Suala la Mwanamke kujenga nyumba kwa siri lipoje kisheria?

Yani hela ya mwanaume iishie kwa kuhonga mahawara na ulevi halafu hela ya mwanamke afanye maendeleo ya sharing na Mwanaume?

Ktk mazingira hayo Mwanamke akiamua kufanya maendeleo yake ni sawa tu.

Labda mwanamke afanye kwa hila kuwa yeye hana kipato anategemea kipato cha mume halafu wakati huo huo anamwibia na kwenda kujenga nyumba yake peke yake.

Lakini iwapo mwanamke akijenga nyumba kwa kipato cha jasho lake 100% ruksa

Tena wakati mwingine huna haja ya kumficha mumeo.

Sababu unatumia jasho lako Kwanini usite kuwa wazi?!
 
Naomba kujua sheria inasemaje juu ya mwanamke anayejenga nyumba kwa siri akiwa ndani ya ndoa

Sheria inaongea acheni mazoea

IMG-20210922-WA0006.jpg
 
IMG_8580.jpg
Mtoa mada soma hio 7.3 ,ndoa haiwezi kumzuia kumiliki mali yake binafsi ,kwaio jipange mwanaume usitolee macho mali ya mwanamke .
 
Naomba kujua sheria inasemaje juu ya mwanamke anayejenga nyumba kwa siri akiwa ndani ya ndoa
Chakujiuliza, anajenga kwa pesa ya nani?

Anatumia Mali zenu/zako au pesa zako kufanya ujenzi? Kama jibu ni ndio basi unayohaki yakuwa sehemu ya umiliki wa mali/nyumba hio.

Lakini ikiwa mkeo anatumia pesa zake kufanya huo ujenzi pasipo kuhusisha sehemu ya pesa zako wala zenu za pamoja. Basi anayohaki yakumiliki kwa asilimia 100% hio nyumba.

Kufanya kwasiri niswala lahofu yakutokujua kuwa mwanandoa anayohaki yakumili maliyake binafsi nje ya ile Mali ya pamoja kati yenu.

Mengine yanachagizwa na namna mnavyoishi, dhamirayake kwako, na malengo aliyonayo juu ya mwelekeo wa ndoa yenu. Lakini katika sheria hayo hayana nafasi.
 
Hapa nilipopanga mimi leo...mwenye nyumba ni mwanamke lakini baada ya mke kufariki ,nyumba inamilikiwa na mumewe na ndie anaechukua kodi
 
Back
Top Bottom