Suala la Mugalu imenifanya nigundue jinsi gani wachambuzi wengi wa soka Bongo ni bendera fata upepo

Hicho ndo tunataka, sio habari za ukabaji alafu Kati ya nafasi 5 za wazi hapati hata moja, zote anazigeuza kosakosa. Hii hatua tuliyofika ni hatua inayohitaji zaidi magoli zaidi hata ya point 3,tukiendelea kwenda na hoja za ukabaji hatuwezi toboa.Jaribu kufikiria tumefungwa mbili kavu ugenini, alafu kwa mkapa sehemu ambayo tunahitaji kupindua matokeo ,tunatengeneza Zaid ya nafasi 5 za wazi ila hatugungi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatau tulipofikia Simba kwasasa timu inatakiwa iwe makini zaidi kwa kila eneo.
Kwa mfano Al Ahly huwa wanabadilika wanakua hatari na wabaya mno wanapofika nafasi kama ya robo na nusu fainali.
Washindi wa pili(runers)kwenye makundi hatua hii ya robo unakuta ndo washindi wa kwanza kuingia hatua ya makundi nusu fainali,hatua hii timu zinabadilika sana kwakweli.
 
Umefanya vema katika kutoa maoni kwa kuambatanisha marejeo.

Mi nauliza.
Hivi kwanini hapa watu wanakwepa kuzungumzia madhaifu ya Mugalu ?

Kweli anacheza vizuri, kweli Anasaidia timu.
Mbona akina Chama Bwalya huwa madhaifu yao yanajadiriwa hapa na yanapelekea hadi kujirekebisha na wanafanya vizuri sasa.

Huyu Mugalu yeye ni nani hadi ajadiriwe kwa mazuri yake tu.

Ukigusa udhaifu wake basi unashambuliwa kwamba hujui soka wewe.

Nini iko Shida ?
Umesoma hizo screenshot, umesikiliza wachambuzi? Mbona wachambuzi wengi walikosoa. Sijajua mnatumia reference ipi. Redioni kuna wachambuzi waliomkosoa na khba wengine walimpa credit. Hata humu kuna wanaomkosoa na kuna wanaoona bado abastahili. Tatizo la wanaomkosoa kutaka kila mtu acheze ngoma wanayoitaka wao. Sisi sio nyumbu tuende sehemu moja. Kila mtu ana mtazamo tofauti latika kila jambo.
 
Wanasimba wakati tunajadili timu yetu embu tupeane taarifa,kombe la VPL pale Karume ofisi za TFF lipo salama?
Maana kuanzia jana baada ya mechi pale kwa Mkapa kumeibuka wimbi la vibaka!
View attachment 1749165
 
Hatau tulipofikia Simba kwasasa timu inatakiwa iwe makini zaidi kwa kila eneo.
Kwa mfano Al Ahly huwa wanabadilika wanakua hatari na wabaya mno wanapofika nafasi kama ya robo na nusu fainali.
Washindi wa pili(runers)kwenye makundi hatua hii ya robo unakuta ndo washindi wa kwanza kuingia hatua ya makundi nusu fainali,hatua hii timu zinabadilika sana kwakweli.
Nakubaliana na wewe mkuu, kuna watu utakuta wanasema mara bora huyu kibonde.. mara oooh sijui yule kibonde, lakini hii hatua ni ngumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani Ally Mayai na Amri Kiemba (wachambuzi waliocheza mpira) wanasemaje kuhusu Mugalu ?
tmp-cam-426967409514432553.jpg

Ngoja nikupe ya amri kiemba mkuu, Ally mayay aliongea hii kitu ya striker kuling na midfield na kumpa credit mugalu kwenye hilo. Ka kumshauli alifanyie kazi suala la scoring.
 
Kwahiyo Ikitokea umeulizwa kutoa maoni bila kuweka siasa (ambazo naona zimekukaa sana), juu ya eneo gani ambalo Simba inapaswa kulifanyia kazi Kati ya Safu ya mabeki,Kiungo na ile ya Ushambuliaji utagusia Safu ipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio kwamba naleta siasa. Maoni yangu yameelemea rasilimali watu iliyopo sasahivi.

Ila kwa swali uliloniuliza, kwa maoni yangu ni kwamba Simba inatakiwa kufanya maboresho yafuatayo:-

Kutafuta mshambuliaji hatari mmoja ambaye uwezo wake uko juu ya Mugalu na Kagere (kama tutafanikiwa kumpata, maana watu hawa ni adimu mno barani Afrika, wengi wanakimbilia Ubelgiji, Ufaransa na Uturuki na nchi zingine za ''soft Europe'').
Tukimpata huyu, basi mmoja kati ya Meddie na Mugalu tumuache.

Je, Mtu huyu awe Dube ?
Kama tukimpata Dube, itakua safi, yeye ni striker wa kisasa (Kagere na nduguye mCongo ni old fashioned) ataisaidia sana kwa nafasi ambazo timu inatengeneza.
Ana footwork nzuri na ni goal attacker mzuri (Ni Haaland wa Kizimbabwe).
Ila ana changamoto ya majeraha, lakini pia hela atakayoitaja Mzee Bakhressa itakua ni balaa.

Sehemu nyingine ni kule upande wa Zimbwe, anahitaji msaidizi ambaye angalau anamkaribia ubora, Gadiel ameshuka sana kiwango. Siku Zimbwe akiumia na tuna mechi ngumu na kubwa itakua balaa.

Upande wa Kapombe Sina shida nako sana kwa sababu Nyoni, Ame na Duchu wote ''wanaweza wakacheza'' eneo hilo. (Japokua sio kwa ubora uleule).

Nafasi ya Mkude na Mzamiru bado Sijaona mchezaji wa ndani anayeweza kuwa bora zaidi ya hao. Na kuleta asiyemzawa maana yake tutatakiwa kumuacha mgeni mmoja kati ya wale kumi wa ligi ya ndani. Bado sijaona ni nani wa kuachwa so far.

Tukiweka pembeni ''siasa'', yangu ni hayo mkuu.
 
Nirudie tena, nafasi hazizawadiwi, zinatengenezwa. Akicheza meddie timu haitengenezi nafasi kama ambavyo inafanya akicheza Mugalu. Hapa hoja yako ya kuwa-subject washambuliaji wengine kwenye nafasi ambazo Simba inatengeneza with Mugalu inakosa mashiko.

Pili nina uhakika mimi na wewe wote hatujui hao washambuliaji wengine wamekosa nafasi ngapi sasa. Kwahiyo kusema wao hawakosi kama Mugalu ni kufanya majumuisho yenye kuelemea upande mmoja.

Mwanzo nilidhani unataka Mugalu afunge magoli, baadae nimegundua kwamba kumbe magoli hayo hayatakiwi kuwa ya penati na pia yanatakiwa kuwa skillful kama ya akina Chama na Luis.
Daah mkuu unataka vitu vingi sana toka Mugalu aisee.

Halafu mkuu, Kwani Makambo ana magoli mangapi huko Horoya au unamzungumzia ''Makambo wa mwaka juzi'' ? Maana mwaka juzi hata Mugalu alikua mfungaji bora wa ligi ya Zambia.
Alafu anamuongelea dube, hii ligi ya bongo ambayo mugalu anahitaji dkk 15 tu za mchezo ili ashinde goli. Kweli wanampima mugalu kwa VPL iwe repracement kwa ajili ya champions league.
 
Japokua uwezo wa mtu kiuchambuzi hauwezi kupimwa kwa umahiri wake katika ''kupiga danadana'' na kuucheza mpira, ila mimi naomba uniambie tu uniambie hao wachambuzi wa Ulaya walisemaje kuhusu Olivier Giroud na Ufaransa yake iliyotwaa ubingwa wa Dunia ?
tmp-cam-7911851991231427904.jpg

Usipate shida mkuu, walisema hivi.
 
Tatizo raia wagumu kuelewa..Mugalu hastahili kuanza na Kagere ni bora kuliko Mugalu....Kagere muda wowote anakupa goli..angalia takwimu zake za vpl msimu huu, kacheza games chache kuliko washambuliaji wengi ila bado anakimbiza...Hii inshu ya kuwa simba ikicheza na Kagere inakuwa haitengenezi nafasi ni unazi na uongo wa kiwango cha SGR....Roho zinawasuta.

Kazi ya striker ni Kufunga..Kufunga na Kufunga..mengine mbwembwe..ni kama ilivyo kazi ya Goalkeeper ni kulinda lango mpira usiingie...Sasa unapomtetea mtu ambae hafanyi jukumu lake la kwanza effectively ni matumizi mabaya ya utetezi..

Hivi ingekuwa Manula anafungwa magoli ya kizembe (Kama vile ambavyo Mugalu anakosa magoli ya wazi), je bado Manula angeendelea kupangwa eti kisa tu ana uwezo wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma? 🤣🤣🤣🤣

Hebu kuweni serious..Mfumo wa guardiola unataka kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma..ila haujiulizi kwanii BRAVO anakaa benchi licha ya kuwa ni mzuri kwenye build up....Jibu ni rahisi, hafanyi vizuri kwenye jukumu lake mama ambalo ni kulinda goli ndio maana anakaa benchi na kapotea kabisa.

Sisi tunamshambulia Mugalu kwa kushindwa kuwa mfanisi kwenye jukumu lake la kwanza...hayo mambo ya kuwa anatengeneza nafasi nyingi sana kwa wenzie ni porojo maana hayana justifications...Ana assists ngapi?...kapiga penetration passes ngapi?...ana shots on target ngapi? au kasababisha rebounds ngapi?....

Tunapowaambia kuwa ubovu wa Mugalu unafichwa na performance ya timu muwe mnaelewa...Liverpool for the past two seasons walikuwa moto sana...Firmino alikuwa hafungi sana lakini bado hakuna shabiki wa liverpool aliyemnyooshea kidole...matokeo ya timu yaliwapa upofu...ila msimu huu mambo yamegeuka, timu ikaanza kusuasua na firmino hafungi ndipo hapo upofu wa mashabiki ukaisha wakaanza kumtaka Jotta achukue nafasi ya firmino.....ila mwanzoni ilikuwa mapambio kama yote mara firmino uwepo wake pale mbele ni faida kubwa isiyoonekana kwa macho ya kawaida na blah blah kama hizo.

Mara mia kidogo hata firmino alikuwa ana shots on target, ana assist na anawin battles kule mbele..sasa huyu Mugalu ndo kabisaa haeleweki anafanya nn kule mbele...ni kazi gani ambayo sisi hatuioni...basi sawa kocha anaiona..ila Time will tell na tutaufufua huu uzi.
 
Hapa nime kopi na ku pest, hoja ya mtoa mada hii. Unaweza kuipitia hasa aya ya kwanza na ya tatu ya mtoa mada.

"Mimi ni shabiki wa mpira na mpira ninaujua kwa kuutazama na kuucheza uwanjani. Haiitaji elimu kubwa kugundua kuwa Chris Mugalu hafai na hastahili kuanza kikosi cha kwanza kulingana na kiwango chake hasa uwezo wake wa kufunga. Bahati nzuri kwake ni kuwa udhaifu wake unafichwa na ubora wa timu.

Na kwa bahati mbaya zaidi wachambuzi wengi wa soka hapa bongo wamekuwa na 'upofu' katika uchambuzi. Analysis zao nyingi zina base kwenye matokeo. Mfano, hata kama timu ikicheza ovyo kwa dk zote 89, ila ikapata goli na kushinda dakika ya 90..Basi tegemea analyis positive kutoka kwa wachambuzi wetu.. Vice versa is true.

Vivyo hivyo kwenye swala la Mugalu, wachambuzi wetu hawajui chochote kuhusu soka. Hata uchambuzi wao juu ya viwango vya wachezaji umemezwa na matokeo ya timu. Wengi utawasikia kuwa Mugalu ni striker mwenye uwezo wa kuhold mpira na kufungua nafasi kwa wengine. Hawazungumzii kabisa ubutu wake golini.

Na mbaya zaidi wachambuzi karibu wote wana copy na kupaste opinions zao zinafanana. Katika kipindi hiki, huwezi kuta wachambuzi wanajadili weaknesses za Mugalu, badala yake wanaelezea umuhimu wake na faida yake kule mbele.Najiuliza, Hivi kama hafungi, ana umuhimu gani sasa wa kuanza?, na je kama timu isingekuwa inapata matokeo na bado Mugalu angekuwa anapoteza zile nafasi, bado wasingemuelezea udhaifu wake?...Jibu ni rahisi tu, wana chambua kulingana na matokeo.

Mfano wa pili, ni Jonas Mkude. Kwa mtu anaejua mpira na aliyeangalia ile game, ilikuwa sio rahisi kuamini kama Mkude angerudi uwanjani second half..Alikuwa flopy sana siku ile.

Cha ajabu timu imepata matokeo kwenye comments unasikia uchambuzi kuwa Mkude alifanya majukumu yake vizuri na aliiunganisha vizuri sana safu ya ulinzi na ushambuliaji..Hivi ni mkude huyu huyu aliyekuwa na pass accuracy mbovu kuliko wachezaji wote wa simba siku hiyo? Ina maana wachambuzi hamuoni udhaifu wa wachezaji kisa tu timu imepata matokeo?

Basi kama ni hivyo, hakuna kazi rahisi kama kucwa mchambuzi wa soka bongo."
Mkude kaloga hadi wachambuzi nikiona amepangwa nakuwa roho juu Mkude alikuwa yule wa miaka miwili iliyopita sio sasa
 
Tatizo la mitazamo yetu ya kibongo ni kule kuutazama ubora wa timu yako na kuacha kuangalia ubora wa yule unayecheza nae.

Kocha mzuri anaitazama timu anayocheza nayo ipo vipi na anaandaa strategies kadri ya kila timu ilivyo.

Mugalu anaweza asifunge lakini akawa anaibuka mshindi wa mapambano mengi ya hewani akiruka na mabeki.

Mugalu ni kama Drogba enzi zile. Anaanza kukabia kule kule mbele, ana nidhamu nzuri ya kimchezo na utulivu wa mechi kubwa.
Acha kumfananisha Drogba na Mugalu. Drogba alikuwa hapotezi nafasi kipuuzi kama Mugalu. Drogba ilikuwa nafasi moja goli.
 
Simba watafute mshambuliaji aina ya Okwi ambaye ana uwezo wa kupangua beki na kufunga.
Usajili wa Simba umejikita kwenye viungo washambuliaji zaidi, msimu ukiisha tuongeze washambuliaji wachezaji kama Ajibu tuachane nao kwani tunao wenhi
 
Acha kumfananisha Drogba na Mugalu. Drogba alikuwa hapotezi nafasi kipuuzi kama Mugalu. Drogba ilikuwa nafasi moja goli.
Naongelea mifumo mkuu sijaongelea uwezo binafsi.

Naongelea majukumu yao uwanjani kama Namba tisa wenye jukumu la kuficha mipira na kuwachezesha shadow strikers.
 
Mimi ni shabiki wa mpira na mpira ninaujua kwa kuutazama na kuucheza uwanjani. Haiitaji elimu kubwa kugundua kuwa Chris Mugalu hafai na hastahili kuanza kikosi cha kwanza kulingana na kiwango chake hasa uwezo wake wa kufunga. Bahati nzuri kwake ni kuwa udhaifu wake unafichwa na ubora wa timu.

Na kwa bahati mbaya zaidi wachambuzi wengi wa soka hapa bongo wamekuwa na 'upofu' katika uchambuzi. Analysis zao nyingi zina base kwenye matokeo. Mfano, hata kama timu ikicheza ovyo kwa dk zote 89, ila ikapata goli na kushinda dakika ya 90..Basi tegemea analyis positive kutoka kwa wachambuzi wetu.. Vice versa is true.

Vivyo hivyo kwenye swala la Mugalu, wachambuzi wetu hawajui chochote kuhusu soka. Hata uchambuzi wao juu ya viwango vya wachezaji umemezwa na matokeo ya timu. Wengi utawasikia kuwa Mugalu ni striker mwenye uwezo wa kuhold mpira na kufungua nafasi kwa wengine. Hawazungumzii kabisa ubutu wake golini.

Na mbaya zaidi wachambuzi karibu wote wana copy na kupaste opinions zao zinafanana. Katika kipindi hiki, huwezi kuta wachambuzi wanajadili weaknesses za Mugalu, badala yake wanaelezea umuhimu wake na faida yake kule mbele.Najiuliza, Hivi kama hafungi, ana umuhimu gani sasa wa kuanza?, na je kama timu isingekuwa inapata matokeo na bado Mugalu angekuwa anapoteza zile nafasi, bado wasingemuelezea udhaifu wake?...Jibu ni rahisi tu, wana chambua kulingana na matokeo.

Mfano wa pili, ni Jonas Mkude. Kwa mtu anaejua mpira na aliyeangalia ile game, ilikuwa sio rahisi kuamini kama Mkude angerudi uwanjani second half..Alikuwa flopy sana siku ile.

Cha ajabu timu imepata matokeo kwenye comments unasikia uchambuzi kuwa Mkude alifanya majukumu yake vizuri na aliiunganisha vizuri sana safu ya ulinzi na ushambuliaji..Hivi ni mkude huyu huyu aliyekuwa na pass accuracy mbovu kuliko wachezaji wote wa simba siku hiyo? Ina maana wachambuzi hamuoni udhaifu wa wachezaji kisa tu timu imepata matokeo?

Basi kama ni hivyo, hakuna kazi rahisi kama kucwa mchambuzi wa soka bongo.​
Nonsense
 
Mi pia naungana na wewe,
Huenda kocha anamuandaa kwa matumizi ya baadae.
Mugalu siyo mzuri kivile lakini ukimweka kwenye mizani moja na kagere ni afadhali Mugalu Mara 100 ukilinganisha na kagere! Wote tulishuhudia alichokifanya kagere kwenye mechi na Al Ahyl!!
 
Mugalu siyo mzuri kivile lakini ukimweka kwenye mizani moja na kagere ni afadhali Mugalu Mara 100 ukilinganisha na kagere! Wote tulishuhudia alichokifanya kagere kwenye mechi na Al Ahyl!!
Kumbe angeanza Mugalu tungewafunga Al-Hilaly kama goli 3 hivi.
Na yote yangewekwa kambani na Mugalu.
Na tusingefungwa hata goli moja kwakuwa Mugalu anakabia juu.
 
Haya jana Kagere ameanza na nazani mmeona kilichotokea. Kuna watu utawasikia,
1. mara oooh kagere sio mzuri akicheza lonely striker...
2. mara ooh akianza kagere timu haitengenezi nafasi.....
3. mara ooh mtibwa sio kipimo kizuri.

sasa tumpime kagere kwa kipimo gani? ikiwa CCL Mugaru kapata play time ya kutosha tangu mtoano ila ana goal 2..Kapata play time ligi ya ndani ila bado anazidiwa goals na Kagere.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom