Suala la posho ni tatizo zaidi ya tujuavyo

kasitile

Member
Feb 22, 2011
32
0
Habari wa JF.

Katika kikao cha bunge kilichopita,suala la posho lilileta msuguano sana hasa kwa vyama vya CHADEMA (isipokuwa Shibuda) na CCM.Katika hilo,Mhe.Zitto Kabwe alikataa kuchukua posho ya vikao suala ambalo lilipelekea msuguano na Spika wa Bunge Bi.Anne Makinda.Baada ya hapo ikawa ni mijadala kwa upande wa wananchi.

Kilichonisukuma kuandika makala hii leo,ni safari ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Abbas Kandoro ya kwenda katika Halmashauri ya mojawapo katika mkoa huo.Hivi ni sahihi kwa waandishi wa Habari kupewa posho na Halmashauri kwa ajili ya kuripoti taarifa ambako wala hawakualikwa na Halmashauri?Waandishi waliolipwa ni Mtangazaji wa TBC1,Mwandishi wa gazeti la Mwananchi,Mwandishi wa gazeti la Habari leo na Mtangazaji wa ITV.Kuna Uhalali gani kwa Sekretariet ya Mkoa kupokea posho kwenye Halmashauri wakati wamepata posho kwenye taasisi yao?Wakati waandishi wa Habari walikuwa mstari wa Mbele sana kupinga posho wanazolipwa waheshimiwa wabunge,vipi kwa upande wao?

Jamani hii ni nchi yetu sote.Ifike sehemu kila mtu awajibike na kufanya kinachotakiwa.Kwa mwendo huu nchi yetu haiwezi kuendelea.Katika kipindi hiki nchi iko taabani sana kifedha,lakini wakati huo huo tunaendeleza malipo hewa ambayo hayawasaidii wananchi wetu,ambao kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu.Tuache unafiki,tuseme kile tunachokitenda.
 
Hii ndiyo Tanzania tunasema yale tusiyoyaishi na kuyatenda yaan yale tuyanayoyataman ndiyo yanayoonekana kila mara kuchukua maisha yetu..
 
Nchi hii inateketea,kila kona kuna ubadhirifu kutoka ngazi ya kijiji hadi Ikulu.Tunahitaji kujikana wenyewe ili tuepukane na hali.
 
Mkuu utaniharibia ujue! Nipo Mtwara nakula posho ivooo!! Nakula kipande ya nchi japo kidogo na mimi.
 
wananchi wanauwalakini

viongozi wanauwalakini

serikali inauwalakini

kiujumla kila kitu kina uwalakini
 
Tueleze wewe uko katika nafasi gani, na kama umelipwa au la. Na kwa nini, isijekuwa ni wivu tu wa kike. Mnachanganya, tatizo la Chadema si ubaguzi katika posho, bali kuondoa kabisa mfumo huo ili kinusuru fedha za umma. Kwa kuwa mfuko haukuondolewa, waache waliobahatika walambe posho kwa mwavuli wa CCM na Shibuda wao
 
Tueleze wewe uko katika nafasi gani, na kama umelipwa au la. Na kwa nini, isijekuwa ni wivu tu wa kike. Mnachanganya, tatizo la Chadema si ubaguzi katika posho, bali kuondoa kabisa mfumo huo ili kinusuru fedha za umma. Kwa kuwa mfuko haukuondolewa, waache waliobahatika walambe posho kwa mwavuli wa CCM na Shibuda wao

Kuusema ukweli kunahitaji nafasi?Wakati mwingine tunatakiwa kujitambua na kutoa hoja ambazo zinajenga.Na kama huna la kuchangia ni vema ukapotezea.Kimtokacho mtu ndicho kimjaacho.Inawezekana unaa element za kike ndio maana unasema ni wivu wa kike.Kitu cha msingi ni kwamba niliyoyasema ni ya kweli?Na kama una nia njema na hii nchi ungesema niwasilishe hapa jamvini ushahidi.Inawezekana wewe ni miongoni mwa watu wanaofaidi posho
 
Una ushahidi kwamba kuna double payment ya posho au unachosema wewe ni kwamba vikao hivyo havistahili kulipwa posho kabisa?
 
Back
Top Bottom