Kama una uwezo wa kuteua na huna uwezo wa kutengua basi wewe sio Rais, huu ni uvunjaji wa wazi kabisa wa katiba ya nchi
 
Wishful thinking....

Kwa mujibu wa katiba jamaa anaenda Chattle 2025!

Atakuja rais mwingine mpya!

Huyo rais jamaa kamshikia kichwa?

Kwanza jamaa anamjua huyo rais atakae chukua nchi badala yake?Hamjui

Sasa huyo rais akiwa kichaa kisawasawa atamkata pumbu hadharani!

Sasa wewe kama bado unadhani ni wishful thinking then think again!
 
Katiba imefanyiwa marekebesho na Raisi hivi sasa na itasema kuwa;

"HAKUNA ALIYEPEWA UWEZO WA KUTEUA AKANYIMWA WA KUTENGUA"

Kwa maana hiyo hata Chief Justice anaweza kutenguliwa tu.
Yaani hapo ndipo napaipendea TZ nchi yangu. Ikulu ni kila kitu mtakiwa muelewe kabisa kabisa. kwa lugha nyingine ni muhimili uliojichimbia chini zaidi ya mingine!!!!!!!!!!!! Mwagahulila ago!!!!
 
Bara kuna lisu mwanasheria ambaye hajawahi pingwa nahuyu wa zanziba ,namsubili lisu anasemaje....uchuro uchuro uchuro
 
Start with your evidence to support those two claims.

Kuwa anataka IST gari simple tu.

Kuwa kakagua mahesabu kaona IST inatumia mafuta vizuri kuliko land cruiser

Ukinipa hizo evidence nami nakupa zangu.haya anza kutoa.😁😁😁😁
Those are hypotheticals to challenge your notions.

Hypotheticals do not ned evidence, that's why they are hypotheticals.

I did not make a claim, I posed a hypothetical.

You made a claim. Know the difference.

Where is your evidence?
 
(Anaandika Muheshimiwa mwenye heshima zake Othman Masoud Othman aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar)

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa FBI nchini Marekani, James Comey, ameandika katika kitabu chake A HIGHER LOYALTY maneno ya kuleta tafakuri kubwa. Amendika _“it is very hard to leave a group of people who are committed only to doing the right thing”_. Alikuwa anaeleza ugumu wanaopata watu waadilifu katika utumishi wa umma kutenda mambo kwa kufata sheria na taratibu. Mara nyingi hujikuta wapo peke yao. Athari ya wanayokutana nayo ni kuzidisha hofu kwa wengine wenye ujasiri na hatimaye kuendelea kuporomoka kwa maadili ya utendaji wa umma.

Katika hili la CAG, imeonyesha wazi kwamba wanasheria katika ngazi mbali mbali hawakutimiza wajibu wao.

Ibara ya 144 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeeleza wazi kama ifuatavyo:

"144 (1) bila ya kuathiri masharti mengine yaliyomo katika ibara hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Jamhuri ya Muungano atalazimika kuacha kazi yake atakapotimiza umri wa miaka siti au umri mwingine wowote utakaotajwa na Sheria iliyotungwa na Bunge”

“(2) Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu aweza tu kuondolewa katika madaraka ya kazi yake kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake(ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote) au kwa sababu ya tabia mbaya, au kwa kuvunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, na hataweza kuondolewa kazini ila kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya [4] ya ibara hii”

Ibara hiyo ya Katiba inaeleza wazi kwamba umri wa kuacha kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni miaka 60. Hata hivyo Bunge limepewa uwezo wa kubadili umri na sio muda wa kazi wa Mdhibiti na Mkaguzi. Ni kanuni ya msingi ya kutafsiri sheria kwamba neno linapokuwa na maana mahsusi, haliwezi kutaftiwa tafsiri nyengine mbadala inayopingana na maana mahsusi ya neno hilo. Ibara ya
144 (1) ilikusudia kuweka umri wa kustaafu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kama ulivyowekwa umri wa kustaafu wa Majaji chini ya ibara ya 110 ya Katiba ambao nao ni miaka 60.

Ibara ya 144 haitoi mwanya kwa Bunge kutunga Sheria ya kuweka muda wa kuendelea na kazi kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ambao utamfanya aondolewe kazini kabla ya muda uliowekwa na Katiba au kuongezwa na Sheria [miaka 65].
Hili linathibitishwa zaidi na ibara ya 144 (6) ya Katiba inayosema:

“ Mtu ambaye ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu au aliyepata kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hawezi kuteuliwa kushika au kushikilia madaraka ya kazi nyingine yoyote katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano”

Kwa ibara hiyo, Profesa Musa Assad hawezi hata kukaimu nafasi yoyote katika utumishi wa umma, na hivyo atakuwa amestaafishwa katika utumishi wa umma kabla ya umri wa kustaafu. Hakuna kiumbe cha namna hiyo katika utumishi wa umma. Ikitokea hivyo, tafsiri sahihi ni kuwa mtu huyo amefukuzwa au kukatishwa utumishi wake. Na hilo, ni batili ya wazi kwa vile inakiuka masharti ya ibara ya 144(2) na (3) ya Katiba.

Sheria au tafsiri inayotoa mwanya kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuondolewa kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria na kwa matakwa ya Rais bila ya kufuata masharti ya wazi ya utaratibu wa kumuondoa kabla ya kufikiksha umri wa kustaafu chini ya ibara ya 144(3) na (4), inavunja msingi wa kinga ya kikatiba [security of tenure].

Inasikitisha sana unapoona wanasheria katika mazingira kama haya, ambapo kuna mgongano baina ya Katiba na Sheria, wanaanza kutafsiri Sheria kuipindua Katiba na sio kutafisiri Katiba ili kuipindua Sheria inayopingana na Katiba kama inavyoelekezwa na ibara ya 64(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Mwanasheria yeyote aliyemshauri Rais kumuondoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kutumia Sheria inayoweka masharti ya vipindi bila kuzingatia masharti ya wazi ya ibara ya 144(1) ya Katiba amemkosea sana Rais, amewakosea sana Watanzania na ameifedhehesha sana taaluma ya Sheria.

Fedheha kubwa zaidi kwa taaluma ya sheria ni pale wanasheria watapoanza kutofautiana katika kutafsiri masharti hayo ya wazi ya Katiba kwa itikadi au mirengo ya kisiasa au kwa baadhi kufanya hivyo kwa kupotosha ili kumfurahisha mteuzi.

Athari ya jambo hili haitokuwa kwa Profesa Mussa Assad. Athari kubwa ni katika mfumo wetu wa kikatiba, utawala wa sheria na matumizi ya mamlaka ya umma.

OTHMAN MASOUD OTHMAN
 
Mwanasheria yeyote aliyemshauri Rais kumuondoa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kutumia Sheria inayoweka masharti ya vipindi bila kuzingatia masharti ya wazi ya ibara ya 144(1) ya Katiba amemkosea sana Rais, amewakosea sana Watanzania na ameifedhehesha sana taaluma ya Sheria.
Othman, niwie radhi Nakusahihisha kidog, sipangiwi katu! alisikia akisema Jiwe! Hakuna cha kushauriwa, dictator huwa hashauriwi! Othman tell the truth! Kutoa kauli kuwa mpya asijifany muhimili ni wazi haya ni maamuzi ya jiwe binafsi!
 
Katiba ina ibara mpya:

"HAKUNA ALIYEPEWA UWEZO KUTEUA AKAZUIWA KUTENGUA".
 
Othman, niwie radhi Nakusahihisha kidog, sipangiwi katu! alisikia akisema Jiwe! Hakuna cha kushauriwa, dictator huwa hashauriwi! Othman tell the truth! Kutoa kauli kuwa mpya asijifany muhimili ni wazi haya ni maamuzi ya jiwe binafsi!
Pia kasome ibara ya 36 ya Katiba ili akili ikuingie vizuri ili uje uendelee kutoa mapovu zaidi.
 
Doh mpaka kwenye history wanamfuta hawana hata aibu
Watanzania tuamke, Katiba ya mwak 1977 ina-limit mihula miwili ya miaka mitanomitano, ndiyo maana kabla ya hiyo katiba muda wao ulikuwa unabadilika.

Heb tupitie historia kidogo.
View attachment 1252969
View attachment 1252970
Yaani prof. Assad anavyochukiwa, hadi picha yake kwenye website (National Audit Office of Tanzania » The CAG) walishafuta kwenye orodha ya ma-CAG.

-Je, kafikisha miaka 60? (Mussa Juma ASSAD Born : 6 October 1961)
-Je, sheria ilibadilishwa lini kustaafishwa kabla ya miaka 60? (Mandatory retirement also known as enforced retirement or compulsory retirement)
-Je, anaumwa ama ametiwa hatiani na tume ya maadili?
-Je, Rais amefuata katiba inavyosema?

View attachment 1252957
View attachment 1252749
 
Pia kasome ibara ya 36 ya Katiba ili akili ikuingie vizuri ili uje uendelee kutoa mapovu zaidi.
A Dictator on the Rise? How President Magufuli is Now Showing His True Colours

“We as Tanzanians are not accustomed to this ... Since independence, we have not seen the army on the streets like this,” said lawyer Fatma Karume.

A Dictator on the Rise? How President Magufuli is Now Showing His True Colours
 
Hili swala la Prof.Assad limeivusha CCM kutoka serikali inayopambana na ufisadi hadi kuwa serikali inayotetea ufisadi.
 
Back
Top Bottom