Suala la Mo naona Jeshi la Polisi bado linatufanya watanzania ni wajinga. Toka wazungu na sulf hadi dereva taxi (kada wa CCM) rafiki wa Dr. Shika

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
FB_IMG_1559147770642.jpg
FB_IMG_1559146981435.jpg


Kuna saa Akili inakataa kabisa kufanya kazi ya kutengeneza Logic. Huyu ni dreva- Tex ambaye anahusishwa na Tukio la kumteka MO.

Rais Magufuli aliwahi kusema watanzania sio wajinga. Ni kwa nini Rais Magufuli aseme kauli kama hii? Bila shaka anaona uzembe na watu kutokuwa Weledi katika eneo flan.

Nachanganyikiwa Surf tuliyoiona kwenye CCTV camera na hatimaye ikatelekezwa tukaikamata hatujajua bado mmiliki ni nani?

Mbona ukitaka kujua ilitengenezwa Lini na wapi, na nani wa kwanza kuinunua, akamuuzia nani mpaka mmiliki wa Mwisho utamjua?

Tupo imara kiasi gani katika maswala ya Kiuchunguzi? Motives ya watekaji ilikuwa ni nn? Si wamuulize mtekaji hao watekaji walikuwa wanataka nn kwake? Maana tukijua watekaji walikuwa wanataka nini watu wa uchunguzi wanaweza kutengeneza madhanio ya watekaji.

Hii Kesi ilikuwa imepoa kabisa na watu walishamsau Mo na maswahibu yake ya kutekwa. Kwa kifupi kesi hii ilikuwa imekumbwa na natural death, tumeenda kufufua maiti sasa inatuletea mainzi bila sababu.

Vyombo vyetu vya habari mpaka Leo havijawahi hata kufikiria kufanya mahojiano na MO katika swala nyeti kama hili la kutekana Nchini.

Akili inakataa kufanya connection kabisa.... Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama visilale hadi Watekaji wote wakamatwe. Itatusaidia sana hasa kuondoa lawama ambazo Serikali imekuwa ikitupiwa kila kukicha.

Saidianeni na Interpol ikishindikana iteni hata CIA ili Ku clear hizi lawama. Duniani Tumezidiana hata Sisi waalimu sio kila kitu unaweza kufundisha mada nyingine ili zipate ufanisi tunatumia Mbinu ya kumwalika Mgeni.... Hata hapa ambapo watekaji wameanza kutuzidi maarifa tunapaswa kuwaita wengine wenye maarifa makubwa na vifaa vya kisasa zaidi.

Kuna faida kufanya hivyo, kwanza kutawaongezea vyombo vyetu vya uchunguzi Weledi kwa kuwa watakuwa wanajifunza pia kwa wenzao mbinu na watajua vifaa gani vinahitajika lakini pia tukiwapata watekaji tutakuwa tumeisaidia sana Serikali inayopakwa matope bila sababu.

Ole Mushi
0712702602
 
Hata miaka ile ya Dr. Ulimboka tulishuhudia mkenya akikamtwa na kuhusishwa na lile tukio. Ni wakati huo pia na sisi wa mikoani ndipo tulipomfahamu Mchungaji/ Askofu Gwajima maana tulijulishwa huyo mtuhumiwa alikamatiwa kanisani kwake alipoenda kutubu dhambi zake.
 
Shida ni polisi wanaoaminiwa wanweza kuplan wengi ni low charge (upstairs), so wanafanya vitu kwa level ya uelewa wao!! Wanawadharirisha polisi wenye uelewa mpana!!
IGP ni Mwanasheria kitaaluma lakini hii movie alichemsha sana, picha ya Sulf kaitoa kwenye mtandao anasema ni CCTV labda alimaanisha sisi TV.
 
Kipindi kile enzi za mwalimu ilikuwa ikitokea tukio lolote la kiharifu, polisi walikuwa fasta sana kuwatia watu ndani harakaharaka huku wakiendelea na uchunguzi. Ikikuwa ni kosa kubwa mnoo kwa masaa 24 kupta baada ya tukio na hakuna "hata mtu mmoja aliyetupwa ndani". Naona sasa polisi wamerudia mbinu zile zile za mwaka 47
 
Tuendelee kusali Mungu atatujulisha ukweli wa saga zima yeye ndio interpol na CIA
 
Back
Top Bottom