Suala la Mishahara ya wafanyakazi wa serikali: Tuzungumze mazuri na mapungufu katika suala hili nyeti, tuweke siasa pembeni

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,261
7,396
Naomba kwanza suala mishahara ya watumishi wa serikali lieleweke tu kuwa si la kulichukulia mzaha mzaha na kulibeba tu kuhamia nalo majukwaani!

Kuna mambo makubwa matatu hapa yamejitokeza tuyachambue kwanza:

Annual increment:

suala hili namlaumu President Magufuli kwa kuwa amelichukulia mzaha mzaha: hili lipo kisheria hata kama angepunguza kiwango tungemuelewa lakini kufuta kabisa ni kama amedharau kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi katika serikali yake katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya watanzania

Kupanda madaraja wafanyakazi:

Hili tuseme ukweli mie ni mmoja wa walipandishwa daraja wakati huu wa awamu ya 5: Tatizo lilitokea kuchelewa kuhakikiwa na watu wa UTUMISHI wanapokuwa wanachakata upandishwaji wa madaraja. Inawezekana watumishi ni wachache pale wizarani lakini kuna watu pale wanakwamisha sana kiasi cha kuonekana kama Rais ndio anazuia kumbe kuna majitu mavivu, yanajiskia, maonevu kama kuna mwanamke mmoja anaitwa ADERA! huyu kuna siku atapigwa na wafanyakazi! anadharau sana na mvivu wa kazi balaa! halafu ndio mkubwa kwa wenzie hapo wizarani! mtoeni nafasi hiyo mpuuzi huyu

Malimbikizo na stahiki mbalimbali:

Kuna uzembe mkubwa unafanyika ofisi ya utumishi hapo wizarani kwani wanafanyia kazi madai mbali mbali kwa kujiskia! yaani inategemea mtu kaamkaje siku hiyo ndio anafanya kazi! ukifika ofisin Mtumba pale ofisi imejaa ma fomu ya malimbikizo mpaka yametapaakaa chini, wanachelewa sana kuhakiki matokeo yakr kazi zinapandana wanaamua kuyashiti tu mafomu, hiki kitengo cha approvers kwa kweli wanakatisha sana tamaa naomba serikali iwaangalie kwa jicho la tatu! ndio wanaomkwamisha RAIS.

Suala la ubaguzi katika nyongeza za mishahara:

Awamu hii ya 5 haya yamefanyika kwa WANAJESHI wa JWTZ, USALAMA WA TAIFA na walio karibu na president tu. hawa wenzetu hasa JWTZ amewaongezea hela nyingi tena zaidi ya laki 3 mwezi Agosti

Hapa namlaumu President Magufuli kwa kusikiliza ushauri wa watu wenye nia mbaya na kumchafulia kwa watanzania! ipo hivi, wafanyakazi wote ni wa muhimu! sasa ikianza suala la huyu mupe huyu muruke kwa kweli inamkosesha BARAKA hata RAIS mwenyewe maana hakuna atakayekuombea mema hasa kama mtu anajua ana fanya kazi kwa bidii mwisho wa siku anapewa mwingine ananyimwa mwingine!

Wanasiasa msichezee na maisha ya wafanyakazi wa serikali:

Nionavyo mie Rais Magufuli ni kama anatuchukia wafanyakazi maana muda mwingi ametumia jukwaa kuwasema wafanyakaz na kuwanyima stahiki mbalimbali! pamoja na kuahidi atawajali kabla hajatoka madarakani hili naona kama siasa lakini WANASIASA wa upinzani naomba sana suala la stahiki za wafanyakazi msilibebe kama agenda kubwa itatuletea matatizo mengine makubwa mbele ya safari hasa kwa President Magufuli maana naona kama anongeza hasira kwa wafanyakazi baada ya kuona mnatusemea sana majukwaani.

Naunga mkono maendeleo kwa kila mtanzania ila sio kunyima haki ya mfanyakazi kwa kisingizio cha kujenga barabara! mambo yote yaende kwa pamoja tena kwa kiwango maana hata MAREKANI wanajenga mabarabara mpaka leo na maisha ya wafanyakazi yanaenda!

Suala la kuwajaza Wanajeshi kwenye kazi za kiraia:
Hili suala linachukuliwa kama kunyima haki za ajira kwa wafanyakazi wengine. Tukumbuke wanajeshi ni mojawapo wa wanaolipwa mishahara minono sana nchi hii, lakini bado wanapewa na kazi za uraiani ambazo zinaleta mgogoro mkubwa kiutendaji mpaka inafikia watu wanaamua tu kuweka migomo baridi.

Ombi langu kwa President Magufuli:
kama wafanyakazi tumekukosea sehemu tunaomba utusamehe! usifikiri Mungu anapenda haya yanayofanyija kwa wafanyakazi hasa wastaafu ambao wanasotea mafao yao, wanaodai malimbikizo yao, waliokwama kupanda madaraja kwa ujinga na uzembe wa watu wa utumishi!

Hali ni mbaya kwa wafanyakazi. Mungu halali!
 
Kiukweli wafanyakazi mkimpa kura magufuli mtakuwa mmekosea sana

Kwanza kawaonyesha nyie si kitu ila vitu ndio kitu

ikiwa miaka mitano ajawafanyia lolote na uchaguzi umekuja ajawafanyia chochote mnategemea nini badae ni maumivu balaa yani atawanyoosha mpaka mtajuta

Yani akipita tegemeeni ongozeko la kodi, tegemeeni maovyo ovyo mengi yakufanya maslahi yenu yapotee tu kwaiyo huu ni mda wakumwambia mtoto, mama, baba, bibi na babu, shangazi na mjomba kuwa magufuli hatufai akija tena umu ndani tutalala njaa wambieni bila woga
 
Tatizo wananchi nao wakisikia wafanyakazi hatujaongezewa mishahara wanafurahia kama vile wanavyofurahia watu kutumbuliwa halafu siku nyingine unasikia "brother hali ngumu huku kijijini, ntoe hata buku saba" ...
Mi mwenyewe nimekaa standby hapa namsikilizia Magufuli,akipandisha tu Mishahara na Mimi napandisha Kodi ya Nyumba zangu!!
 
Juzi kwenye kampeni anasema huwezi kuongeza mishahara ukaacha kujenga barabara

Nadhani kasahau watumishi wa serikali ndio elite group la wapiga kura.

Subiri atakiona cha mtema kuni.
Unforgetable
 
Tatizo wananchi nao wakisikia wafanyakazi hatujaongezewa mishahara wanafurahia kama vile wanavyofurahia watu kutumbuliwa halafu siku nyingine unasikia "brother hali ngumu huku kijijini, ntoe hata buku saba" ...
Kuna watu wakisikia huyu ni mwajiriwa mioyo inawapasuka. Hakuna raia wa kutetea watumishi.
 
Watumishi nyie sindio mmewakata wagombea nafasi mbalimbali mnajipendekeza ACHENI MSIONGEZEWE MISHAHARA NA MEKO AKIONGEZA MISHAHARA BABA WA TAIFA ATAFUFUKA VYAMA VYA WAFANYAKAZI WENYEWE KUTWA KUSIFIA SIFIA

MNAKATA WAGOMBEA NA NAMBA TUNAISOMA WOTE BORA USIMKATE NA TUENDELEE KUISOMA
 
Back
Top Bottom