, anatoa bonus, anasafirisha timu kwa ndege kwenda kote mikoani na nje ya nchi kwa mashindano mbalimbali.

Binafsi naona kama hapa huwa inatumika hisia zaidi ku-conclude Mo anavuna pakubwa toka Simba SC, unless aje mtu anioneshe kwa mahesabu kitu gani Mo anapata kutoka kwa Simba, then tutoe hizo gharama nilizoorodhesha pale juu, ndio ijulikane kama Simba inapigwa au vipi.

Na kama ni brand ya Simba SC, Mo himself amechangia kuikuza kutokana na uwekezaji wake anaoufanya, mafanikio ya Simba kwa ngazi ya vilabu bingwa Afrika ni kutokana na nguvu za Mo kiuchumi, kwani kabla ya hapo Simba ilikuwa inaringia fan base waliyonayo ambayo hata hivyo hawakujua waitumie kwa namna gani ili kuiletea maendeleo klabu.
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
Ningependa uelezee vizuri hapo kwa Mo ni vipi ana win pakubwa, kwa sasa kama nijuavyo, Mo ndie analipa mishahara ya wachezaji, anasajili wachezaji, anaweka timu kambini, anatoa bonus, anasafirisha timu kwa ndege kwenda kote mikoani na nje ya nchi kwa mashindano mbalimbali...
Hii mindset ya kusema Mo anatoa pesa za kufanya hiki na kile, hatuwezi kuthibitisha uhalali wake ikiwa Simba haichapishi taarifa zake za kifedha. Kuonesha kama klabu imetengeneza pesa kiasi gani na matumizi yake ni kiasi gani.

Na sijui serikali kwanini imelala, ingekuwa mimi ni waziri wa michezo ningeshurutisha hizi klabu za wanachama zote ziwe zinatoa taarifa za kifedha kila mwaka.

Ukiwa na taarifa ya kifedha itakuwa inakusaidia kujua kila mwaka club imetengeneza kiasi gani cha pesa na imetumia kiasi gani.

Sasa mimi sijawahi kuona popote taaarifa za kifedha za Simba, naskia kila siku mnasema Mo analipa mishahara anafanya hiki anafanya kile, ni as if Simba ni hohe hahe kitu ambacho mimi siamini.

Ukweli lazima uwekwe wazi kwa pande zote, we need to get facts!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,430
2,000
Hii mindset ya kusema Mo anatoa pesa za kufanya hiki na kile, hatuwezi kuthibitisha uhalali wake ikiwa Simba haichapishi taarifa zake za kifedha. Kuonesha kama klabu imetengeneza pesa kiasi gani na matumizi yake ni kiasi gani...
I thought ungekuja na hizo facts ili kuhalalisha bandiko lako, vinginevyo hoja uliyoiweka hapa haijitoshelezi, kuna taarifa ulitakiwa ukusanye kwanza kabla ya kuja na hoja nusu nusu.

Moreover, hata kama Simba ni tajiri kwa mtazamo wako, ndio nikakujibu pale juu, huo "utajiri" unaosema upo haukuwahi kuinufaisha Simba SC kwa chochote, ni mpaka Mo alivyokuja Simba SC, ndio watu wa aina yako mkajitokeza.

Mo ni mfanyabiashara, lazima kabla ya kulalamika anaiibia klabu, ukumbuke pia anachotoa kwa Simba SC, hapo ndio utatengeneza fair argument, na kiwe calculated kujua which is which.
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
4,520
2,000
I thought ungekuja na hizo facts ili kuhalalisha bandiko lako, vinginevyo hoja uliyoiweka hapa haijitoshelezi, kuna taarifa ulitakiwa ukusanye kwanza kabla ya kuja na hoja nusu nusu.

Moreover, hata kama Simba ni tajiri kwa mtazamo wako, ndio nikakujibu pale juu, huo "utajiri" unaosema upo haukuwahi kuinufaisha Simba SC kwa chochote, ni mpaka Mo alivyokuja Simba SC, ndio watu wa aina yako mkajitokeza.

Mo ni mfanyabiashara, lazima kabla ya kulalamika anaiibia klabu, ukumbuke pia anachotoa kwa Simba SC, hapo ndio utatengeneza fair argument, na kiwe calculated kujua which is which.
Ndo mana nikakuambia.. masuala yoyote yanayohusu pesa huwezi ukayajadili bila uwepo wa taarifa za kifedha.

