Suala la mpaka ktk ziwa Nyasa liwe kielelezo cha umoja na utaifa wetu siyo la rais Jakaya peke yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suala la mpaka ktk ziwa Nyasa liwe kielelezo cha umoja na utaifa wetu siyo la rais Jakaya peke yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Penguine, Oct 6, 2012.

 1. P

  Penguine JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Mzozo kuhusu Suala la Mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa ni miongoni mwa masuala ambayo yanagonga vichwa vya watu, taasisi na tawala mbalimbali duniani kwa sasa. Zaidi ni kati ya Utawala wa Rais JK waTanzania na Utawala wa Rais JB wa Malawi.

  Kama ilivyo ada, yawezekana yapo mataifa yanayofurahia mzozo huo ukue na kukomaa mpaka moshi ufuke kwasababu ni muuhimu kwa mauzo ya bidhaa zao ikiwa ni pamoja na silaha zitakazouzwa endapo vita itatokea (Mungu aepushie mbali).

  Suala la mpaka huo linasemekana kugusa maagano, mapatano na sheria za kimataifa. Ningependa kusikia Taasisi zetu za masuala ya kisheria (kwa mfano TLS , LHR hata UDSM School of Law na Ile Sehemu ya Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa zinatuelimisha kuhusu hili. TAASISI HIZI SIZISIKII WALA SIZIONI KUFANYA HIVYO. Hii siyo vita ya JKpeke yake. Kama suala hili liko chini ya taratibu zilizowazi kuhusu mipaka ya namna hiyo HOFU YETU YA NINI KUELIMISHANA? Au taratibu za uhusiano wa kimataifa zinakataza?

  Nilitegemea pia kuwasikia Wasemaji Wakuu Wa Vyama vya Upinzani katika Masuala ya Kimataifa wakitolea maoni na kumpa nguvu Rais kuhusu Suala la Mpaka huu, SIWASIKII WALA SIWAONI KATIKA HILI!

  Simaanishi kwamba waliongelee kwa namna ambayo ni yakukuuza mgogoro bali kwa namna itakayoonesha kuwa inapokuja kwenye masuala ya kitaifa, tuko pamoja.

  Ni maoni tu.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
 3. P

  Penguine JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Invisible,
  Asante kwa article hiyo sikujua kwamba wenzetu wameanza kukutana. Lkn hatujachelewa.
   
 4. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sasa wengine waseme nini, walisema wakaambiwa ni wapinzani ndio wanaleta chokochoko
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ukweli ni kwamba sisi wa Tanzanzania tunafanya zulma dhidi ya malawi, lile ziwa ni mali yao lotee, mipaka yote inaonyesha hivyo.
   
 6. B

  Bwaga ya moyoni Senior Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Umezungumza vizuri sana. Katika mambo kama haya, ni vizuri zaidi kuwa na msimamo wapamoja. Kimsingi wenzetu wako united sana katika hili na ni janja ya Joyce Banda kuhakikisha hata kama katika mazungumzo yanayoendelea Malawi itashindwa na kukubariana na msimamo wa Tanzania kuwa mpaka unapita katikati ya Ziwa, basi yeye asipate kulaumiwa kuwa amemega sehemu ya nchi yake kwa Tanzania. Kumbuka watakuwa na uchaguzi 2014 so asipowashirikisha wapinzani, basi suala la mpaka litamuangusha mwaka 2014. Kulipeleka suala hili International Court of Justice (ICJ) kunatokana na msingi huo huo kuwa kwa vile Tanzania haiwezi kubadilisha msimamo wake, na haswa baada ya kutoa new map, basi ni bora wasiendelee kupoteza pesa za walipa kodi wao katika mazungumzo ambayo wanaamini hayana tija so ni bora waende ICJ.

  Nilipata kusoma makala moja inayoonyesha kuwa nchi zote mbili wanazo hoja za msingi sana na Joyce Banda anaelewa hilo kuwa hoja yetu ni ya msingi ingawa nchi yake pia inayo hoja ya msingi na hapa ndipo unapotokea ugumu wa kulimaliza suala hili bila mtu watatu ambaye, kama ambavyo wenzetu walivyoamua, ICJ ni sehemu sahihi kabisa. Joyce anaelewa kucheza na akili za wapinzani wake kwani anavyowashirikisha, na amekuwa akifanya hivyo tangu mzozo uanze, anauhakika kuwa hata kama wao watashindwa na hatimaye mzozo huu uliodumu kwa miaka 50, ukaamriwa na mpaka ukatambulika kuwa unapita katikati kama msimamo wetu ulivyo, basi atakuwa amewafunga midiomo wote wenye nia yakusema utawala wake umemega sehemu ya nchi yao kwani jibu lake litakuwa rahisi tu kuwa: Wote tulishiriki kikamiifu katika mazungumzo so kwakifupi, ni sheria yakimataifa ndio ilaumiwe.

  Kwetu sisi hapa siasa zetu kidogo siyo zile zakushirikishana kwenye mambo mazito yanayogusa maisha ya watu wote bila kujali itikadi zao na huwa tunafanya hivyo kwa maneno tu huku tukiwaachia wachache wakitupa lectures kana kwamba wao ndio wenye akili nyingi kiasi chakuweza kufikiri kwa niaba ya watanzania wote. Lakini kwa upande mwingine, huu ni mtaji wakisiasa kwani chama tawala kinajivisha kitanzi kwakutowashirikisha wapinzani. Ninahakika, tukishindwa hii case ICJ, itakuwa ndio mwisho wa CCM. Inawezekana CCM wanaelewa kuwa wapinzani wenyewe, ukiacha Chadema, ndio hao hao CCM B so hawana sababu za kuambiwa kwani hata mawazo ya wafanye nini na wakati gani (mfano CUF na V4C Arusha), ni mpaka waambiwe na chama baba. Katika mazingira kama haya, sitarajii kuona CCM ikiwashirikisha vijana wake katika hili kwani vijana hawa (except Chadema) ni wakuambiwa tu kile ambacho baba ameamua kufanya.
   
 7. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kulinda mipaka ya nchi ni zaidi ya kulinda shamba lako la migomba ambapo jirani yako akiwa mbabe unaweza kuamua kumuachi hatua tano au kumi hivi...Mipaka ya nchi inafundishwa kuanzia shule ya chekechea mpaka University ya wananchi husika na inakua seheme ya imani yao na kama ujuavyo imani huishi hata kwenye damu ya mhusika...Hivyo kukubali au kukataa sehemu ya ardhi yako kuchukuliwa ni suala shirikishi na lisilojali itikadi maana hapa hakuna Mtanzania na mtanzania saaana..wote ni watz kwa maana ya usawa kitaifa hasa suala la eneo la nchi hivyo tutumie hili suala kuwa kipimo cha uzalendo wetu na kiu uongozi bora maana hapandipo majuto ya kuchagua viiongozi wezi yanapoanzaga...Taifa halina pesa viongozi wanaiba kila wanachokiona mbele polisi wanaua raia wenzao kwa maslahi ya majambazi viongozi..Sasa itakapobidi tuingie vitani tutataabika sana kiuchumi ila mpaka mwisho tutawarudia majambazi Ccm nakuwaangamiza vibaya sana...Shime watz wenzangu
   
 8. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mpiinzani wa Joyce banda anaitwa undule mwakasungura sasa kwa tabia ya Ccm na polisi kuwauwa wanyakyusa katika migogoro kama hii kuna haja ya kuhamia malawi maana nimesikia hata kyela anaitaka bora tuende malawi ambapo tutatendewa haki kuliko huku ambapo wanatusaka watuue kila kuchapo...Tunawatakia maisha mema our former Tanzanians sisi sasa hivi ni wamalawi
   
 9. P

  Penguine JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Malafyale Gwakisa Mwandule,
  Ni kweli kwa trend ya vifo vya jamaa zenu inatia shaka na kuleta simanzi kiasi cha baadhi yenu (kama wewe)kutaka kupata hifadhi kwa Dada Joy Banda, lakini nakusihi kwa uzi huu tujadili utaifa kwanza Gwakisa. Naona una mawazo chanya sana ktk suala hili. Ipo siku tutaleta uzi kuhusu trendi ya mauaji na mateso ya watu wa kabila lako kama ni bahati mbaya au planned termination. Karibu Gwakisa ktk mjadala wa mpaka wa nchi hizi mbili.

   
 10. P

  Penguine JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Bwaga ya Moyoni,
  Unabwaga yaliyoko moyoni.

  Nawasubiri WanaJF wengine tujadili suala hili. Uko wapi Nnauye Jr, zitto, mnyika, pasco,mwanakijiji, preta,ngambongali,jason bourne, kiranga, phD, etc?
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Wapinzani tulishirikiana na serikali kwenye swala zima la kuwalipua mafisadi ila uyo JK akajitokeza na kubeza kuwa wapinzani wanadandia hoja za ccm.
  Nashauri tuanze kushirikiana kuwatambua wamiliki wa mabilion huko uswiss, pia tuonyeshe ushirikiano kuwabaini wale waliotorosha wanyama hai alafu ndo tuanze kushurikiana kwenye maswala ya kitaifa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 13. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #13
  Oct 6, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Tatizo kikwete mwenyewe alijimilikisha huu mgogoro, wakati watanzania wazalendo wakitoa misimamo thabiti juu ya mipaka yao jk akawaita ni wapinzani.!
   
 14. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe 100%, lakini mara zote serikali inakimbilia wanasheria wa Kimataifa ka REX attorney, ambao walituingiza katika balaa la Richmond. Viongozi wa serikali ya JK wanapenda sakata hili kwa manufaa yao binafsi
   
 15. Jagarld

  Jagarld JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 1,537
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa mkuu,hata Membe alilishupalia sana swala hili mwanzon lakini baada ya kubaini msimamo wake uko tofauti na boss wake kanywea kama hayupo vile,sidhan kama jk ni muumini mzuri wa ushauri nje na ikulu au watu wake wa karibu
   
 16. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Umaja wa kitaifa uliokosa nguzo ya kuwaongoza.
   
 17. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kimsingi ndugu yangu pengins mambo ya umoja wa kitaifa ni kama vazi lililokusitiri ukiruhusu kujitenga hasa katika issue ya ardhi ni kukubali kuelekea hadharani ukiwa uchi...so jambo la msingi ni kuachana kwanza na tofauti zetu tunusuru ardhi yetu kwa gharama yooyote ile then tushughulike na tofauti zetu ila kwa kuwa suala hili limejitokeza kipindi hiki wakati siasa yetu inachemka ni vizuri tukapambana na maadui wote wawili ikibidi katika mikutano ya M4C Agenda ya mpaka iwe ya kwanza bila kuathiri mtazamo wa Adui wa kwanza ni CCM wa pili ni Malawi...Kisha tuendelee kuweka sawa masuala ya kiuongozi inteernally ikiwa ni pamojaa na kupanga baraza la mawaziri la CDM litakaloweza kutuandaa kiuchumi wakati wa machafuko na wakati wa neema tofauti na majambazi wanavyotudhoofisha kiuchumi hasa kama tutaingia vitani na malawi. Hii ni kwasababu tutakua na uchumi mbovu hata uwanja wa mapambano hautakua wakuridhisha japo tutakua tunawajibika kutetea ardhi yetu kwa gharama kubwa...Hii ni sawa na kkusema tumeshambulliwa kwanza na mafisadi kabla malawi hajaanza kutushambulia hivyo mafisadi wanawasaidia malawi
   
 18. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Point yako ni nzuri sana hata kama tuna tofauti lakini linapokuja swala lenye maslahi ya kitaifa inabidi utaifa tuuweke mbele kwani mabadiliko yoyote yatakayotokea yatatuathiri wote kama taifa.Kitendo cha baadhi ya taasisi kuwa kimya ni dhahiri wanapiga makelele kwenye mambo ambayo yanawafanya wapate pesa kutoka kwa wafadhili wao na sio maslahi ya nchi.
   
 19. M

  Mayunga96 Member

  #19
  Jan 24, 2014
  Joined: Oct 11, 2013
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwani wewe ni mtanzania toka lini...kwende kule mwehu mkubwa wee!!!
   
 20. M

  Mayunga96 Member

  #20
  Jan 24, 2014
  Joined: Oct 11, 2013
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na siku nyingine usome sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu mipaka ya kwenye maji we mkimbizi mavi sawa?? Halafu ndio uje humu kunya.
   
Loading...