Mimi nnachohitaji ni kwanza kupata taarifa za kifedha za Simba ambazo mpaka sasa sijawahi kuziona popote, ndiposa sasa nianze kuthibitisha ikiwa kweli Simba ni hohe hahe kiasi cha kukosa kulipa miashahara kiasi cha kumtegemea mwekezaji Mo.
 

Anonymous Caller

Senior Member
Sep 8, 2016
197
250
Kama Atcl inaendesha shirika kwa hasara basi ni kwa kujitakia kwao.

Nchi ina watu zaidi ya milion 50.
aiport destinations zipo takriban kila mkoa.
iweje popular Air routes ziwe mbili tu.

Bei yao ipo juu.
kutokana na bei kutokuwa rafiki midege mingi inasafiri ikiwa vacant.
hebu wafanye flat fare..kwamba bei iwe laki moja..haijalishi popote uendako waone foleni ya tiketi.

Udalali wa air tiketi.
ukomeshwe, pasiwe na variation ya nauli kunakotokana na
muda ama udharura.nauli iwe ileile.

Kujitangaza na ofa.
sijawahi kusikia tangazo lolote la atcl iwe redion, kwny simu wala tv.
hata tbc!

Uteuzi wa boss wa shirika..
serikali itangaze nafasi hiyo kuwa wazi..na kwamba wahitaji waombe.
ifanyike public interview kila applicant aeleze kwann ateuliwe yeye na si mwingne..atafanya nn kukabiliana na changamoto za atcl na aviation business kwa ujumla.

Iwe ni lazima kwa Public officials kutumia public airline..iwe ni kwa nauli ya umma au yao binafsi.
 

DENLSON

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
648
1,000
Ningependa uelezee vizuri hapo kwa Mo ni vipi ana win pakubwa, kwa sasa kama nijuavyo, Mo ndie analipa mishahara ya wachezaji, anasajili wachezaji, anaweka timu kambini, anatoa bonus, anasafirisha timu kwa ndege kwenda kote mikoani na nje ya nchi kwa mashindano mbalimbali.

Binafsi naona kama hapa huwa inatumika hisia zaidi ku-conclude Mo anavuna pakubwa toka Simba SC, unless aje mtu anioneshe kwa mahesabu kitu gani Mo anapata kutoka kwa Simba, then tutoe hizo gharama nilizoorodhesha pale juu, ndio ijulikane kama Simba inapigwa au vipi.

Na kama ni brand ya Simba SC, Mo himself amechangia kuikuza kutokana na uwekezaji wake anaoufanya, mafanikio ya Simba kwa ngazi ya vilabu bingwa Afrika ni kutokana na nguvu za Mo kiuchumi, kwani kabla ya hapo Simba ilikuwa inaringia fan base waliyonayo ambayo hata hivyo hawakujua waitumie kwa namna gani ili kuiletea maendeleo klabu.
MO anafaidika zaidi na Simba kuliko Simba kufaidika na MO kwa sababu zifuatazo.

1. MO anatumia brand ya Simba kufanyia matangazo ya biashara zake kwa mfano. NMB walikuwa na mkataba na timu ya Azam ambapo nembo ya NMB iliwekwa kwenye jezi ya Azam na Azam walikuwa wanalipwa 1 billion kwa mwaka. Kwa maana nyingine MO alitakiwa kuwalipa Simba 2 -3 billion kwa matangazo ya biashara zake kwenye jezi ya Simba.

2. Udhamini wa Sportpessa na Azam TV. Fedha zote za udhamini zinakwenda kwa MO kwasababu yeye ndio anae meneji fedha za Simba na bila shaka unafahamu kuwa Sportpessa wanatoa 1 billion kwa Simba na Azam ni 300-500 million kwa mwaka hivyo ukijumlisha inakuwa 1.4 billion

3. Viingilio vya uwanjani.

4. Mauzo ya Jezi. Nadhani umeona mkataba na vunja bei ni wa 3 billion hivyo ukiangalia na kulinganisha utagundua MO alikuwa anapata zaidi ya 3 billion kwa kuuza jezi za Simba.

5. Kuna uwezekano jezi anatengeneza MO sababu anakiwanda cha nguo hivyo hapo faida ni zaidi ya 2 billion.

Jumlisha zote hapo juu = 2 billion (brand usage) + 1.4 billion ( fee of other sponsors) + 500 m ( viingilio) + 3 billion (mauzo ya jezi )+ 2 billion ya (kutengeneza jezi) utagindua anapata zaidi ya 8 billion kwa mwaka.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom